940 Tabia ya Haki ya Mungu ni Halisi na Dhahiri

1 Tabia ya Mungu ni kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au sanamu ya udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe mwenye uhai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Angeweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi msiba na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao.

2 Fikira za Mungu zinabadilika siku zote kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, vipengele tofauti vya kiini cha Mungu vitafichuliwa. Katika kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye hufichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake mwenyewe wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, wema Wake na uvumilivu Wake.

3 Kiini Chake kitafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia Yake ya haki hairuhusiwi kushukiwa, kukiukwa, kubadilishwa au kupotoshwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi vipengele hivi katika kila sehemu ya asili na kuzitekeleza kila wakati kwa uwazi.

4 Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka na muda au nafasi, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kama inavyoongozwa na mipaka ya muda au nafasi. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kukoma kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inajumuisha maneno matupu? Wakati Mungu anapoonyesha hasira kali na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu?

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 939 Ishara ya Tabia ya Mungu

Inayofuata: 941 Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp