935 Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu
1 Kila kitendo ambacho Mungu hufanya kina hali Yake ya uenyezi ndani yake, na pia kina hali Yake ya utendaji. Uenyezi wa Mungu ni kiini Chake, lakini utendaji Wake pia unajumuisha upande mmoja wa kiini Chake; hali hizi mbili hazitenganishwi. Mungu kufanya matendo katika uhalisi ni hali Yake ya vitendo ikitekeleza kazi, na kwamba Anaweza kufanya kazi kwa njia hii ni hali Yake ya uenyezi. Kitu chochote ambacho Mungu hufanya kina hali hizo mbili za uenyezi Wake na utendaji Wake, na yote hutekelezwa kulingana na kiini Chake; ni maonyesho ya tabia Yake, na ni ufunuo wa kiini Chake na kile Alicho.
2 Uwezo wa Mungu wa kufanya kazi Yake kwa kweli na kwa vitendo, na kutakasa na kutatua upotovu wa binadamu kwa kuonyesha ukweli, na pia Yeye kuweza kuwaongoza watu moja kwa moja—mambo haya yanaonyesha upande Wake wa vitendo. Mungu hufanya kazi katika uhalisi, Yeye huonyesha tabia Yake mwenyewe na kile Alicho. Kazi yoyote asiyoweza kuifanya mwanadamu, Yeye anaweza kuifanya, na hili linahusu hali Yake ya uenyezi. Maneno anayonena Mungu yana hali Yake ya uenyezi na Yeye hushika mamlaka Yake, akikamilisha Anachosema Atakamlisha. Ni wazi kwamba matokeo ya mwisho yatakuwa nini; Anaponena maneno haya, uenyezi Wake hufichuliwa. Mungu hutawala vitu vyote, humfanya Shetani amtumikie, hupanga mazingira ili kuwajaribu na kuwasafisha watu, na kuzitakasa na kubadili tabia zao—haya yote ni maonyesho ya upande wa Mungu wenye uweza. Kiini cha Mungu Mwenyewe ni uenyezi pamoja na vitendo, na hali hizi mbili hutimizana. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni maonyesho ya tabia Yake na ni ufunuo wa kile Alicho. Kile Alicho kinahusisha uenyezi Wake, haki Yake na adhama Yake.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo