672 Majaribio ya Mungu kwa Wanadamu ni ili Kuwatakasa
1 Katika imani yao kwa Mungu, kile ambacho watu hutafuta ni kupata baraka kwa ajili ya siku zijazo; hili ndilo lengo lao katika imani yao. Watu wote wana kusudi na tumaini hili, lakini upotovu ulio katika asili yao lazima uondolewe kupitia majaribu. Katika hali ambazo bado hujatakaswa, hizi ndizo hali ambamo lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili uweze kujua upotovu wako mwenyewe. Hatimaye, unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu. Kwa hiyo, ikiwa watu hawana miaka kadhaa ya usafishaji, wasipovumilia kiwango fulani cha mateso, hataweza kujiondolea vifungo vya upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yake.
2 Katika hali zozote zile ambazo bado ungali mtumwa wa Shetani, na katika hali zozote zile ambazo bado ungali na tamaa zako mwenyewe na matakwa yako mwenyewe, hizi ndizo hali ambamo unapaswa kuteseka. Ni kupitia mateso tu ndiyo mafunzo yanaweza kupatikana, kuweza kupata ukweli, na kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika kwa kupitia majaribu makali. Hakuna anayeweza kufahamu mapenzi ya Mungu, kutambua uweza na busara ya Mungu, wala kuiona tabia ya haki ya Mungu anapokuwa katika mazingira ya utulivu na rahisi au wakati hali ni nzuri. Hilo halingewezekana! Ikiwa watu hawana miaka kadhaa ya usafishaji, wasipovumilia kiwango fulani cha mateso, hataweza kujiondolea vifungo vya upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yake.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Mtu Anapaswa Kumridhisha Mungu Katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo