15 Mungu Mwenye Haki, Uweza na wa Utendaji
1
Mungu mmoja wa kweli, ambaye ni wa milele,
Alizungumza maneno Yake, viumbe kuwa hai.
Alinena na ikawa, Aliamuru na ikasimama.
Vumbi liligeuka kuwa wanadamu.
Aliwalea viumbe Wake,
na uhai ukajaza mbingu na dunia.
2
Alitoa sheria, Akatenda maajabu.
Alimwongoza mwanadamu na kumtunza.
Lakini mwanadamu alijiachilia kwa uovu,
mchafu na mpotovu, asiyestahili kuangaliwa.
Mnyenyekevu katika mwili, Mungu alimsamehe,
Akatelekeza hadhi, Akakabili udhalimu.
Baada ya miaka thelathini ya maisha magumu,
Aliteseka msalabani na kuondoka kimya kimya.
Damu Yake ya thamani, Alimwaga katika dhabihu,
kumkomboa mwanadamu na kuacha upendo wa kweli.
3
Umeme umeangaza kutoka Mashariki,
wingu jeupe limeshuka katika Sinim.
Akiwa amejawa haki, Mungu amerejea duniani,
Yeye ni Mwenyezi Mungu mwenye mwili.
Anaanzisha enzi mpya, Analeta kazi mpya,
Anaonyesha ukweli kumwokoa mwanadamu, Akihukumu wakati wote.
4
Binadamu wamejawa na uasi na upinzani,
na Mungu anahisi huzuni nyingi, chuki, karaha nyingi moyoni Mwake.
Akilia machozi ya damu, Anaonyesha uvumilivu mkubwa.
Nani anayeweza kuufariji moyo Wake unaoomboleza?
Mwenye hasira ilhali mwenye huruma, Yeye huruzuku.
Anafanya kazi na kusubiri na hutoa moyo Wake wa kweli.
Maua yamechanua na kufa mara ngapi?
Mara nyingine tena, bata bukini wanaruka kwenda kusini na kurudi.
Mwili Wake usio na hatia unadhalilishwa,
Moyo Wake ukiumizwa karibu kutoweza kupona.
Anateseka peke Yake, bila mahali pa kupumzika,
Akifanya kazi mchana na usiku, bila kujali chakula au usingizi.
Na moyo wa mama Yake mwenye fadhila, Analia machozi na damu,
lakini maneno Yake ya kweli yanadhihakiwa.
Kwa siri akiwa amejificha, Anaendeleza kazi Yake.
Hatimaye, Anapata kundi la watu
ambao ni wa moyo mmoja na akili moja naye.
Kwa siri akiwa amejificha, Anaendeleza kazi Yake.
Hatimaye, Anapata kundi la watu
ambao ni wa moyo mmoja na akili moja naye.
Haki, uweza vikionyeshwa katika mwili,
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu!