23. Vita

Na Zhang Hui, China

Jina langu ni Zhang Hui, na mnamo mwaka wa 1993 familia yangu yote ilikuja kumwamini Bwana Yesu. Nilikuwa mwenye kutafuta kwa shauku kubwa, kwa hivyo nikawa mhubiri haraka. Mara nyingi ningetembea kila mahali kwa makanisa mbalimbali kufanya kazi na kuhubiri. Baada ya miaka michache, niliacha kazi yangu na kuanza kumtumikia Bwana wakati wote. Hata hivyo, kwa sababu fulani isiyojulikana, imani na upendo wa ndugu zangu ulipoa polepole, na wivu na ugomvi uliongezeka kati ya wafanyikazi wenza. Nilihisi pia kuwa roho yangu ilikuwa ikififia, na sikuwa na kitu kilichosalia cha kuhubiri kuhusu. Mnamo mwaka wa 2005, mke wangu alipata saratani, na alifariki mara baada ya hapo. Jambo hili lilikuwa pigo kubwa kwangu na nilizidi hata kudhoofika. Siku moja, nilienda kukaa nyumbani kwa binamu yangu na nilikutana na dada wawili huko waliohubiri injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Baada ya muda wa siku kadhaa za ushirika na mjadala, nilikuja kuamini kweli kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi na kwamba Yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mwili. Kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, moyo wangu wenye kiu ulinyunyiziwa na kuruzukiwa, na nilifurahia utamu wa kazi ya Roho Mtakatifu, nikifahamu ukweli mwingi na siri nyingi ambazo sikuwa nimewahi kufahamu hapo awali. Hata hivyo, kama vile tu nilikuwa nimezama katika furaha ya kukutana tena na Bwana, majaribu na mashambulio ya Shetani yalininyemelea kuliko wakati wowote mwingine …

Siku moja alasiri, nilikuwa nikitia ibada ya kiroho kwenye vitendo palipotokea bisho la ghafla mlangoni. Nilipoufungua, niliwapata Mchungaji Li Yang na Mfanyikazi mwenzangu Wang Jun kutoka kanisa langu la zamani wakisimama nje. Nilishtuka kwa mshangao, na kujiuliza: “Wanafanya nini hapa? Je, inawezekana kuwa wamepata habari ya imani yangu katika Mwenyezi Mungu? Awali, kina ndugu ambao walikuwa watafutaji wazuri walipoanza kumwamini Mwenyezi Mungu, Mchungaji Li na Mfanyikazi mwenza Wang waliwatisha kwa uvumi na kuchochea familia zao kuwashurutisha kuepukana na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Walifanya kila walichoweza kuwazuia kumfuata Mwenyezi Mungu. Leo, sijui ni aina gani ya mbinu watakazotumia kunisumbua.” Niliwasalimu na kuwaketisha. Baadaye kidogo, binti yangu Xiaoyan na mwanangu Dayong walirudi pia. Nilikanganyikiwa: Watoto wangu walikuwa wamesema walikuwa wenye kazi nyingi sana, hivyo kwa nini wawili hawa waje nyumbani leo? Je, inawezekana kuwa Mchungaji Li aliwataka waje? Ilionekana kana kwamba Li Yang na Wang Jun walikuwa wamekuja wakiwa tayari! Nilimwomba Mungu haraka: “Mwenyezi Mungu! Leo, wamekuja haswa kunizuia na kunivuruga. Mungu, kimo changu ni kidogo sana. Nakuomba Uniongoze na Unisaidie kukabiliana nao. Niko tayari kuwa shahidi Kwako!” Baada ya kuomba, moyo wangu ulitulia. Wakati huo, Li Yang alitabasamu ghafla tabasamu lenye hila na kusema: “Ndugu Zhang, nimesikia kwamba sasa unaamini katika Umeme wa Mashariki. Je, jambo hilo ni kweli? Bila kujali pana ukweli kiasi gani katika Umeme wa Mashariki, hatuwezi kuukubali. Ndugu Zhang, sote tumemwamini Bwana kwa muda wa miaka mingi, na tumehubiri na kufanya kazi kwa ajili Yake. Sote tunaelewa vizuri kuhusu ukweli kwamba Bwana Yesu alisulubiwa na kuwa sadaka ya dhambi, jambo ambalo limetukomboa kutoka kwa dhambi zetu. Tumefurahia pia neema kubwa, na amani na furaha tuliyopewa na Bwana, kwa hivyo lazima tudumishe jina na njia ya Bwana nyakati zote. Hatuwezi kumwamini Mungu mwingine. Je, si kuondoka kwako kutoka kwa Bwana Yesu na kumwamini Mwenyezi Mungu ni usaliti wa Bwana?”

Nilisema kwa utulivu: “Ndugu Li, tunapozungumza, tunapaswa kuwa wasio na mapendeleo na wenye busara, kuthibitisha ukinzani wetu kwa ushahidi na kutotoa shutuma zisizo na mantiki. Je, umechunguza njia ya Umeme wa Mashariki? Je, umesoma maneno ya Mwenyezi Mungu? Hujawahi kuuchunguza, kwa hivyo unawezaje kufikia uamuzi kwamba nimemsaliti Bwana kwa kukubali Umeme wa Mashariki? Je, unajua ukweli unatoka wapi? Je, unamjua anayeonyesha ukweli? Bwana Yesu alisema, ‘Mimi ndiye njia, ukweli na uhai’ (Yohana 14:6). Mungu ndiye ukweli! Unawezaje kusema kuwa bila kujali ni ukweli kiasi gani upo katika Umeme wa Mashariki, hutaukubali? Je, si hivyo ni kuupinga ukweli kwa makusudi, na kumpinga Mungu? Tungefanya hivyo, je, tungeweza hata kuchukuliwa kama waumini katika Bwana? Kusema ukweli, kwa sababu wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini wanaipinga peupe na kuilaani kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, nilipoanza kumwamini Mwenyezi Mungu pia mimi niliogopa kuwa huenda nikawa mwenye kosa, na kwamba pengine naweza kuwa nimepotoka. Lakini, baadaye nilisoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu, na nimegundua kuwa yote ni ukweli, kwamba yanafichua siri nyingi, kama vile siri ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka 6,000 na ukweli wa ndani wa hatua tatu za kazi, siri za Mungu kupata mwili, hadithi ya kweli ya ndani ya Bibilia, na mengineyo. Mkanganyiko na matatizo ambayo nimekumbana nayo katika miaka yangu mingi ya kumwamini Bwana yote yametatuliwa kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kadiri ninavyozidi kusoma maneno ya Mungu, ndivyo ninavyozidi kuhisi kwamba haya ni maneno ya Roho Mtakatifu, kwamba ni sauti ya Mungu. Ninaamini kabisa kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na kwamba Bwana anaonekana kwetu! Ndugu Li, Ndugu Wang, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu mmoja. Kumwamini Mwenyezi Mungu ni kukaribisha ujio wa Bwana! Hebu tutafakari juu ya jambo hilo. Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi, watu wengi waliondoka hekaluni ili wamfuate. Wakati huo, bila shaka kulikuwa na watu wengi waliowahukumu wakisema kwamba walikuwa wamemsaliti Yehova Mungu na walikuwa na hatia ya ukanaji wa imani. Sasa sote tunajua kuwa ingawa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ilikuwa tofauti na kazi ya Yehova Mungu ya kutoa sheria, na jina la Mungu lilibadilishwa pia, Bwana Yesu na Yehova Mungu ni mmoja na Mungu mmoja. Kumwamini Bwana Yesu sio kumsaliti Yehova Mungu, lakini hakika ni kwenda mwendo sawa na nyaya za Mungu na kupata wokovu Wake. Kwa kweli, wale waliomwamini Yehova Mungu lakini hawakumfuata Bwana Yesu ndio waliokuwa kwa kweli wakimkana Mungu na kumsaliti. Jambo lilo hilo linatumika leo. Hata ingawa kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho sio sawa na kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, na jina la Mungu limebadilika, Mwenyzi Mungu na Bwana Yesu ni mmoja na Mungu mmoja. Huu ni ukweli usiokanika. Katika Enzi ya Neema, kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ilisamehe tu dhambi za mwanadamu, lakini haikumsamehe mtu tabia zake za shetani na asili yenye dhambi. Kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ni kutatua tabia za shetani za mwanadamu na asili yake yenye dhambi, kumwokoa kikamilifu, kumfanya afumue ushawishi wa Shetani na kupatwa na Mungu. Ni wazi kwamba, hatua hizi mbili za kazi ni za kukamilishana, zimeunganishwa kwa karibu na huongezeka uketo zinapoendelea. Jambo hili kweli linafanywa na Mungu mmoja. Imani yangu katika Mwenyezi Mungu sio usaliti wa Bwana Yesu. Ni kuenda mwendo sawa na nyayo za Mwana-kondoo. Tukimwamini tu Bwana Yesu na kukataa kumfuata Mwenyezi Mungu, sio tu kwamba tutakuwa sawa na Mafarisayo waliomwamini Yehova Mungu pekee na kumkataa Bwana Yesu, wakipoteza wokovu wa Mungu, lakini pia tutapatwa na adhabu ya Mungu. Huu tu ndio upinzani na usaliti wa kweli wa Bwana! Je, hudhani hivyo?”

Li Yang aliponisikia nikisema haya, alionekana kuwa na wasiwasi sana, na Wang Jun alijaribu kutuliza hali kwa kusema: “Mzee Zhang, Mchungaji Li anakupa ushauri huu kwa sababu ya kuhisi kuwajibikia maisha yako, akihofia unaweza kuchukua njia isiyo sahihi. Umemwamini Bwana kwa muda wa miaka mingi na mmetumikia Bwana pamoja. Kwa miaka mingi, kustahimili mema na mabaya haya yote hakujakuwa jambo rahisi. Wewe ni mzee katika kanisa letu na umetoa mengi kwa ajili ya kazi ya kanisa. Ndugu zetu wote wanakuheshimu na kukuamini, lakini wewe kuacha kanisa na kumwamini Mwenyezi Mungu kumekuwa jambo la kuwakatisha tamaa sana! Mzee Zhang, tafadhali rudi upesi!”

Li Yang kisha alitangulia, akijaribu kunibembeleza, akisema: “Ndugu Wang yupo sawa. Umefanya kazi kwa bidii miaka hii yote. Je, unawezaje kupoteza kwa kutakabari sifa njema na hadhi uliyoijenga kanisani? Ni aibu mno! Rudi sasa. Kila mtu anakusubiri urudi! Kanisa letu limeanzisha makazi ya kustaafu, tumeunda mahusiano na makanisa ya nchi za nje na wanatupa msaada wa kifedha. Ukirudi, tutakupa gari mara moja. Ikiwa unataka kusimamia makazi ya kustaafu, au kusimamia kanisa, au kuendelea kutunza fedha za kanisa, hiyo ni juu yako. Chochote unachotaka kufanya ni sawa!” Kadiri nilivyozidi kuwasikiliza, ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa pana jambo lisilo la kawaida. Waliyokuwa wakiyasema hayakuonekana hata kidogo kama mambo ambayo waumini katika Bwana wangeyasema. Majaribu ya ibilisi Shetani ya Bwana Yesu kama yalivyosemwa katika Biblia yalinijia akilini: “Tena, Ibilisi akampeleka hadi kwenye mlima mrefu sana, na kumwonyesha falme zote za dunia, na fahari yao; Na akasema kwake, Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu” (Mathayo 4:8-9). Je, si mambo hayo yote waliyokuwa wakiyasema yana hisia sawa kabisa, sauti sawa na yale Shetani alisema? Je, si haya yalikuwa majaribu ya Shetani? Kusudi lao katika kunishawishi na umaarufu, hadhi, na utajiri lilikuwa kunifanya nikane njia ya kweli na kumsaliti Mwenyezi Mungu. Huu ulikuwa ulaghai wa Shetani! Nilikuwa nimemwamini Mungu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na hatimaye nilikuwa nimekaribisha kurudi kwa Bwana. Singeweza kudanganywa na ulaghai wa Shetani sasa la sivyo ningejutia maisha yangu yote. Niligundua basi kwamba Mungu alikuwa akiniongoza, akinielekeza, ili kwamba niweze kutambua njama zao za hila. Nikitafakari haya, nilisema kwa ukali, “Je, si nimemwamini Mungu miaka hii kwa matumaini ya kukaribisha kurudi Kwake? Kwa kuwa sasa Amerudi, chaguo langu la pekee linaweza kuwa kwenda pamoja na Mungu. Msijaribu kunishawishi tena. Sitarudi tena kwenye dini.”

Wakati huu, binti yangu aliniambia akitokwa na machozi, “Baba. Tafadhali tusikilize! Mama alifariki hivi majuzi na tayari tunateseka ya kutosha. Ukiendelea kuamini katika Umeme wa Mashariki, tutawakabilije ndugu kutoka kanisa letu katika siku zijazo? Ndugu zetu watatuacha!” Nilipowaona watoto wangu wakilengwa na machozi, nilihisi maumivu na mateso moyoni mwangu. Nilifikiria kuhusu jinsi walivyokuwa wakihuzunika kwa sababu walikuwa wamempoteza mama yao kipindi kifupi kilichopita, na jinsi wangechekelewa na kutelekezwa kwa sababu ya imani yangu katika Mwenyezi Mungu. Kwa kweli sikuwa na moyo mgumu wa kuwaruhusu kupitia mateso zaidi. Nilihisi kukanganyikiwa sana moyoni mwangu: Ningekubali masharti yaliyowekwa na Li Yang na Wang Jun kurudi kwenye dini, familia yangu ingeweza kuishi kwa amani; nisingefuata kupata mwili kwa Mungu kwa mwisho aliyekuja miongoni mwa wanadamu ili kuwaokoa wanadamu, jambo hilo lingekuwa usaliti wa Mungu, na ningepoteza nafasi yangu ya wokovu. Nilikuwa katika mtanziko kuhusu jinsi ya kuchagua. Katikati ya maumivu haya kile nilichoweza tu kufanya ni kumlilia Mungu kimoyomoyo: “Ee Mungu, nimekabiliwa na hali mbili mbaya za kuchagua na moyo wangu ni dhaifu. Ninakuomba Unipe imani na nguvu ili niwe huru kutokana na usumbufu wao na kuwa thabiti katika imani yangu kukufuata.” Baada ya kuomba, nilifikiria kuhusu maneno kadhaa ya Mungu ambayo nilikuwa nimeyasoma siku chache hapo awali: “Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo…. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo!” (“Sura ya 17” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mwenyezi Mungu yalinipa nguvu na kutumika kama ukumbusho kwamba lazima nijifunze kuwa na utambuzi. Kile nilichokuwa nimekumbana nacho siku hiyo kilikuwa kimejawa na udanganyifu na ulaghai wa Shetani. Walitumia hadhi, pesa, na hisia zangu mwenyewe kunijaribu na kunishambulia, wakisababisha vurugu moyoni mwangu wakiwa na lengo la kunifanya nimsaliti Mungu. Singeweza hata kidogo kuanguka katika mtego wa Shetani au kusumbuliwa sana na hila zake! Kwa hivyo, niliwaambia watoto wangu, “Xiaoyan, Dayong, nimechunguza jambo hili na nina uelewa. Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa kweli, na maneno Yake na kazi Yake ndiyo ukweli na njia ya kweli. Kwa muda wa miaka mingi tumetamani kurudi kwa Bwana, na leo tumepata nyayo za Mungu na njia ya kweli. Jambo hili ni la thamani zaidi kuliko kitu chochote. Hatuwezi kuacha njia ya kweli kwa sababu tu tunaogopa kuachwa na watu wengine. Wakituacha, ikiwa hawatutaki tena, hakuna chochote cha kutisha kuhusu jambo hilo. Watu daima wanaweza kuendelea kuishi baada ya wengine kuwaacha, lakini tukimwamini Mungu, na hatutafuti au kuchunguza njia ya kweli, tukipoteza nafasi yetu ya kunyakuliwa na Bwana na tufukuzwe na kuondolewa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, tutaangamizwa. Hakika tutakumbana na baa na kuadhibiwa! Je, maisha yetu yangekuwa na maana gani basi? Xiaoyan, Dayong, hamwelewi. Ikiwa mngechunguza kazi ya Mwenyezi Mungu kwa dhati, mngegundua kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi.” Li Yang na Wang Jun walipoona jinsi nilivyokuwa thabiti katika imani yangu, walichoweza tu kukifanya ni kuondoka kwa mfadhaiko usioweza kutatuliwa.

Siku chache baadaye, Li Yang na Wang Jun walikuja nyumbani kwangu tena. Wakati huu hawakunihimiza nirudi kanisani, lakini badala yake walitumia ndoa kunijaribu. Li Yang alisema, “Ndugu Zhang! Mke wako alifariki, binti yako ameolewa, na mtoto wako hayuko nyumbani. Uko peke yako tu. Kwa kweli unapaswa kuwa na mtu hapa wa kukupikia. Dada Wang kutoka kanisa letu pia hana mchumba sasa, na ni mwenye mali kiasi. Kanisa letu linaweza kuwasaidia nyinyi wawili kuoana, na kisha mnaweza kumtumikia Bwana pamoja. Je, maoni yako ni gani? Unapaswa kutafakari jambo hilo zaidi. Ndugu zetu kanisani wanakuombea, wakitumaini kuwa utarudi hivi karibuni. Lazima usifuate njia hiyo kuingia gizani!” Dada Wang alinipigia simu jioni hiyo, na katika kipindi cha mawasiliano ya simu alinibembeleza mfululizo nirudi kanisani. Alisema pia kwamba ikiwa nilikuwa na upungufu wa pesa ya ndoa ya mwanangu, yuani 100,000 au 200,000, ninahitaji tu kukubali…. Nilipomsikia akisema haya, na nilipofikiria jinsi Dada Wang alivyokuwa mzuri daima kwa familia yangu na mara nyingi alikuwa amemtunza binti yangu, nilihisi shukrani kubwa kwake. Nilikanganyikiwa kwa sababu nilijua kuwa Dada Wang alikuwa amekuja kunishauri kutokana na wema wa moyo wake na kwa kweli sikutaka kusema chochote ambacho kingemsononesha, kwa hivyo kwa moyo mzito, nilisema, “Dada Wang, najua kuwa umeitunza familia yangu daima, na ninakushukuru kwa ajili ya jambo hilo.” Baada ya kumaliza mawasiliano yetu ya simu, nilihisi vita vikiendelezwa moyoni mwangu. Nilikuwa nimemheshimu Sista Wang siku zote, lakini leo nilikuwa nimesononesha hisia zake na nilihisi vibaya sana kuhusu jambo hilo! Hata hivyo, ulikuwa ulinzi wa Mungu ambao uliniokoa kutoka kwa kushawishiwa na maneno yake na kumsaliti Mwenyezi Mungu.

Siku moja, nilikuwa nikifanya kazi mashambani Mchungaji Li aliponipata na kuniambia: “Ndugu Zhang, hata ikiwa hutajijali mwenyewe, lazima uwajali watoto wako. Dayong amechumbiwa hivi majuzi, na familia nzima ya mchumba wake inamwamini Bwana. Wakigundua kuwa unamwamini Mwenyezi Mungu, je, bado watamruhusu aolewe ndani ya familia yako? Je, si jambo hilo litakuwa balaa kwa mipango ya ndoa ya Dayong? Unapaswa kutafakari kuhusu jambo hilo zaidi.” Niliposikia kile Mchungaji Li alikuwa akiseme, nilijiwazia: “Ili kunirudisha kanisani, wanatumia hata ndoa ya mtoto wangu kunitishia. Je, kukubali kwangu kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kuna uhusiano gani na ndoa ya mtoto wangu? Zaidi ya hayo, mwanangu na mchumba wake wanapendana sana, kwa nini wasifunge ndoa kwa sababu tu ninamwamini Mwenyezi Mungu?” Kwa hivyo, nilimwambia kwa utulivu mwingi: “Kama mtoto wangu atafunga ndoa au la yote yako mikononi mwa Mungu, na jambo hilo halina uhusiano wowote na imani yangu katika Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa nimeamua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerejea, nitamfuata mpaka mwisho. Watoto wangu wanaweza kuwa hawajaelewa jambo hili bado na tuna suitafahamu yetu, lakini siku moja watanielewa.”

Siku moja, nilienda kwenye duka la mwanangu la kutia weko kwa umeme na kuona kuwa alikuwa amelala kitandani kwake siku nzima na hafanyi kazi, kwa hivyo nilishangaa na kumuuliza kuna nini. Alionekana mwenye huzuni na kusema kwa sauti ya chini, “Baba, mchumba wangu alipiga simu na kusema kwamba ikiwa umeamua kuamini Umeme wa Mashariki, basi hatafunga ndoa nami.” Kusikia haya kwa kweli kulinishtua na kunikasirisha, na niliwaza: “Li Yang na wengine wanachukia kwamba ninamwamini Mwenyezi Mungu na imetosha kwamba wananishambulia peke yangu. Je, wangewezaje kutumia kitu muhimu kama ndoa ya mwanangu kunitishia?” Nilipomwona mwanangu akiwa amekata tamaa sana, nilihisi vibaya sana. Machozi yalikuwa yamejaa machoni pangu. Mwanangu aliendelea, “Yeye pia anasema kwamba usiporudi kanisani, basi ikiwa bado ningetaka kufunga ndoa, lazima ningetoa ahadi tatu kwake. Kwanza, lazima ningevunja uhusiano wetu wa baba na mtoto. Pili, singeweza kukutunza katika uzee wako. Tatu, ningepaswa kukata uhusiano wote wa familia nawe. Baba, tafadhali rudi kanisani kwa ajili ya familia yetu.” Maneno ya mwanangu yaliingia moyoni mwangu kama kisu. Nilijiwazia: “Kwa sababu tu naamini katika njia ya kweli, wamemlazimisha mwanangu kukata uhusiano nami. Kwa nini ni vigumu sana kuamini katika njia ya kweli?” Nilijizuia kulia na kumwambia mwanangu, “Mwanangu, lazima nimwamini Mwenyezi Mungu na ninakubaliana na madai ya mchumba wako. Sitawahusisha katika jambo hili tena kuanzia sasa na kuendelea. Ishini maisha ya furaha pamoja.” Kisha niligeuka na kuondoka dukani, lakini nilipokuwa nikitembea barabarani, sikuweza kuzuia machozi tena. Mara nilipofika nyumbani, nilipiga magoti chini na kulia kwa sauti kubwa: “Ee Mwenyezi Mungu! Nina maumivu mengi sana! Ee Mungu, najua hii ndio njia ya kweli na kwamba Umekuja, na siwezi kukufuata. Lakini tangu nilipokubali kazi Yako ya siku za mwisho, watu wamenishambulia mara kwa mara, na sasa mwanangu hata anataka kuvunja uhusiano wetu wa baba na mtoto. Ee Mungu! Kimo changu ni kidogo sana, na siwezi hasa kustahimili haya peke yangu. Ninakuomba Uniongoze na Unipe imani, ili niweze kusimama kidete….” Baada ya kuomba, nilifungua kitabu changu cha nyimbo na kusoma wimbo huu wa maneno ya Mungu: “Unapokabiliwa na mateso ni lazima uweze kuweka kando masilahi ya mwili na usifanye malalamiko dhidi ya Mungu. Wakati Mungu anajificha kutoka kwako, ni lazima uweze kuwa na imani ya kumfuata Yeye, kudumisha upendo wako wa awali bila kuuruhusu ufifie au kutoweka. Haijalishi anachofanya Mungu, ni lazima utii mpango Wake na uwe tayari kuulaani mwili wako mwenyewe badala ya kulalamika dhidi Yake. Wakati unakabiliwa na majaribu, lazima umridhishe Mungu, ingawa unaweza kulia kwa uchungu au uhisi kusita kuhusu kuacha kitu unachopenda. Huu tu ndio upendo wa kweli na imani” (“Jinsi ya Kukamilishwa” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipokuwa nikisoma maneno ya Mungu, nilimhisi Mungu akinifariji na kunitia moyo, Akinipa imani na kuniruhusu kuelewa mapenzi Yake: Mungu anatarajia nimtegemee, nidumishe imani naye na sio kumsaliti bila kujali ni hali gani mabaya au majaribu yanaweza kunifika. Niliwaza kuhusu wafanyikazi wenzangu kutoka kwa kanisa langu la zamani waliokuwa wamekuja tena na tena kunishambulia mara kwa mara na kunishinikiza zaidi na zaidi, lakini kila wakati nilipokuwa kwenye lindi la mateso, mradi tu nilimwomba Mungu na kumtegemea Mungu kwa kweli, maneno ya Mungu yalinipa nuru kila wakati na kunielekeza, yakinipa nguvu na kunionyesha njia ya vitendo. Sikuwa peke yangu hata hivyo, kwa kuwa Mungu alikuwa karibu nami kila wakati. Wakati huo, nguvu ilirudi tena moyoni mwangu, na nikawa tayari kuvumilia uchungu na kuachana na vitu ambavyo nilithamini zaidi ili kumridhisha Mungu—singemsaliti Mungu hata kidogo na kurudi nyuma.

Siku iliyofuata, Dada Gao na Dada Zhao kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuja nyumbani kwangu, na niliwaambia kuhusu yaliyokuwa yamejiri katika siku chache zilizopita. “Ndugu, unahisi vipi kuhusu mambo haya ambayo yametokea?” Sista Gao aliuliza. Niliwaza kwa muda mfupi, na kusema, “Mwanzoni, nilidhani Mchungaji Li na wale wengine walikuwa wakitenda kwa manufaa yangu, ingawa walikuwa hawajachunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na hawakuelewa. Lakini sikuwahi kufikiria wangetumia kitu muhimu kama ndoa ya mwanangu kunitishia. Jambo hili ni ngumu sana kwangu kulielewa.” Dada Zhao kisha akasema, “Ndugu, unaonaje tukisoma kifungu cha maneno ya Mungu? Mwenyezi Mungu alisema, ‘Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. … Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu, hata hawakaribii kumridhisha Mungu, na wanarusha tu maneno matupu!’ (“Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yanafichua asili ya kweli ya vita vinavyoendelezwa katika ulimwengu wa kiroho. Tunapokumbana na mambo kama hayo, nje inaonekana kana kwamba viongozi wa kidini wanatushambulia mara kwa mara, lakini kwa kweli, vita vinaendelezwa katika ulimwengu wa kiroho, na Shetani anashindana na Mungu juu ya mwanadamu. Kwa kweli, viongozi wengi wa madhehebu ya kidini wanakubali mioyoni mwao kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, lakini kwa sababu kazi ya hukumu kupitia maneno ambayo Mungu hutekeleza katika siku za mwisho hayapatani hata kidogo na dhana zao na mawazo yao, na inaharibu ndoto yao ya kubarikiwa na kuinuliwa tu hadi mbinguni, wanapinga kwa ukaidi na kukataa kukubali kazi mpya ya Mungu. Zaidi ya hayo, wanaogopa kwamba watu wengi zaidi wakikubali kazi ya Mwenyezi Mungu basi watapoteza hadhi yao na riziki yao, na kwa hivyo wanafanya yote wanayoweza kuwalazimisha watu na kuwazuia kumgeukia Mwenyezi Mungu, wakiwafanya waache njia ya kweli na kumsaliti Mungu. Kwa kweli, wao ni mfano wa Shetani katika ulimwengu wa kiroho na, kwa kweli, kuvuruga kwao kwa watu kumgeukia Mungu ni Shetani kujaribu kuwaangamiza watu. Alimradi tunaweza kutambua dhamira na motisha inayosababisha matendo na mienendo yao, basi tutaweza kuelewa kabisa kiini chao. Ayubu alipokuwa akipitia majaribu, macho ya watu ya kimwili yaliwaambia kwamba wezi walikuwa wakiondoka na mali ya Ayubu, lakini katika ulimwengu wa kiroho Shetani na Mungu walikuwa wakiweka dau. Wakati huo, ingawa Ayubu hakujua kwamba vita vilikuwa vikiendelea vikali katika ulimwengu wa kiroho, alichagua kuvumilia maumivu hayo yote na hata kulaani siku ambayo alizaliwa badala ya kumlaumu Mungu. Bado alitukuza sana jina la Yehova na kuwa shahidi kwa Mungu, na hivyo kumwaibisha Shetani na kujipatia sifa za Mungu. Kuzingirwa sasa na Shetani, ingawa tumepitia maumivu ya vitisho na kuachwa na tumepoteza raha za muda mfupi za mwili, tumedumisha njia ya kweli, tumekuwa washahidi kwa Mungu na kupata sifa ya Mungu. Maumivu ambayo tumepitia yamekuwa ya maana sana!” Niliposikia maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa dada huyo, moyo wangu ulichangamka, na kusema, “Naam, nilikuwa mjinga hapo awali na sikuwa nimeelewa kabisa asili ya wafanyikazi wenzangu kutoka kanisa langu la zamani. Nilidhani walikuwa wakitenda kwa manufaa yangu. Ni leo tu ndipo ninaelewa kuwa wao ni Shetani halisi wa maisha. Ni kwa kupitia ushirika huu tu ndiyo sasa nina utambuzi kiasi kuhusu hali ya kweli ya vita katika ulimwengu wa kiroho. Ingawa bado sielewi ukweli na kuna mambo fulani ambayo bado sijaelewa kabisa, kupitia njia hii nimejionea binafsi Mungu akiniongoza na kunilinda, na haya yote yamekuwa baraka ya Mungu kwangu.” Dada hao wawili kisha wakasema kwa furaha, “Kwa kweli, shukrani na ziwe kwa Mungu! Wakikuja tena kukusumbua, omba zaidi, na unaweza kumshinda Shetani kwa kumtegemea Mungu!” Kwa kujawa na imani, niliamkia kwa kichwa kwa maafikiano.

Asubuhi moja, wafanyikazi wenzangu kadhaa kutoka kanisa langu la zamani walikuja kunitembelea tena, na nilimwomba Mungu haraka moyoni mwangu anipe imani, hekima na ujasiri. Mchungaji Li papo hapo alinitishia, akisema, “Ndugu Zhang, usipotoka Umeme wa Mashariki, basi kanisa letu litakuacha na halitakuruhusu kuwa na mawasiliano yoyote tena na ndugu zetu.” Nilimwambia, “Mnaweza kuniacha ikiwa mnataka, lakini natumaini kwamba mnaweza kuwajibikia maisha ya kina ndugu zaidi ya elfu moja kanisani. Mnaweza kutokubali kuwa Bwana amerudi, lakini msijaribu kuwazuia kina ndugu kuchunguza na kukubali njia ya kweli. Angalia hali ya sasa kanisani—kina ndugu wanahisi dhaifu na waliovunjwa moyo. Wengine wamekwenda kutafuta kazi mahali pengine na wengine wameacha kanisa na hawaamini Bwana tena, na kuna mifano mingi ya watu kuwa na pepo. Ni dhahiri kuwa kanisa limepoteza utunzaji na ulinzi wa Bwana. Halafu angalia hali yetu sisi wahubiri—hakuna hata chembe cha nuru mpya katika mahubiri yetu, kila wakati tunahubiri mambo ya zamani yasiyo na upya wowote na kina ndugu hawajaruzukiwa hasa. Je, jambo hili halistahili kutafakariwa na kufikiriwa sana? Je, haistahili tutafute ili kupata ukweli wa jambo hilo?” Baada ya kusema hayo, moyo wangu ulihisi kusisimuka na niliwaambia kwa moyo safi, “Sisi sote hapa ni wafanyikazi wenza wakuu wa kanisa, na tungefanya vizuri kudhukuru kwa muda mfupi: Sisi huzungumza kuhusu kuchunga kondoo wa Bwana siku nzima, lakini Bwana amerudi kutekeleza kazi mpya na kuonyesha maneno mapya, na bado hatuyatafuti au kuyachunguza hata kidogo, na hatuwaongozi ndugu zetu kukubali kunyunyiziwa na kulishwa na maneno ya Mungu. Badala yake, tunawazuia kina ndugu kuchunguza njia ya kweli kwa njia yoyote inayowezekana—kwa kufanya hivi, je, hatuwasababishi ndugu zetu kufa kwa ajili ya kiu na kuchoka kwa kuwaweka wakifungwa kwa dini? Je, watu ambao wana uwezo wa kufanya hivi ni watumishi wazuri au watumishi waovu? Je, umewahi kufikiria matokeo ya matendo haya yatakuwa nini?” Wakati huo, Mchungaji Li alisema kwa ghadhabu, “Tumekuja nyumbani kwako kukuambia haya leo kwa sababu tuna nia njema nawe, lakini unatukemea badala yake!” Kwa kuzungumza kwa nguvu ya haki, nilisema, “Mmekuja tena na tena kunisumbua, mkijua vizuri sana kuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu lina ukweli, lakini hamwezi kuniruhusu niukubali na hamwezi kuniruhusu nipate uzima. Je, hii ni dhana yenu ya ‘kuwa na nia njema’? Mmeeneza uvumi juu yangu, mkasababisha utesi kati yangu na watoto wangu, na kusababisha mwanangu kuvunja uhusiano wetu wa baba na mtoto. Je, huu ndio upendo mnaouzungumzia? Je, mmekuwa na nia njema kwa kubuni njama hizi zote au kuwa na nia fulani iliyofichika?” Aliposikia nikizungumza namna hii, sura ya Li Yang ilibadilika mara moja, na akaniambia kwa sauti kubwa kwa hasira, “Hujui nini kizuri kwako!” Nilimjibu kwa sauti kubwa, “Tukatize uhusiano wetu kuanzia sasa. Mungu anachukua jukumu la maisha yangu, na hamhitaji kujishughulisha nayo!” Waliposikia nikiyasema haya, Li Yang na wale wengine waliondoka wakionejana wenye huzuni. Kuanzia siku hiyo kuendelea, hakuna aliyekuja kunisumbua tena.

Baada ya kupitia vita hivi vya kiroho, nilikuja kupata utambuzi kiasi wa udanganyifu wa Shetani na pia nilikuja kuwa na ufahamu kamili wa kiini kinachomkataa Mungu cha viongozi katika ulimwengu wa kidini. Sikuwahi kuzuiliwa tena na nguvu mbaya za dini, na hatimaye nilikuwa huru na aliyekombolewa kumfuata Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: 22. Kukimbia Kutoka katika “Tundu la Chui”

Inayofuata: 24. Ni Nani Aliye Kizuizi kwenye Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

4. Mwamko wa Roho Aliyedanganywa

Na Yuanzhi, BraziliNilizaliwa katika mji mdogo huko Kaskazini mwa China na mnamo 2010, nikafuata jamaa kwenda Brazili. Hapa nchini Brazili,...

47. Kurejea Kutoka Ukingoni

Na Zhao Guangming, ChinaMwanzoni mwa miaka ya 1980, nilikuwa katika miaka yangu 30 nami nilikuwa nikifanyia kazi kampuni ya ujenzi....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki