720 Mungu Ataka Utiifu wa Kweli wa Mwanadamu
1 Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka. Watu ambao hawafanyi kitu zaidi ya kufurahia neema za Mungu hawawezi kukamilishwa, au kubadilishwa, na utii wao, uchaji Mungu, na upendo na ustahimilivu vyote hivyo ni vya juujuu tu. Wale ambao wanafurahia tu neema za Mungu hawawezi kumfahamu Mungu kweli, na hata pale wanapomjua Mungu, maarifa yao ni ya juujuu, na wanasema mambo kama vile Mungu anampenda mwanadamu, au Mungu ni mwenye huruma kwa mwanadamu. Hii haiwakilishi maisha ya mwanadamu, na haionyeshi kwamba kweli watu wanamjua Mungu.
2 Ikiwa, maneno ya Mungu yatakapowasafisha, au majaribu yake yatakapowajia, watu hawataweza kumtii Mungu—ikiwa, badala yake, watakuwa watu wa mashaka na kuanguka chini—basi hawana utii hata kidogo. Ndani yao, kuna kanuni na masharti mengi kuhusu imani kwa Mungu, uzoefu wa zamani ambao ni matokeo ya miaka mingi ya imani, au mafundisho mbalimbali kutoka kwenye Biblia. Je, watu kama hawa wanaweza kumwamini Mungu? Watu hawa wamejawa na mambo ya wanadamu—wanawezaje kumtii Mungu? Wote wanatii kulingana na mapendeleo yao binafsi—je, Mungu anaweza kutamani utii kama huu? Huku sio kumtii Mungu bali ni kufungamanishwa na mafundisho, ni kujiridhisha na kujifariji mwenyewe. Ikiwa unasema kwamba huu ni utii kwa Mungu, je, hivi hutakuwa unamkufuru Yeye? Wewe ni Farao wa Misri, unafanya uovu, unajishughulisha katika kazi ya kumpinga Mungu—je, Mungu anaweza kutaka kazi kama hii? Ni bora ungefanya haraka ukatubu na kuweza kujitambua kiasi fulani. Hutaingilia wala kusumbua, utakuwa umeijua sehemu yako, na kuishi vizuri—na hiyo haitakuwa bora zaidi? Kwa namna hiyo utakuwa umeepuka kumpinga Mungu na kuweza kuadhibiwa!
Umetoholewa kutoka katika “Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili