941 Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee
1 Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za binafsi za kipekee; Hategemei kudhibitiwa au kuzuiliwa na watu, matukio au mambo yoyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi Yeye na kubadilisha uamuzi wowote Wake.
2 Uzima wa tabia na fikira za uumbaji upo katika hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama atatumia hasira au huruma; ni kiini cha Muumba tu—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—kinaweza kuamua hili. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
3 Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; ni isiyokosewa pamoja na kushukiwa; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyokosewa Vivyo hivyo.
4 Kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, anavyoweza kubadilisha au kuwakilisha Mungu katika vitendo Vyake, wala hakuna yeyote anayeweza kubadilisha au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili