43 Vitu Vyote Viko Mikononi Mwa Mungu

Nimeyasema maneno haya: Kile Nilichosema lazima kihesabiwe, kile kilichohesabiwa lazima kikamilishwe, na hili haliwezi kubadilishwa na yeyote.

1 Kama ni kile Nilichosema katika wakati uliopita au Nitakachosema katika siku za usoni, yote yatatimia, na wanadamu wote wataliona hili. Hii ni kanuni inayoelekeza maneno na kazi Yangu. Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu? Chochote Nisemacho hufanyika, na miongoni mwa wanadamu, ni nani aliyepo anayeweza kuyabadilisha mawazo Yangu? Yaweza kuwa agano Nililofanya juu ya dunia? Hakuna chochote kinachoweza kuuzuia mpango Wangu.

2 Mimi huwepo wakati wote katika kazi Yangu na vilevile katika mpango wa usimamizi Wangu. Ni mwanadamu gani anaweza kuingilia? Je, sio Mimi binafsi Niliyetengeneza mipango hii? Kuingia katika hali hii leo, bado haipotei kutoka kwa mpango Wangu au Nilichoona mbele; yote iliamuliwa Nami zamani sana. Ni nani miongoni mwenu anaweza kufahamu mpango Wangu wa hatua hii? Watu Wangu wataisikiliza sauti Yangu, na kila mmoja wa wale wanaonipenda kwa kweli atarudi mbele ya kiti Changu cha enzi.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 1” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 42 Muda Upotezwao Hautawahi Kuja Tena

Inayofuata: 44 Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp