C. Maonyo ya Mungu kwa Mwanadamu

644. Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

645. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.

Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

646. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake. Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi ya binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumvulia mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

647. Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

648. Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua mambo bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe wenye kuchukulia mambo bila uzito na wenye msiofikiria katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

649. Wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu tu ya “mchango” ambao umetoa, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambazwa kote ulimwenguni hadi miisho ya dunia. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu[a]. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Hasha, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

650. Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

651. Kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

652. Madai Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama mnazungumzia tu mambo haya bila kufikiria, mkiongea sana kwa kuparaganya kwa maneno matupu ya majivuno yanayopita kiasi, basi ramani zenu na matakwa yenu yatakuwa ukurasa mtupu milele. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale kati yenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Mimi Huwatendea wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, siyo zawadi, sembuse huruma yoyote. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa wafuasi kwa miaka mingi mnaweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote hadi sasa mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na kutokuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa bora zaidi Niigeuze miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa utupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

653. Sasa ndio wakati ambao Roho Wangu anafanya kazi pakubwa, na wakati Ninapofanya kazi miongoni mwa Mataifa. Hata zaidi, ndio wakati ambapo Naainisha viumbe wote na kuweka kila kiumbe katika kundi lenye uhusiano, ili kazi Yangu iweze kuendelea haraka zaidi na kwa njia ya kufaa zaidi. Kwa hiyo, bado Nahitaji kwamba mjitoe mzimamzima kwa minajili ya kazi Yangu yote; aidha, mnafaa kutambua waziwazi na kuwa na hakika ya kazi ile yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kuweka nguvu zako zote katika kazi Yangu ili iweze kuwa ya matokeo bora zaidi. Hilo ndilo ambalo lazima uelewe. Msipigane tena wenyewe kwa wenyewe, kutafuta mbinu za usuluhishi, au kutafuta raha za mwili, mambo ambayo yanaweza kuchelewesha kazi Yangu na kuharibu mustakabali wako mzuri. Kufanya hivyo, mbali na kuweza kukupa ulinzi, litakuletea maangamizo. Je, si huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unafurahia leo kwa tamaa ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke majaribio ambayo yatakuwa magumu kujinasua kutoka na kuepuka kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako. Wakati ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katika hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imekaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza mwangaza anaofuata na kuingia katika giza totoro. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

654. Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, na bila kukoma wanatafuta maiti za wanadamu zinazoweza kuliwa. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya utunzaji Wangu na ulinzi. Kamwe msiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani. Katika hali yoyote usiishi kama ilivyokuwa katika siku za awali, kufanya jambo moja mbele Yangu na jingine nyuma Yangu—ukifanya hivyo umeshapita kiwango cha kukombolewa. Hakika Nimetamka zaidi ya kiasi cha kutosha maneno ya aina hii, sivyo? Ni kwa sababu asili ya mwanadamu ya zamani hairekebiki ndiyo maana Nimemkumbusha tena na tena. Usichoke! Haya yote Niyasemayo ni kwa mujibu wa kuhakikisha hatima yako! Kile Shetani anahitaji kwa hakika ni uchafu na pahali pabaya; na kadri unavyokosa kuokoleka kabisa, na kadri unavyokuwa mpotovu, ukikataa kujiwasilisha kwa hali ya kujizuia, ndivyo roho wachafu watakavyotumia nafasi yoyote ya kupenyeza. Mara unapowasili katika hii nafasi, uaminifu wako utakuwa kelele tupu, bila uhalisi wowote, na azimio lako litaliwa na pepo wachafu, kugeuzwa kuwa uasi au hila za Shetani, na kutumiwa kuzuia kazi Yangu. Kuanzia hapo, unaweza kupigwa na Mimi wakati wowote. Hakuna anayeelewa uzito wa hali hii; watu wote hupuuza tu yale wanayosikia na hawachukui tahadhari kwa vyovyote. Sikumbuki kile kilichofanywa katika siku za nyuma. Je, bado unasubiri Niwe mpole kwako Nisahau kwa mara nyingine tena?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

655. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kupima uungwana wa mtu kwa kipimio chenu wenyewe; kwa hiyo kazi Yangu inakuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawatumeni, mmoja baada ya mwingine, katika janga kupitia ili “mfundishwe” kupitia moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama, “Ujanja ndio moyo wa binadamu!” Hali za akili zenu zitakuwa zipi wakati huu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. … Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa, jinsi ilivyoandikwa katika rekodi ya majaliwa yako. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu akuchukue kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

656. Sasa, iwapo ufuatiliaji wenu umekuwa wa kufaa au la linatathminiwa na kile mlicho nacho sasa. Hiki ndicho kinachotumiwa kuamua matokeo yenu; yaani, matokeo yenu yanafichuliwa katika kujitolea mlikofanya na mambo ambayo mmefanya. Matokeo yenu yatadhihirishwa na ufuatiliaji wenu, imani yenu na mambo ambayo mmefanya. Kati yenu nyote, kuna wengi ambao tayari hawawezi kuokolewa, kwani leo ndiyo siku ya kufichua matokeo ya watu, na Sitakanganyikiwa katika kazi Yangu; Sitawaongoza wale wasioweza kuokolewa kabisa katika enzi ifuatayo. Kutakuwa na wakati ambapo kazi Yangu itakuwa imekamilika. Sitafinyanga maiti hizo ambazo haziwezi kuokolewa hata kidogo; sasa ndizo siku za mwisho za wokovu wa mwanadamu, na Sitafanya kazi isiyo ya maana. Usishutumu Mbingu na dunia—mwisho wa dunia unakuja. Hauepukiki. Mambo yamefika hapa, na hakuna kitu ambacho wewe kama mwanadamu unaweza kufanya kuyasimamisha; huwezi kubadili vitu jinsi utakavyo. Jana, hukulipa gharama ya kufuatilia ukweli na hukuwa mwaminifu; leo, wakati umewadia, huwezi kuokolewa; na kesho, utaondolewa, na hakutakuwa na uhuru wa matendo kwa ajili ya wokovu wako. Hata ingawa moyo wangu ni mpole na Ninafanya kila Niwezalo kukuokoa, usipojitahidi wewe mwenyewe ama kujifikiria hata kidogo, hili linanihusu vipi? Wale wanaofikiria tu miili yao na wanaofurahia faraja, wale wanaoonekana kuamini lakini wasioamini kwa kweli; wale wanaojihusisha katika uganga na uchawi; wale ambao ni wazinzi, walio duni kabisa; wale wanaoiba sadaka za Yehova na mali Yake; wale wanaopenda hongo; wale walio na njozi za kupaa mbinguni; wale ambao ni wenye majivuno na fidhuli, wanaojitahidi tu kwa sababu ya umaarufu na utajiri wa kibinafsi; wale wanaoeneza maneno ya safihi; wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe; wale wanaotoa tu hukumu dhidi ya Mungu Mwenyewe na kumkashifu; wale wanaounda vikundi na kutafuta kujitegemea; wale wanaojitukuza juu ya Mungu, wale wanaume na wanawake wadogo, wa makamo na wakubwa ambao ni wapuuzi na wametegwa katika uasherati; wale wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu na utajiri wa kibinafsi na wanafuatilia hadhi ya kibinafsi miongoni mwa mengine; wale watu wasiotubu walionaswa katika dhambi—je, si wote hawawezi kuokolewa? Uasherati, kutenda dhambi, uganga, uchawi, matusi na maneno ya safihi yote yamejaa kwenu; na ukweli na maneno ya uzima yanakanyagwa miongoni mwenu, na lugha takatifu inachafuliwa miongoni mwenu. Ninyi Mataifa, mliojaa uchafu na uasi! Matokeo yenu ya mwisho yatakuwa yapi? Je, wale wanaopenda mwili, wanaotenda uchawi wa mwili, na waliotegwa katika dhambi ya uasherati wanawezaje kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi! Je, hujui kwamba watu kama ninyi ni mabuu wasioweza kuokolewa? Ni nini kinachowapa haki ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo katika wale wasiopenda ukweli na wanapenda tu mwili—watu kama hawa wanawezaje kuokolewa? Wale wasiopenda njia ya uzima, wasiomtukuza Mungu ama kumshuhudia, wanaopanga njama kwa ajili ya hadhi yao wenyewe, wanaojisifu sana—je, si bado wao wako vivyo hivyo, hadi leo? Kuna thamani gani katika kuwaokoa? Iwapo unaweza kuokolewa hakutegemei ukubwa wako ama ni miaka mingapi umekuwa ukifanya kazi, sembuse sifa ambazo umeongeza. Badala yake, kunategemea iwapo ufuatiliaji wako umezaa matunda. Unapaswa kujua kwamba wale waliookolewa ni “miti” inayozaa matunda, siyo miti iliyo na majani yaliyositawi sana na maua mengi lakini ambayo hayazai matunda. Hata kama umeshinda miaka mingi ukizurura mitaani, hilo lina maana gani? Ushuhuda wako uko wapi? Uchaji wako wa Mungu ni kidogo sana kuliko upendo wako kwako mwenyewe na hamu zako zenye tamaa—je, si mtu kama huyu ni mpotovu? Anawezaje kuwa kielelezo na mfano wa wokovu? Asili yako ni isiyorekebishika, wewe ni mwasi sana, huwezi kuokolewa! Je, si watu kama hawa ni wale watakaoondolewa? Je, si wakati ambapo kazi Yangu inakamilika ni wakati wa kufika kwa siku yako ya mwisho? Nimefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana miongoni mwenu—kweli mmeyasikiliza kiasi kipi? Mmewahi kutii kiasi kipi? Kazi Yangu ikamilikapo, huo utakuwa wakati ambapo unakoma kunipinga, wakati ambapo unakoma kusimama dhidi Yangu. Nifanyapo kazi, mnanipinga bila kukoma; kamwe hamyatii maneno Yangu. Nafanya kazi Yangu na wewe unafanya “kazi” yako mwenyewe, ukitengeneza ufalme wako mdogo. Ninyi ni kundi la mbweha na mbwa tu, mnaofanya kila kitu kunipinga! Mnajaribu kila wakati kuwakumbatia wale wanaowapa upendo wao wa dhati—uchaji wenu uko wapi? Kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu! Hamna utii wala uchaji, na kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hawa wanaweza kuokolewa? Wanadamu ambao ni waasherati na wakware daima hutaka kuwavutia makahaba wenye ubembe kwao kwa ajili ya raha zao wenyewe. Sitawaokoa mashetani wa kisherati kama hawa hata kidogo. Nawachukia ninyi mashetani wachafu, na ukware na ubembe wenu utawatumbukiza kuzimuni. Mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi mashetani wachafu na pepo waovu ni wa kutia kinyaa! Mnachukiza! Watu ovyo kama ninyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi wanaweza kuokolewa bado? Leo, ukweli huu, njia hii, na uzima huu hauwavutii; badala yake mnavutiwa na utendaji dhambi, fedha, hadhi, umaarufu na faida; mnavutiwa na raha za mwili; sura nzuri za wanaume na uzuri wa wanawake. Ni nini kinachowastahiki kuingia katika ufalme Wangu? Sura yenu hata ni ya juu zaidi kuliko ya Mungu, hadhi yenu hata ni ya juu kuliko ya Mungu sembuse fahari yenu kubwa miongoni mwa wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hujageuka kuwa malaika mkuu? Wakati matokeo ya watu yanafichuliwa, ambao pia ndio wakati kazi ya wokovu itakaribia kuisha, wengi kati yenu mtakuwa maiti msioweza kuokolewa na lazima muondolewe. Wakati wa kazi ya wokovu, Mimi ni mwenye huruma na mzuri kwa watu wote. Kazi inapokamilika, matokeo ya watu wa aina tofauti yatafichuliwa, na wakati huo, Sitakuwa mwenye huruma na mzuri tena, kwa kuwa matokeo ya watu yatakuwa yamefichuliwa, na kila mmoja atakuwa ameainishwa kulingana na aina yake, na hakutakuwa na haja ya kufanya kazi zaidi ya wokovu, kwa sababu enzi ya wokovu itakuwa imepita, na kwa sababu imepita, haitarudi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

657. Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba daima Mimi hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi kuishi pamoja na nyinyi kwa namna hii—lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine. Natumai mtaniendekeza, nami Natumai hata zaidi kwamba mtaweza kuamini kila neno Ninalosema, na bado zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Msiwe na shaka juu ya yale Ninayosema, au hata kuchukua maneno Yangu mnavyotaka na kuyatupilia mbali kwa hiari, jambo ambalo mimi Ninaona halistahimiliki. Msiyahukumu maneno Yangu, wala kutoyachukulia kwa uzito, au kusema kwamba daima Nawajaribu, au mbaya zaidi, kusema kwamba kile ambacho Nimewaambia kinakosa usahihi. Ninaona kuwa mambo haya hayavumiliki. Kwa sababu mnanichukulia Mimi na kuyachukulia Ninayoyasema kwa shaka kuu na kamwe hamyazingatii, Ninamwambia kila mmoja wenu kwa uzito kabisa: Msiunganishe kile Ninachosema kwa falsafa, msikiweke pamoja na uongo wa matapeli, na hata zaidi, msiyajibu maneno Yangu kwa dharau. Labda katika siku zijazo hakuna mtu yeyote atakuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninayowaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma sana, sembuse kuwaeleza mambo haya kwa uvumilivu hivi. Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kugumia kwa maumivu, au mtakuwa mkiishi katika usiku wa giza bila hata chembe ya ukweli au kupewa maisha, au kusubiri tu bila matumaini, au katika majuto machungu mengi kiasi kwamba hamwezi kufikiri…. Huu uwezekano mbadala hauwezi kuepukika kabisa kwa mtu yeyote kati yenu. Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu ambaye anamiliki kiti ambacho kwacho kwa kweli mnamwabudu Mungu; mnajitumbukiza katika dunia ya uasherati na maovu, kuchanganya ndani ya imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili, mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yanapingana nayo. Hivyo kile Ninachotumai kwenu ni kuwa muweze kuletwa kwa njia ya mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba muweze kujitunza, muweze kujiangalia, si kuweka mkazo mwingi sana juu ya hatima yenu kiasi kwamba muitazame mienendo na dhambi zenu kwa kutojali.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

658. Kadri dhambi zako zilivyo nyingi, ndivyo nafasi zako za kupata hatima iliyo nzuri zilivyo chache. Kinyume chake, kadri dhambi zako zilivyo chache, ndivyo nafasi zako za kusifiwa na Mungu zilivyo nyingi. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambapo haiwezekani Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata. Kama wewe ni mtu mwenye ari anayetenda ukweli basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kitakuwa kidogo zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu asiye radhi kutenda ukweli basi hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitakua zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kufurahisha ya kupokea baraka itaharibiwa. Usizichukulie dhambi zako kama makosa ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora wako wa tabia ulio duni ulifanya isiwezekane kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hataupata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukusumbua, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza madai ya ukweli na kukufanya milele kuwa mwenzi mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

659. Ingawa sehemu ya kiini halisi cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau hoja kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Anao upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na kwamba Yeye hana hisia zozote, au mijibizo yoyote. Kwamba Anayo rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote kuhusiana na namna Anavyoshughulikia watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Yeye si kikaragosi kilichofikiriwa au kitu kingine tu. Kwa sababu Yeye yupo, tunafaa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake siku zote, kutilia makini mwelekeo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatufai kutumia kufikiria kwa watu ili kumfafanua Mungu, na hatufai kulazimisha fikira na matamanio ya watu kwa Mungu, kumfanya Mungu kutumia mtindo na fikira za binadamu katika namna Anavyomshughulikia binadamu. Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu mlio hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusiana na namna mnavyoshughulikia Mungu, mnapokuwa makini zaidi na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi! Wakati huelewi mwelekeo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kama unaweza kutimiza hoja hii kati ya zote, na kumiliki mwelekeo huu kati ya yote, basi Mungu hatakulaumu wewe kwa upumbavu wako, kutojua kwako, na ukosefu wa kuelewa kwa sababu zinazosababisha vitu. Badala yake, kutokana na hofu yako ya kumkosea Mungu, heshima yako kwa nia za Mungu, na mwelekeo wako wa kuwa radhi kumtii Yeye, Mungu atakukumbuka, atakuongoza na kukuangaza wewe, au kustahimili kutokuwa mkomavu kwako na kutojua kwako. Kinyume chake, endapo mwelekeo wako kwake Yeye utakuwa usioheshimu—kuhukumu Mungu kiholela, kukisia kiholela, na kufafanua maana ya Mungu—Mungu atakupa hukumu, nidhamu, au hata adhabu; au Atakupa taarifa. Pengine kauli hii inahusisha matokeo yako. Hivyo basi, Ningali bado nataka kutilia mkazo jambo hili kwa mara nyingine: Unapaswa uwe makini na mwenye busara katika kila kitu kinachotoka kwa Mungu. Usiongee kwa uzembe, na usiwe mzembe katika matendo yako. Kabla ya kusema chochote, unafaa kufikiria: Je, kufanya hivi kutamghadhabisha Mungu? Kufanya hivi ni kumcha Mungu? Hata katika masuala mepesi, bado unafaa kujaribu kuelewa hakika maswali haya, yafikirie kwa kweli. Kama unaweza kwa kweli kutenda haya kulingana na kanuni hizi kila pahali, katika hali zote, katika vitu vyoye, nyakati zote, na kushikilia mtazamo wa aina hiyo hasa wakati huelewi kitu basi Mungu siku zote atakuongoza wewe, na kukupa na hata njia ya kufuata. Bila kujali ni nini ambacho watu wanaonyesha, Mungu anaona yote waziwazi, dhahiri, na Atakupa utathmini sahihi na unaofaa kwa maonyesho haya. Baada ya kupitia jaribio la mwisho, Mungu atachukua tabia yako yote na kuijumlisha ili kuasisi matokeo yako. Matokeo haya yatashawishi kila mmoja bila shaka lolote. Kile ambacho Ningependa kuwaambia ni kwamba kila kitendo chenu, kila hatua yenu, na kila fikira yenu vyote vitaamua majaliwa yenu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

660. Kuhusu jinsi watu humtafuta na jinsi wanavyomweleka Mungu, mitazamo ya watu ni ya umuhimu wa kimsingi. Usimwache Mungu kana kwamba yeye ni fungu la hewa kavu tu linaloelea karibu na nyuma ya kichwa chako. Usikose kumjali Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu nyuma ya kichwa chako. Siku zote fikiria kuhusu Mungu wa imani yako kama Mungu hai, Mungu halisi. Yeye hayupo kule juu kwenye mbingu ya tatu bila chochote cha kufanya. Badala yake, siku zote bila kusita Anaangalia kwenye mioyo ya kila mmoja, Akiangalia ni nini unachofanya, akichunguza kila neno dogo na kila tukio dogo, akiangalia mwenendo wako na mwelekeo wako kwa Mungu. Kama uko radhi kujitolea kwa Mungu au la, tabia yako yote na fikira zako na mawazo yako ya ndani zaidi ziko mbele ya Mungu, na yanaangaliwa na Yeye. Ni kulingana na tabia yako, kulingana na vitendo vyako, na kulingana na mwelekeo wako kwa Mungu, ambapo maoni Yake kwako, na mwenendo Wake kwako, vinaendelea vikibadilika. Mimi Ningependa kutoa ushauri fulani kwa baadhi ya watu. Msijiweke kwenye mikono ya Mungu kama watoto wachanga, kana kwamba Yeye Anapaswa kukupenda sana, kana kwamba Asingewahi kukuacha, na kana kwamba mwelekeo Wake kwako ni imara na usingeweza kubadilika, na Ninawashauri muache kuota ndoto! Mungu ni mwenye haki katika kutendea kila mtu. Anakabiliana na kazi ya ushindi wa wanadamu na wokovu kwa bidii. Huo ndio usimamizi Wake. Anashughulikia kila mmoja kwa umakinifu, na wala si kama kiumbe cha kufugwa cha kucheza nacho. Upendo wa Mungu kwa binadamu si ule wa kudekeza au kupotosha; rehema na uvumilivu Wake kwa wanadamu si dokezi au ya kutotilia maanani. Kinyume cha mambo, upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kutunza, kusikitikia, na kuheshimu maisha; rehema na uvumilivu Wake vyote vinaonyesha matarajio Yake kwa binadamu; rehema na uvumilivu Wake ndivyo ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Mungu yuko hai, na kwa hakika Mungu yupo; mwelekeo Wake kwa wanadamu unafuata kanuni, si yenye kutangazwa kama imani ya dini, na unaweza kubadilika. Mapenzi Yake kwa binadamu yanabadilika kwa utaratibu na kurekebishwa kwa muda, hali na mwelekeo wa kila mtu. Kwa hiyo, unafaa kujua rohoni mwako na uwazi wote kwamba kiini halisi cha Mungu hakibadiliki, na kwamba tabia Yake itajitokeza katika nyakati tofauti, na muktadha tofauti. Huenda usifikirie kwamba hili si suala muhimu, na wewe unatumia dhana zako za kibinafsi katika kufikiria namna ambavyo Mungu anafaa kufanya mambo. Lakini zipo nyakati ambapo kinyume kabisa cha mtazamo wako ni kweli, na kwa kutumia dhana zako za kibinafsi katika kujaribu na kumpima Mungu, tayari umemghadhabisha. Hii ni kwa sababu Mungu hafanyi kazi kama unavyofikiria wewe, Naye Mungu hatalishughulikia suala hili kama vile unavyosema Atalishughulikia. Na hivyo basi Nakukumbusha kuwa makini na mwenye hekima katika mtazamo wako katika kila kitu, na ujifunze namna ya kufuata kanuni ya kutembea kwenye njia ya Mungu katika mambo yote—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima uimarishe uelewa dhabiti katika masuala ya mapenzi ya Mungu na mwelekeo wa Mungu; kutafuta watu walio na nuru kuuwasilisha kwako, na kutafuta kwa dhati. Usimwone Mungu wa imani yako kama kikaragosi—kuhukumu kiholela, kufikia hitimisho kiholela, kutomshughulikia Mungu kwa heshima Anayostahili. Katika mchakato wa wokovu wa Mungu Anapofafanua matokeo yako, bila kujali kama Yeye atakupa rehema, au uvumilivu, au hukumu na kuadibu, mwelekeo Wake kwako wewe unabadilika. Inategemea na mwelekeo wako kwa Mungu, na uelewa wako wa Mungu. Usiache dhana moja ya kupita ya maarifa au uelewa wako katika Mungu kumfafanua Yeye daima. Usisadiki katika Mungu aliyekufa; amini kwa yule aliye hai.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

661. Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, lakini sio ushughulikiaji na upogoaji Wake; hata zaidi hamwezi kukubali mpangilio Wake wote, kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni gani hapa? Kimsingi, imani yenu ni kaka tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada. Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mkondo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kujipendekeza kwa Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na hauwezi kuchukuliwa kuwa imani ya kweli hata kidogo. Kifaranga anaweza kujitokezaje kwa imani kama hii? Kwa maneno mengine, ni tunda lipi ambalo imani kama hii inaweza kuzalisha? Azma ya imani yenu kwa Mungu ni kutimiza nia zenu kupitia kumtumia Mungu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo. Unaamini kwamba unaweza kutenda utakavyo kwa Kristo alimradi wewe ni mwaminifu kwa Mungu aliye mbinguni? Makosa! Kutomjua Kristo kwako ni kutomjua Mungu aliye mbinguni. Bila kujali uaminifu wako kwa Mungu aliye mbinguni, ni maneno matupu tu na kujifanya, kwani Mungu aliye duniani si muhimu tu kwa mwanadamu kupokea ukweli na ufahamu mkubwa zaidi, lakini hata zaidi ni muhimu kwa lawama ya mwanadamu na baadaye kwa kuushika ukweli kuwaadhibu waovu. Umeelewa matokeo yenye faida na yanayodhuru hapa? Umepata kuyapitia? Ningependa siku moja hivi karibuni ninyi muelewe ukweli huu: Kumjua Mungu, mnapaswa kumjua sio tu Mungu wa mbinguni lakini, hata muhimu zaidi, Mungu aliye duniani. Msiyachanganye yaliyo kipaumbele ama kuruhusu yaliyo ya pili kuchukua nafasi ya yaliyo ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kupeleka moyo wako karibu na Yeye. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima iwe kuwa mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, ila badala yake imeingiza njia zako ovu ndani ya asili yako, na huna maono maradufu ya uwongo kuhusu fahari kuliko awali pekee lakini kutonielewa kwako kumeongezeka pia, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako mdogo wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya juujuu tena, lakini yamepenya ndani kwa mifupa yako. Yote yaliyosalia ni wewe kusubiri matayarisho ya mazishi yako kufanywa. Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini lile lililo kubwa sana kiasili. Wakati utakapofika, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha mbeleni. Yote yanarudia haya: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, yaani, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

662. Kila mwanadamu, katika kuishi maisha yake ya imani katika Mungu, amemkataa na kumdanganya Mungu wakati fulani. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za utawala, yaani, yanaikosea tabia ya Mungu. Wengi ambao wanajali majaliwa yao binafsi wanaweza kuuliza matendo haya ni yapi. Lazima mjue kwamba nyinyi mna kiburi na wenye majivuno kiasili, na hamko radhi kutii ukweli. Kwa sababu hii, Nitawaambia kidogo kidogo baada ya nyinyi kutafakari kujihusu. Ninawashawishi kuwa na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu nyinyi hamna maadili katika matendo yenu, kufanya na kutenda kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili sana katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa kuzimu. Kwa binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote zaidi. Je, una habari, hata hivyo, kwamba katika macho ya Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwake hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za utawala za Mungu zaidi ya mara moja na hujaonyesha ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia kuzimu pale ambapo Mungu anamwadhibu mwanadamu. Katika wakati wao wa kufuata Mungu, idadi ndogo ya watu ilitenda matendo yaliyoenda kinyume na kanuni, lakini baada ya kushughulikiwa na kuongozwa, waligundua polepole upotovu wao, na kisha wakachukua njia iliyo sawa ya uhalisi, na leo wanabaki wenye msingi imara katika njia ya Bwana. Binadamu kama hawa ndio watakaobakia mwisho. Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya kiwango kilichowekwa. Yeyote asiyemcha Mungu na asiye na moyo unaotetema kwa woga atakiuka amri za utawala za Mungu kwa urahisi. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya hisia kali, na hawajui katu amri za utawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyokatiza usimamizi wa Mungu. Kwa hali za uzito sana, wanatupwa nje na kunyang’anywa fursa yoyote zaidi ya kumfuata, na wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba ya Mungu unakoma. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa bila jitihada. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si mafungu wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu, na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na hujajiandaa ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

663. Kila sentensi Niliyoizungumza ina tabia ya Mungu ndani yake. Mngefanya vizuri endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka kwa maneno hayo. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuelewa, lakini Ninaamini kwamba nyinyi nyote mnayo angalau mawazo fulani kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatulizwa moyo. Kwa mfano, mweke Mungu katika moyo wako siku zote. Unapochukua hatua, fanya hivyo kulingana na maneno Yake. Tafuta nia Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Hata zaidi usimweke Mungu nyuma ya akili zako ili ukajaze uwazi wa baadaye katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umekosea tabia ya Mungu. Tena, tuchukulie kwamba kamwe hutamki matamshi ya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu maisha yako yote, na tena, tuchukulie kwamba unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho amekuaminia wewe na pia kutii maneno Yake yote katika maisha yako yote, basi utakuwa umeweza kuepuka kwa kukosea amri za utawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya ni nuru kiasi ya Roho Mtakatifu tu,” “Katika maoni yangu, si kila kitu ambacho Mungu anakifanya lazima ni sahihi,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukubwa zaidi kuliko wangu,” “Maneno ya Mungu hayaiaminiki kabisa,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakusihi wewe kukiri na kutubu dhambi zako mara nyingi zaidi. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani hukosei mwanadamu, ila Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unamhukumu mtu tu, lakini Roho wa Mungu haichukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia Yeye heshima. Kama hali ni hivi, basi si ni kweli kwamba umekosea tabia ya Mungu? Lazima ukumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu kinafanywa ili kukinga kazi Yake katika mwili na ili kazi hii ifanywe vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ni mtu ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, kwa hivyo Atatumia adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

664. Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, umefanya hitimisho lolote kuhusiana na namna unavyofaa kumtunza Mungu? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili utende, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anafanya na wewe, kile Anachopanga na wewe, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

665. Labda umeteseka sana katika wakati wako, lakini sasa bado huelewi chochote; hujui kila kitu kuhusu uzima. Ingawa umeadhibiwa na kuhukumiwa, hujabadilika kamwe na ndani yako kabisa hujapata uzima. Wakati wa kutathmini kazi yako utakapofika, utapitia majaribio makali kama moto na hata majonzi makuu zaidi. Moto huu utageuza nafsi yako yote kuwa majivu. Kama mtu asiyekuwa na uzima, mtu asiye na aunsi ya dhahabu safi ndani yake, mtu ambaye bado amekatalia tabia potovu ya kale, na mtu asiyeweza hata kufanya kazi nzuri ya kuwa foili, ni jinsi gani hutaweza kuondoshwa? Kazi ya kushinda ina faida gani kwa mtu aliye na thamani ya chini kuliko peni na asiyekuwa na uzima? Wakati huo ufikapo, siku zenu zitakuwa ngumu zaidi kuliko za Nuhu na Sodoma! Maombi yenu hayatawasaidia wakati huo. Mara tu kazi ya wokovu ikiisha, utaanzaje tena kutubu? Mara tu kazi ya wokovu itakuwa imefanywa, hakutakuwa tena na kazi ya wokovu. Kitakachokuwepo ni mwanzo wa kazi ya kuadhibu uovu. Wewe hupinga, huasi, na hufanya mambo unayojua ni maovu. Je, wewe sio shabaha ya adhabu kali? Ninakuelezea hili wazi leo. Ukichagua kutosikia, wakati maafa yakufike baadaye, je, hautakuwa umechelewa kama utaanza wakati huo tu kuhisi majuto na kuanza kuamini? Nakupa nafasi ya kutubu leo, lakini wewe hauko radhi kufanya hivyo. Unataka kungoja kwa muda gani? Mpaka siku ya kuadibu? Sikumbuki dhambi zako za zamani leo; Nakusamehe tena na tena, kugeuka kutoka upande wako mbaya kutazama tu upande wako mzuri, kwa sababu maneno na kazi Yangu yote ya sasa yanatakiwa kukuokoa wewe na sina nia mbaya kwako. Lakini unakataa kuingia; huwezi kutambua mema kutoka kwa mabaya na hujui namna ya kufurahia wema. Je, mtu wa aina hii hanuii tu kungoja ile adhabu na malipo yenye haki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

666. Kufanya kazi Kwangu miongoni mwenu sio kabisa sawa na Yehova kufanya kazi katika Israeli, na hasa si sawa na Yesu kufanya kazi Uyahudi. Ni kwa uvumilivu mkuu ndio Nanena na kufanya kazi, na ni kwa hasira na vilevile hukumu ndio Nawashinda wapotovu hawa. Si chochote kama Yehova kuwaongoza watu Wake katika Israeli. Kazi Yake katika Israeli ilikuwa kutoa chakula na maji ya uzima, na Alijawa huruma na upendo kwa watu Wake katika utoaji Wake wa vitu kwao. Kazi ya leo hufanywa katika taifa ambalo halijachaguliwa, ambalo limelaaniwa. Hakuna chakula tele, wala hakuna ustawishaji wa maji ya uzima ya kukata kiu sembuse utoaji wa bidhaa za mwili za kutosha; kunao tu utoaji wa hukumu, laana, na kuadibu vya kutosha. Hawa mabuu katika lundo la samadi hawastahili kwa uthabiti kupata vilima vya ng’ombe na kondoo, utajiri mwingi, na watoto wazuri zaidi kotekote katika nchi ambavyo Nilitoa kwa Israeli. Israeli ya siku hizi hutoa juu ya madhabahu ng’ombe na kondoo na vitu vya dhahabu na fedha ambavyo Mimi huwastawisha navyo, kushinda sehemu moja ya kumi inayotakiwa na Yehova chini ya sheria, na kwa hiyo Nimewapa hata zaidi, zaidi ya mara mia moja ya kile ambacho Israeli ilikuwa ipate chini ya sheria. Kile ambacho Nastawisha Israeli nacho kinashinda kile ambacho Abrahamu na Isaka walipata. Nitaifanya familia ya Israeli kuzaa na kuongezeka, na Nitawafanya watu Wangu wa Israeli kuenea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa ulimwengu mzima. Wale ambao Mimi hubariki na kutunza bado ni wateule wa Israeli, yaani, watu ambao hutoa kila kitu Kwangu, ambao wamepata kila kitu kutoka Kwangu. Ni kwa sababu wao huniweka Mimi mawazoni ndiyo wao hutoa sadaka ya ndama na wanakondoo waliozaliwa karibuni juu ya madhabahu Yangu takatifu na hutoa mbele Yangu kila kitu walicho nacho, hata kwa kiwango cha kutoa wana wao wa kwanza waliozaliwa karibuni kwa matarajio ya kurudi Kwangu. Na ninyi je? Ninyi huamsha hasira Yangu, ninyi huwa na matakwa mengi kutoka Kwangu, ninyi huiba sadaka za wale wanaotoa vitu Kwangu na hamjui kwamba mnanikosea Mimi, hivyo mnachopata ni kutoa machozi na adhabu katika giza. Ninyi mmechochea hasira Yangu mara nyingi na Nimenyesha moto Wangu wa kuchoma, kiasi kwamba kumekuwa na wengi waliopatwa na mwisho wa majonzi, ambao makazi yao ya furaha yalikuwa makaburi ya kuhuzunisha. Yote Niliyo nayo kwa mabuu hawa ni hasira isiyoisha, na sina kusudi la baraka. Ni kwa ajili ya kazi Yangu tu ndiyo Nimefanya kinzano na kuwatia ninyi moyo, na kwamba Nimevumilia fedheha kuu kufanya kazi miongoni mwenu. Isingekuwa mapenzi ya Baba Yangu, Ningewezaje kuishi katika nyumba moja na mabuu wanaobingirika kutoka upande mmoja hadi mwingine ndani ya rundo la samadi? Nahisi chuki mno kwa vitendo na maneno yenu yote, na vyovyote vile, kwa sababu Nina “shauku” kiasi katika uchafu na uasi wenu, huu umekuwa mkusanyiko mkubwa wa maneno Yangu. La sivyo Mimi bila shaka singebaki miongoni mwenu kwa muda mrefu hivi. Kwa hiyo, mnapaswa kujua kwamba mtazamo Wangu kuelekea kwenu ni wa upole na huruma tu, mmoja ambao kwao hakuna upendo, ila stahamala tu kwenu, kwa sababu Mimi hufanya hili kwa ajili ya kazi Yangu tu. Na mmeyaona matendo Yangu tu kwa sababu Nimechagua uchafu na uasi kama “mali ghafi.” La sivyo Mimi bila shaka singeyafichua matendo Yangu kwa mabuu hawa; Nafanya tu kazi ndani yenu na usitaji; si chochote kama wepesi na hiari ya kazi Yangu katika Israeli. Nazungumza miongoni mwenu kwa kusita, Nikiibeba hasira Yangu. Isingekuwa kazi Yangu kuu zaidi, Ningewezaje kuvumilia mtazamo wenye kuendelea wa mabuu hawa? Isingekuwa kwa ajili ya jina Langu Ningekuwa Nimepanda vilele vya juu zaidi kitambo na kuwateketeza kabisa hawa mabuu na lundo la samadi! Isingekuwa kwa ajili ya utukufu Wangu, Ningewezaje kuwakubalia pepo hawa waovu kunipinga Mimi waziwazi na vichwa vyao vikitikiswa mbele ya macho Yangu? Isingekuwa kusababisha kazi Yangu kutekelezwa kwa urahisi bila kizuizi hata kidogo, Ningewezaje kuwakubalia hawa watu wanaofanana mabuu kunitusi Mimi kwa utukutu? Kama watu mia moja kijijini mwa Israeli wangeinuka kunipinga Mimi hivi, hata kama wangetoa sadaka Kwangu bado Ningewafutilia mbali chini ya nyufa zilizo ardhini ili watu katika miji mingine hawangeasi tena. Mimi ni moto uteketezao na Sivumilii kosa. Kwa sababu wanadamu wote waliumbwa na Mimi, chochote Nisemacho na kufanya, watu lazima watii na hawawezi kukiasi. Watu hawana haki ya kuingilia kazi Yangu, na wao hasa siyo wenye sifa zinazostahili kuchambua kilicho cha kweli au chenye makosa katika kazi Yangu na maneno Yangu. Mimi ni Bwana wa uumbaji, na viumbe wanapaswa kutimiza kila kitu Ninachohitaji kwa moyo wa kunicha Mimi; hawapaswi kutoa sababu ili kunishawishi Mimi na wao hasa hawapaswi kunipinga. Ninatumia mamlaka Yangu kuwatawala watu Wangu, na wale wote ambao ni sehemu ya uumbaji Wangu wanapaswa kuyatii mamlaka Yangu. Ingawa leo ninyi ni, jasiri na wenye kiburi mbele Yangu, ninyi hukaidi maneno ambayo Nawafunzia, na hamwogopi, Mimi hukumbana tu na uasi wenu na uvumilivu. Singekasirika na kuathiri kazi Yangu kwa sababu mabuu wadogo sana walipindua uchafu katika rundo la samadi. Mimi huvumilia kuendelea kuwepo kwa kila kitu ambacho Mimi huchukia kabisa na mambo ambayo Mimi huchukia kabisa kwa ajili ya mapenzi ya Baba Yangu, mpaka matamshi Yangu yawe kamili, mpaka dakika Yangu ya mwisho kabisa. Usijali! Siwezi kuzama katika kiwango sawa na buu asiyefaa kutajwa, na Sitafananisha kiwango cha ujuzi na wewe. Nakuchukia kabisa, ilhali Naweza kuvumilia. Wewe hunikaidi Mimi, ilhali huwezi kuepuka siku ya Mimi kukuadibu ambayo Baba Yangu ameniahidi Mimi. Je, buu aliyeumbwa anaweza kufananishwa na Bwana wa uumbaji wote? Katika majira ya kupukutika kwa majani, majani yaangukayo hurudi kwa mizizi yake, wewe hurudi kwa nyumba ya “baba” yako, na Mimi hurudi ubavuni pa Baba Yangu. Mimi huandamana na upendo mwema wa Baba Yangu, na wewe hufuatwa na kuvyogwa kwa baba Yako. Nina utukufu wa Baba Yangu, na wewe una aibu ya baba yako. Mimi hutumia kuadibu ambako Nimeshikilia kwa muda mrefu kuandamana na wewe, na wewe hukutana na kuadibu Kwangu na mwili wako uliooza ambao tayari umekuwa mpotovu kwa makumi ya maelfu ya miaka. Nimehitimisha kazi Yangu ya maneno ndani yako, ikiandamana na uvumilivu, na umeanza kutimiza wajibu wa kupitia msiba kutoka kwa maneno Yangu. Mimi hufurahia sana na kufanya kazi katika Israeli; wewe hulia na kusaga meno yako na huishi na kufa matopeni. Nimepata tena umbo Langu la asili na Sibaki tena ndani ya uchafu na wewe, huku umepata tena ubaya wako wa asili na bado unafukua kila mahali katika lundo la samadi. Wakati ambapo kazi na maneno Yangu yatakamilika, itakuwa siku ya furaha Kwangu. Wakati ambapo upinzani na uasi wako utakwisha, itakuwa siku ya kulia kwako machozi. Sitakuonea huruma, na hutaniona Mimi tena. Sitakuwa tena na mazungumzo na wewe, na hutakutana na Mimi tena. Nitachukia uasi wako, na utakosa kupendeza Kwangu. Nitakupiga wewe, na utanikosa Mimi. Nitaondoka kwako kwa furaha, na utafahamu deni lako Kwangu. Sitakuona wewe tena, lakini wewe kila mara utanitarajia Mimi. Nitakuchukia kwa sababu unanipinga Mimi sasa, na utanikosa Mimi; kwa sababu Nakuadibu sasa. Siko radhi kuishi ubavuni pako, lakini utalitamani sana kwa uchungu na kulia machozi katika milele, kwa sababu utajuta kila kitu ambacho umenifanyia Mimi. Utajuta uasi wako na upinzani wako, na hata utaulaza uso wako juu ya ardhi kutokana na kujuta, na utaanguka chini mbele Yangu na kuapa kutonikaidi Mimi tena. Lakini ndani ya moyo wako wewe hunipenda Mimi tu na hutaweza kamwe kuisikia sauti Yangu, lazima Nikufanye ujionee haya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

667. Naona sasa mwili wako usiozuiwa ambao umenibembeleza Mimi, na Nina onyo kidogo tu kwako. Mimi bila shaka sichukui hatua kupitia kuadibu “kukutumikia” wewe. Unapaswa kujua ni wajibu gani ambao wewe huchukua katika kazi Yangu, na kisha Nitaridhika. Kuongezea kwa hili, ukinipinga Mimi au kutumia pesa Zangu, au kula sadaka za Mimi, Yehova, au ninyi mabuu mnaumana, au kuna ugomvi au kuingiliana kati ya ninyi viumbe mfano wa mbwa—Sihusiki na yoyote kati ya hayo. Mnahitaji tu kujua ninyi ni vitu vya aina gani, na Nitaridhika. Mbali na vitu hivi, ni sawa kama mko radhi kuvutiana panga au mikuki au kupigana kwa maneno yenu. Sina tamaa ya kuingilia mambo hayo, na Mimi sihusiki hata kidogo katika mambo ya binadamu. Sio kwamba Sijali kuhusu ugomvi kati yenu, lakini ni kwa sababu Mimi si mmoja wenu, hivyo, Sishiriki katika mambo yaliyo kati yenu. Mimi Mwenyewe si mmoja wa uumbaji na si wa dunia hii, kwa hiyo, Nachukia kabisa maisha ya kuharakisha miongoni mwa watu na hayo mahusiano yasiyofaa, yasiyofaa kati ya watu. Mimi hasa Nachukia kabisa hayo makundi ya makelele ya watu. Hata hivyo, Najua kwa kina uchafu ndani ya mioyo ya kila kiumbe, na kabla ya Mimi kuwaumba ninyi, Nilijua tayari udhalimu uliokuwepo ndani ya kina cha mioyo ya binadamu, na Niliujua udanganyifu na uhalifu wote katika mioyo ya binadamu. Kwa hiyo, hata ingawa hakuna kabisa dalili zozote wakati ambapo watu hufanya mambo ya udhalimu, bado Najua kwamba udhalimu uliowekwa ndani ya mioyo yenu hushinda utajiri wa vitu vyote Nilivyoumba. Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani? Ninyi, minyoo wadogo wenye uvundo mnaiba sadaka kutoka kwa madhabahu ya Mimi, Yehova; kwa kufanya hivyo, mnaweza kuokoa majina yenu yaliyoharibika, yenye kasoro kuwa wateule wa Israeli? Ninyi ni mafukara wasio na haya! Hizo sadaka juu ya madhabahu zilizotolewa Kwangu na watu, kuonyesha hisia karimu kutoka kwa wale ambao hunicha Mimi. Ni za udhibiti Wangu na za matumizi Yangu, kwa hiyo inawezekanaje wewe kuniibia Mimi hua wadogo waliotolewa na watu? Je, huogopi kuwa Yuda? Je, huogopi nchi yako kuwa “konde la damu”? Wewe kitu kisicho na haya! Unadhani kwamba hua waliotolewa na watu wote ni wa kustawisha tumbo la wewe buu? Kile ambacho Nimekupa ni kile ambacho Nimefurahia na kuwa radhi kukupa wewe; kile ambacho Sijakupa kiko chini ya Mamlaka Yangu, na huwezi tu kuiba sadaka Yangu. Yule Anayefanya kazi ni Mimi, Yehova—Bwana wa uumbaji, na sababu ya watu kutoa sadaka ni Mimi. Unadhani kwamba ni fidia ya kukimbia kila mahali ambako wewe hufanya? Wewe kwa kweli ni usiye haya! Ni nani ambaye unamkimbilia kila mahali? Je, si kwa ajili yako mwenyewe? Kwa nini wewe huiba sadaka Zangu? Kwa nini wewe huiba pesa kutoka kwa mfuko Wangu wa pesa? Je, wewe si mwana wa Yuda Iskariote? Sadaka Zangu, za Yehova, ni za kufurahiwa na makuhani. Je, wewe ni kuhani? Wewe huthubutu kula kwa kujisikia sadaka Zangu na hata unazitandaza juu ya meza; huna thamani yoyote! Wewe fukara asiye na thamani! Moto Wangu, wa Yehova, utakuteketeza wewe!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

668. Nimefanya kazi na kusema kwa njia hii miongoni mwenu, Nimetumia nguvu na juhudi, ila ni wakati upi kamwe mmewahi kusikiliza kile Ninachowaambia wazi wazi? Ni wapi mmeniinamia Mimi, Mwenyezi? Kwa nini mnanitendea namna hii? Kwa nini kila kitu mnachokisema na kufanya huchochea hasira Yangu? Kwa nini, mioyo yenu imeshupaa? Je, Nimewahi kuwapiga kumbo kamwe? Kwa nini hamfanyi kitu chochote kingine ila kunifanya mwenye huzuni na wasiwasi? Mnasubiri siku ya ghadhabu Yangu, Yehova, kuja juu yenu? Je, mnanisubiri Mimi kutuma hasira kwenu iliyochochewa na makosa yenu? Si kila kitu Ninachokifanya ni kwa ajili yenu? Ilhali kila wakati mmenitendea Mimi, Yehova, kwa njia hii: kuiba sadaka Yangu, kuchukua sadaka ya madhabahu Yangu nyumbani kwa jamii ya mbwa mwitu kuwalisha wana wa mbwa mwitu na vitukuu vyake; watu wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wakikabiliana na mtazamo wa hasira kwa panga na mikuki, kurusha maneno ya Mimi, Mwenyezi, kwenye choo kuwa machafu kama kinyesi. Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu umekuwa unyama! Mioyo yenu kwa muda mrefu imegeuka kuwa jiwe. Je, hamjui kwamba siku Yangu ya ghadhabu itakapofika itakuwa ndio wakati Nitakapokuhukumu mabaya mliyotenda dhidi Yangu leo, Mwenyezi? Je, mnafikiri kwamba kwa kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa kutupa maneno Yangu katika matope na kutoyasikiza—unafikiri kwamba kwa kutenda namna hii nyuma Yangu mnaweza kutoroka macho Yangu ya ghadhabu? Je, hamjui kwamba mlishaonekana na macho Yangu, Mimi Yehova, wakati mliiba sadaka Yangu na kutamani mali Yangu? Je, hamjui kwamba wakati mliiba sadaka Yangu, ilikuwa mbele ya madhabahu ambapo dhabihu hutolewa? Mnawezaje kujiamini wenyewe mlivyo wajanja kutosha kunidanganya Mimi kwa njia hii? Ghadhabu Yangu kali ingewezaje kuondoka kutoka katika dhambi zenu za kuchukiza? Ghadhabu Yangu yenye hasira ingepitaje juu ya matendo yenu maovu? Maovu mnayotenda leo hayawafungulii njia yenu kutokea, bali huhifadhi kuadibu kwa ajili ya kesho yenu; yanachochea kuadibu Kwangu, Mwenyezi, kwenu. Matendo yenu maovu na maneno yenu mabaya yangewezaje kuepuka kuadibu Kwangu? Maombi yenu yangeyafikiaje masikio Yangu? Ningefunguaje njia kwa ajili ya udhalimu wenu? Ningewezaje kuyatupilia mbali matendo yenu maovu ya kunikaidi? Ingewezekanaje Nisizikate ndimi zenu ambazo ni za sumu kama ya nyoka? Hamniombi msaada kwa ajili ya haki yenu, lakini badala yake mnahifadhi ghadhabu Yangu kama matokeo ya udhalimu wenu. Ningewezaje kuwasamehe? Katika macho Yangu, Mwenyezi, maneno na matendo yenu ni machafu. Macho Yangu, Mwenyezi, huona udhalimu wenu kama kuadibu kusikolegea. Kuadibu Kwangu kwa haki na hukumu vingeondokaje kwenu? Kwa sababu mmenitendea hivi, na kunifanya mwenye huzuni na ghadhabu, Ningewaachaje nyinyi muepe kutoka mikono Yangu na muondoke katika siku ambayo Mimi, Yehova, Nawaadibu na kuwalaani wewe? Je, hamjui kwamba maneno yenu yote mabaya na matamko tayari yamefikia masikio Yangu? Je, hamjui kwamba udhalimu wenu tayari umelilaghai vazi Langu takatifu la haki? Je, hamjui kwamba makosa yenu tayari yameichochea hasira Yangu kali? Je, hamjui kwamba kwa muda mrefu mmeniacha Nikitokota, na kwa muda mrefu mmeujaribu uvumilivu Wangu? Je, hamjui kwamba tayari mmeshauharibu mwili Wangu kuwa matambara? Nimevumilia mpaka sasa, kiasi kwamba Natoa hasira Zangu, kutokuwa mvumilivu kwenu tena. Je, hamjui kwamba matendo yenu maovu tayari yamefikia Macho Yangu, na kwamba kilio changu tayari kimefikia masikio ya Baba Yangu? Angewaruhusu vipi mnitendee Mimi jinsi hii? Kuna kazi yoyote Ninayofanya ndani yenu isiyo kwa ajili yenu? Ilhali nani kati yenu amekuwa na upendo zaidi kwa kazi Yangu, Yehova? Ningeweza kutokuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Baba Yangu kwa sababu Mimi ni mnyonge, na kwa sababu ya uchungu Nilioupitia? Je, hamwelewi Moyo Wangu? Nasema na ninyi kama Yehova alivyofanya; je, Sijajinyima mengi kwa ajili yenu? Hata ingawa Niko tayari kuvumilia mateso haya yote kwa ajili ya kazi ya Baba Yangu, ni jinsi gani nyinyi mnaweza kuachwa huru kutokana na kuadibu ambako Nawaleteeni kama matokeo ya mateso Yangu? Je, hamjanifurahia kwa wingi sana? Leo, Nimetolewa kwenu na Baba Yangu; hamfahamu kwamba mnafurahia zaidi ya maneno Yangu mengi? Je, hamjui kwamba maisha Yangu yalibadilishwa na maisha yenu na mambo yote mnayofurahia? Je, hamjui kwamba Baba Yangu alitumia maisha Yangu kupigana na Shetani, na kwamba Yeye pia ametoa maisha Yangu kwenu, na kusababisha nyinyi kupokea mara mia zaidi, na kuwaruhusu kuepuka majaribu mengi? Je, hamjui kwamba ni kwa njia ya Kazi Yangu kwamba mmepewa msamaha kutokana na vishawishi vingi, na kuadibu kwingi kukali? Je, hamjui kwamba ni kwa sababu Yangu tu ndio Baba Yangu anawaruhusu kufurahia mpaka sasa? Jinsi gani mmebaki wagumu na wasiyoyumba leo, kiasi kwamba ni kana kwamba ugume umemea rohoni mwenu? Maovu mnayoyatenda leo yangeepukaje siku ya ghadhabu itakayofuata kuondoka Kwangu duniani? Ningewezaje kuwaruhusu wale ambao ni wagumu na wasiokubali kuepuka hasira ya Yehova?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

669. Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi? Ni wakati upi Nimewakaripia bila mantiki? Ni wakati upi Nimewakemea usoni mwenu? Je, si ni kwa ajili ya kazi Yangu ndio kwamba Mimi namwomba Baba Yangu kuwaweka mbali na majaribu? Kwa nini mnanitendea Mimi hivi? Je, Nimewahi kutumia mamlaka Yangu kuipiga miili yenu? Kwa nini mnanilipa Mimi kwa njia hii? Baada ya ninyi kuwa moto na baridi Kwangu, nyinyi si moto wala baridi, na kisha mnajaribu kunirairai Mimi na kuficha mambo kutoka Kwangu, na vinywa vyenu vimejaa mate ya wasio haki. Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kumdanganya Roho Wangu? Je, mnafikiri kwamba ndimi zenu zinaweza kuepuka ghadhabu Yangu? Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kupitisha hukumu kwa matendo Yangu, Yehova, jinsi zinavyopenda? Je, Mimi ni Mungu ambaye mwanadamu hupishia hukumu? Ningewezaje kuruhusu buu dogo linikufuru hivyo? Ningewezaje kudai wana wa uasi kuwa miongoni mwa baraka Zangu za milele? Maneno na matendo yenu kwa muda mrefu yamewafichua na kuwahukumu. Wakati Nilieneza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe yeyote kushiriki atakavyo, sembuse kuruhusu jambo lolote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu, vile linavyopenda. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kuwasamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Je, majaliwa ya mwanadamu hayako katika mikono Yangu, Mwenyezi? Ningeuchukua vipi udhalimu wako na uasi kama vitu vitakatifu? Jinsi gani dhambi zako zingenajisi utakatifu Wangu? Mimi sijanajisika na uchafu wa wasio haki, wala kufurahia sadaka ya wasio haki. Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kukufuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu? Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Mngewezaje kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kuwaruhusu kunipinga na kuniasi kwa njia hii, mara kwa mara? Nawaambia wazi, siku itakapokuja, basi kuadibu kwenu kutakuwa kusikovumilika zaidi kuliko ile ya Misri! Mnawezaje kuitoroka siku ya ghadhabu Yangu? Nawaambia kwa kweli: Uvumilivu Wangu ulitayarishwa kwa ajili ya matendo yenu maovu, na upo kwa ajili ya kuadibu kwenu siku hiyo. Je, ninyi si wale mtakaopata hukumu ya ghadhabu Yangu punde Nifikapo mwisho wa uvumilivu Wangu? Si mambo yote yapo mikononi Mwangu, Mwenyezi? Ningewezaje kuwaruhusu mniasi hivyo, chini ya mbingu? Maisha yenu yatakuwa magumu sana kwa kuwa mmekutana na Masiha, ambaye ilisemekana Angekuja, lakini ambaye kamwe Hakuja. Je, si nyinyi ni maadui Wake? Yesu amekuwa rafiki wenu, lakini bado mu maadui wa Masiha. Je, hamjui kwamba ingawa nyinyi ni marafiki wa Yesu, matendo yenu maovu yamejaza vyombo vya wale ambao ni wa karaha? Ingawa nyinyi mu karibu sana na Yehova, je, hamjui kwamba maneno yenu mabaya yamefikia masikio ya Yehova na kuchochea ghadhabu Yake? Ingekuwaje awe karibu nawe, na jinsi gani Yeye asingevichoma hivyo vyombo vyako, ambavyo vimejaa matendo mabaya? Ingekuwaje Asiwe adui wako?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

670. Ninyi nyote huketi kwenye viti vya umbuji, mkiwakaripia wale wa vizazi vidogo ambao ni wa namna yenu na mkiwafanya waketi pamoja nanyi. Ila hamjui kwamba “wazawa” wenu waliishiwa na pumzi kitambo sana na kuipoteza kazi Yangu. Utukufu Wangu unang’aa kutoka katika nchi ya Mashariki hadi katika nchi ya Magharibi, lakini utakapoenea hadi miisho ya dunia na kuanza kuinuka na kuangaza, Nitauchukua utukufu Wangu kutoka Mashariki na kuuleta Magharibi ili kwamba watu waovu, ambao wamenitelekeza huko Mashariki watanyimwa mwangaza kuanzia wakati huo na kuendelea. Hilo litakapofanyika, mtaishi katika bonde la kivuli. Hata ingawa watu siku hizi ni bora mara mia moja kuliko hapo awali, bado hawawezi kutimiza matakwa Yangu, na bado wao sio ushuhuda kwa utukufu Wangu. Kwamba mnaweza kuwa bora mara mia moja kuliko hapo awali ni matokeo ya kazi Yangu kabisa; ni matunda yatokanayo na kazi Yangu duniani. Hata hivyo, bado Ninahisi kuchukizwa na maneno na matendo yenu, na vile vile na tabia yenu, na Ninahisi chuki kubwa sana kuhusu jinsi mnavyotenda mbele Yangu, kwa kuwa hamna ufahamu wowote kunihusu. Basi, mnawezaje kuja kuishi kwa kudhihirisha utukufu Wangu, na mnawezaje kuwa waaminifu kabisa kwa kazi Yangu ya baadaye? Imani yenu ni ya kupendeza sana; mnasema kwamba mko tayari kutumia maisha yenu yote kwa ajili ya kazi Yangu, na kwamba mko tayari kutoa maisha yenu kwa ajili ya kazi hiyo, lakini tabia zenu hazijabadilika sana. Mnazungumza tu kwa kiburi, licha ya ukweli kwamba tabia yenu halisi ni mbovu sana. Ni kana kwamba ndimi na midomo ya watu iko mbinguni lakini miguu yao iko chini duniani, na kwa sababu hiyo, maneno na matendo yao na sifa zao bado ni mbovu na zisizoheshimika. Sifa zenu zimeharibiwa, tabia yenu imepotoka, njia yenu ya kuzungumza ni duni, na maisha yenu ni yenye kustahili dharau; hata ubinadamu wenu wote umezama katika hali duni ya chini kabisa. Ninyi ni wenye mawazo finyu kuhusu wengine, na ninyi hubishana kuhusu kila jambo dogo. Ninyi hugombana kuhusu heshima na hadhi zenu wenyewe, hadi kufikia kiwango ambapo mko tayari kushuka kuzimuni na kuingia kwenye ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha Mimi kubaini kwamba ninyi ni wenye dhambi. Mitazamo yenu kwa kazi Yangu inatosha Mimi kubaini kuwa ninyi ni wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kuonyesha kwamba ninyi ni watu wachafu mliojaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua vinatosha kusema kwamba ninyi ni watu ambao mmekunywa damu ya roho wachafu hadi mkatosheka. Kuingia katika ufalme kunapotajwa, hamfichui hisia zenu. Je, mnaamini ya kwamba jinsi mlivyo sasa inatosha kwa ninyi kupita katika lango la kuingia katika ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini ya kwamba mnaweza kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu, bila maneno na matendo yenu wenyewe kujaribiwa na Mimi kwanza? Ni nani anayeweza kunihadaa? Tabia na mazungumzo yenu yenye kustahili dharau na yaliyo duni yanaweza kuepukaje macho Yangu? Maisha yenu yamebainiwa na Mimi kuwa maisha ya kunywa damu na kula nyama ya roho hao wachafu kwa sababu ninyi huwaiga mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu, tabia yenu imekuwa mbaya hasa, kwa hiyo Ninawezaje kukosa kuwaona kuwa wenye kuchukiza? Maneno yenu yana uchafu wa roho wachafu: Mnabembeleza, kuficha na kujipendekeza kama tu wale wanaoshiriki katika uchawi na kama wale walio wadanganyifu na wanaokunywa damu ya wadhalimu. Maonyesho yote ya mwanadamu ni dhalimu mno, kwa hivyo watu wote wanaweza kuwekwaje katika nchi takatifu ambako wenye haki wako? Je, unafikiri kwamba hiyo tabia yako yenye kustahili dharau inaweza kukubainisha kama mtakatifu ikilinganishwa na wale wadhalimu? Ulimi wako ulio kama wa nyoka hatimaye utauangamiza huu mwili wako ambao huleta uharibifu na kutekeleza machukizo, na hiyo mikono yako iliyojaa damu ya roho wachafu pia hatimaye itaipeleka roho yako jahannamu. Basi, kwa nini huipokei kwa furaha nyingi fursa hii ili uitakase mikono yako iliyojaa uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kwa manufaa yako uukate huo ulimi wako unaozungumza maneno ya kudhulumu? Je, inawezekana kwamba uko tayari kuteseka katika moto wa jahannamu kwa ajili ya mikono, ulimi na midomo yako? Mimi huuchunga moyo wa kila mtu kwa macho yote mawili, kwa sababu muda mrefu kabla Niwaumbe wanadamu, Nilikuwa nimeifumbata mioyo yao mikononi Mwangu. Nilikuwa nimeibaini mioyo ya watu kitambo, kwa hiyo mawazo yao yangeyaepukaje macho Yangu? Muda utakosaje kuwa umewaishia wa kuepuka kuchomwa na Roho Wangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

671. Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina? Kazi Yangu kwa kweli ni ya nani? Inawezekana kuwa tu ni ya kuwapiga nyinyi nyote ili kufichua mamlaka Yangu? Je, si maisha yenu yameshikiliwa na neno moja kutoka Kwangu? Ni kwa nini Ninatumia maneno tu kuwaagiza na Sijayageuza maneno kuwa ukweli ili kuwapiga haraka iwezekanavyo? Je, maneno Yangu na kazi Yangu ni ya kuwapiga wanadamu tu? Je, Mimi ni Mungu ambaye huwaua wasio na hatia bila ubaguzi? Hivi sasa, ni wangapi wenu ambao wako hapo mbele Yangu ambao wanatafuta njia sahihi ya maisha ya mwanadamu na nafsi zao nzima? Ni miili yenu tu iliyo mbele Yangu, lakini mioyo yenu iko huru, na iko mbali, mbali na Mimi. Kwa sababu hamjui kwa kweli kazi Yangu ni nini, kuna baadhi yenu ambao mnataka kuondoka Kwangu, mnaojitenga na Mimi, na mnataka kuishi katika mahali hapo pa raha ambapo hakuna kuadibu, hakuna hukumu. Je, hili ndilo watu wanatamani katika mioyo yao? Mimi hakika sikulazimishi. Njia yoyote utakayoichukua ni uchaguzi wako mwenyewe, na njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Niliyowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

672. Nafsi zote zilizopotoshwa na Shetani zimeshikwa mateka katika miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa, waliookolewa kutoka katika kambi ya Shetani, na kuletwa ndani ya ufalme wa leo. Watu hawa hawaishi tena chini ya ushawishi wa Shetani. Hata hivyo, asili ya mwanadamu bado imekita mizizi katika mwili wa mwanadamu, yaani, ingawa nafsi zenu zimeokolewa, asili yenu bado ni kama ilivyokuwa awali, na uwezekano kwamba mtanisaliti unabaki kuwa asilimia mia moja. Hii ndiyo sababu kazi Yangu hudumu kwa muda mrefu sana, kwa kuwa asili yenu haiwezi kudhibitiwa kwa urahisi. Sasa, ninyi nyote mnapitia shida kadri ya uwezo wenu mnapotimiza wajibu wenu, ilhali kila mmoja wenu anaweza kunisaliti na kurudi katika miliki ya Shetani, kambini mwake, na kurudia maisha yenu ya zamani—huu ni ukweli usiopingika. Wakati huo, haitawezekana kwenu kudhihirisha chembe ya ubinadamu au mfano wa binadamu, kama mnavyofanya sasa. Katika hali mbaya zaidi, mtaangamizwa, na zaidi ya hayo, mtahukumiwa milele, mwadhibiwe vikali, msizaliwe upya kamwe. Hii ndiyo shida iliyowekwa mbele yenu. Ninawakumbusha kwa njia hii, kwanza, ili kazi Yangu isiwe imekuwa bure, na pili, ili ninyi nyote mweze kuishi katika siku za nuru. Kwa kweli, kama kazi Yangu ni bure si tatizo la muhimu sana. Kilicho cha muhimu sana ni kwamba mnaweza kuwa na maisha yenye furaha na mustakabali mzuri sana. Kazi Yangu ni kazi ya kuziokoa nafsi za watu. Nafsi yako ikianguka mikononi mwa Shetani, mwili wako hautaishi kwa amani. Ikiwa Ninaulinda mwili wako, hakika nafsi yako pia itakuwa chini ya uangalizi Wangu. Nikikuchukia sana, mwili na nafsi yako vitaanguka mikononi mwa Shetani mara moja. Je, unaweza kukisia hali yako wakati huo? Ikiwa, siku moja mtayapuuza maneno Yangu, basi Nitawakabidhi nyote kwa Shetani, ambaye atawatesa sana hadi hasira Yangu itakapoisha kabisa, au Mimi binafsi Nitawaadhibu ninyi wanadamu wasioweza kuokoleka, kwa kuwa mioyo yenu inayonisaliti haitakuwa imewahi kubadilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

673. Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mnaweza kutekeleza kwa kujitokeza, kujitoa kikamilifu, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote muwe na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwenu nyinyi mfanye uamuzi bora kabisa katika kujitoa Kwangu pekee na moyo wa ibada ya mwisho. Kama mtu hana moyo huo wa ibada pekee, mtu huyo hakika atakwenda kuwa thamani ya Shetani, na Mimi Sitaendelea kumtumia. Nitamtuma nyumbani akatunzwe na wazazi wake. Kazi yangu imekuwa ya msaada sana kwa ajili yenu; kile Natarajia kupata kutoka kwenu ni moyo ulio mwaminifu na unaotia msukumo kwenda juu, lakini hadi sasa mikono Yangu bado ni tupu. Fikiria kulihusu: Wakati siku moja bado Nitakuwa na kukwazika kusikoelezeka, mtazamo Wangu kuwaelekea utakuwa upi? Je, Mimi bado Nitakuwa mwema? Je, Moyo wangu utakuwa bado mtulivu? Je, mnaelewa hisia za mtu ambaye kwa kujitahidi amelima lakini hakuvuna hata nafaka moja? Je, mnaelewa ukubwa wa jeraha la mtu ambaye amepigwa kipigo kikubwa? Je, mnaweza kuonja uchungu wa mtu aliyejawa na matumaini ambaye anafaa kuachana na mtu kwa uhusiano mbaya? Je, mmeona hasira ya mtu ambaye amekasirishwa? Je, mnaweza kujua hisia ya kulipiza kisasi kwa haraka ya mtu ambaye amekuwa akichukuliwa kwa uadui na udanganyifu? Kama mnaelewa fikira za watu hawa, Nadhani haipaswi kuwa vigumu kwenu kuwaza mtazamo Mungu Atakuwa nao wakati ule wa adhabu Yake. Hatimaye, Natarajia nyote mnaweka jitihada kali kwa ajili ya hatima yenu wenyewe; hata hivyo, ni bora msitumie njia za udanganyifu katika juhudi zenu, au bado Nitasikitishwa nanyi katika moyo Wangu. Je, kusikitishwa kwa aina hii huelekea wapi? Je, hamjidanganyi wenyewe? Wale ambao hufikiria kuhusu hatima yao na bado wanaiharibu ni watu wenye uwezekano mdogo zaidi wa kuokolewa. Hata kama watu hawa watakerwa, ni nani atawahurumia? Kwa jumla, bado Niko tayari Kuwatakia muwe na hatima inayofaa na nzuri. Hata zaidi, Natarajia kwamba hakuna kati yenu atakayeanguka katika maafa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

674. Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Tanbihi:

a. Kipande cha mti mkavu: nahau ya Kichina inayomaanisha “hali isiyo na matumaini.”

Iliyotangulia: B. Kushawishi kwa Mungu wa Mwanadamu

Inayofuata: XIV. Maneno Juu ya Viwango vya Mungu vya Kuyafafanua Matokeo ya Mwanadamu na juu ya Mwisho wa Mtu wa Kila Aina

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp