VII. Maneno Juu ya Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho

255. Kila alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, tulizo kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye ambaye hawezi kukosewa (wala Hatavumilia kukosewa)[b] na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanao uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu ni ishara tu ya mamlaka kidogo ya binadamu juu ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali katika dutu yake ni yule ambaye kwa woga yuko chini ya watu, matukio na mambo ya kila aina. Raha ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa wanadamu; raha Yake ni raha ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi, ishara ya fadhili. Hasira ya Mungu inatokana na uharibifu ambao kuwepo na kuingilia kwa dhuluma kunaleta kwa wanadamu Wake, kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na chema. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule mwanadamu mzuri lakini mwenye upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu hupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kutoka wakati huu kuendelea, na ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote huibuka kwa ajili ya masilahi yake mwenyewe, na wala si kwa ajili ya haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, sembuse neema inayotolewa na Mbinguni. Hisia za wanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa hapohapo. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na ni mwenye heshima kila wakati, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote asiye na thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa wanadamu; mwanadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na kujitahidi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia kwa dhati kuendelea kuishi kwa wanadamu, ilhali mwanadamu kamwe hachangii kitu kwa ajili ya mwangaza au haki. Hata kama mwanadamu anajitahidi sana kwa muda, ni dhaifu sana kiasi cha kutoweza kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mwenye ubinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vya uzuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

256. Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe. Msiwe na hamu sana ya matokeo ya haraka, kazi Yangu si kitu ambacho kinaweza kufanywa mara moja. Ndani yake kuna hatua Zangu na hekima Yangu, hivyo hekima Yangu inaweza kufichuliwa. Nitawawezesha kuona ni nini kinachofanywa kwa mikono Yangu—kuadhibu uovu na kuzawadia mema. Mimi hakika Simpendelei mtu yeyote. Ninakupenda kwa dhati wewe unayenipenda kwa dhati, na ghadhabu Yangu daima itakuwa pamoja na wale wasionipenda kwa dhati, ili kwamba waweze kukumbuka daima kwamba Mimi ni Mungu wa kweli, Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu. Usitende kwa njia moja mbele ya wengine na utende kwa namna nyingine bila wao kufahamu; Ninaona wazi kila kitu unachofanya na ingawa unaweza kuwadanganya wengine huwezi kunidanganya Mimi. Ninaona yote waziwazi. Haiwezekani kwako kuficha chochote; vyote vimo mikononi Mwangu. Usifikiri kuwa wewe ni mjanja sana, kwa kufanya hesabu zako ndogondogo zikufaidi. Nakwambia: Haijalishi mwanadamu anaweza kubuni mipango kiasi kipi, iwe elfu kadhaa ama elfu nyingi, mwishowe hawezi kuepuka kutoka kwenye kiganja cha mkono Wangu. Vitu na matukio yote huendeshwa katika mikono Yangu, sembuse mtu mmoja! Usijaribu kuepuka au kujificha, usijidanganye au kuficha. Je, huwezi kuona kwamba uso Wangu mtukufu, hasira Yangu na hukumu Yangu imefichuliwa hadharani? Nitahukumu mara moja na bila huruma wale wote ambao hawanitaki Mimi kwa dhati. Huruma Yangu imefika mwisho na hakuna tena iliyobaki. Usiwe mnafiki tena na acha njia zako za kishenzi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 44

257. Mimi ndiye mwanzo, na Mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyefufuka na kamili. Nasema maneno Yangu mbele yenu, na lazima muamini Ninachosema kwa thabiti. Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au mstari mmoja wa kile Ninachosema kitawahi kupita. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Punde ambapo Nimesema, hakuna neno hata moja limewahi kurudishwa na kila neno litatimizwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 53

258. Ulimwengu na vitu vyote vimo mikononi Mwangu. Kama Nikisema, itakuwa. Kama Nikiliamua, ndivyo litakavyokuwa. Shetani yu chini ya miguu Yangu, yu katika kuzimu! Sauti Yangu itakapotoka, mbingu na nchi zitapita na kuwa bure! Mambo yote yatafanywa upya na huu ni ukweli wa kweli sana usiobadilika. Nimeushinda ulimwengu, kuwashinda waovu wote. Naketi hapa nikizungumza nanyi; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza na wale wote wanaoishi wanapaswa kukubali.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 15

259. Kile Nilichosema lazima kihesabiwe, kile kilichohesabiwa lazima kikamilishwe, na hili haliwezi kubadilishwa na yeyote; hili ni thabiti. Kama ni kile Nilichosema katika wakati uliopita au Nitakachosema katika siku za usoni, yote yatatimia, na wanadamu wote wataliona hili. Hii ni kanuni inayoelekeza maneno na kazi Yangu. … Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu? Chochote Nisemacho hufanyika, na miongoni mwa wanadamu, ni nani aliyepo anayeweza kuyabadilisha mawazo Yangu? Yaweza kuwa agano Nililofanya juu ya dunia? Hakuna chochote kinachoweza kuuzuia mpango Wangu; Mimi huwepo wakati wote katika kazi Yangu na vilevile katika mpango wa usimamizi Wangu. Ni mwanadamu gani anaweza kuingilia? Je, sio Mimi binafsi Niliyetengeneza mipango hii? Kuingia katika hali hii leo, bado haipotei kutoka kwa mpango Wangu au Nilichoona mbele; yote iliamuliwa Nami zamani sana. Ni nani miongoni mwenu anaweza kufahamu mpango Wangu wa hatua hii? Watu Wangu wataisikiliza sauti Yangu, na kila mmoja wa wale wanaonipenda kwa kweli atarudi mbele ya kiti Changu cha enzi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1

260. Ninawapenda wote wanaojitumia na kujitoa wenyewe kwa dhati kwa ajili Yangu. Nawachukia wale wote waliozaliwa kutoka Kwangu ila bado hawanijui Mimi, na hata wananipinga Mimi. Sitamwacha yeyote ambaye kwa dhati yuko kwa ajili Yangu; badala yake, baraka zake Nitazifanya ziwe mara dufu. Nitawaadhibu mara dufu wale wasio na shukrani na wanaokiuka fadhila Zangu, na sitawaachilia kwa urahisi. Katika ufalme Wangu hakuna upotovu au udanganyifu, na hakuna udunia; yaani, hakuna harufu ya wafu. Badala yake, yote ni unyofu na haki; yote ni usafi na uwazi, bila kuwa na chochote kilichofichika au kisicho wazi. Kila kitu ni kipya, kila kitu ni starehe, na kila kitu ni cha kujenga. Yeyote ambaye bado ananuka wafu hawezi kamwe kubakia katika ufalme Wangu, na badala yake atatawaliwa na fimbo Yangu ya chuma.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 70

261. Mimi ni moto uteketezao na Sivumilii kosa. Kwa sababu wanadamu wote waliumbwa na Mimi, chochote Nisemacho na kufanya, watu lazima watii na hawawezi kukiasi. Watu hawana haki ya kuingilia kazi Yangu, na wao hasa siyo wenye sifa zinazostahili kuchambua kilicho cha kweli au chenye makosa katika kazi Yangu na maneno Yangu. Mimi ni Bwana wa uumbaji, na viumbe wanapaswa kutimiza kila kitu Ninachohitaji kwa moyo wa kunicha Mimi; hawapaswi kutoa sababu ili kunishawishi Mimi na wao hasa hawapaswi kunipinga. Ninatumia mamlaka Yangu kuwatawala watu Wangu, na wale wote ambao ni sehemu ya uumbaji Wangu wanapaswa kuyatii mamlaka Yangu. Ingawa leo ninyi ni, jasiri na wenye kiburi mbele Yangu, ninyi hukaidi maneno ambayo Nawafunzia, na hamwogopi, Mimi hukumbana tu na uasi wenu na uvumilivu. Singekasirika na kuathiri kazi Yangu kwa sababu mabuu wadogo sana walipindua uchafu katika rundo la samadi. Mimi huvumilia kuendelea kuwepo kwa kila kitu ambacho Mimi huchukia kabisa na mambo ambayo Mimi huchukia kabisa kwa ajili ya mapenzi ya Baba Yangu, mpaka matamshi Yangu yawe kamili, mpaka dakika Yangu ya mwisho kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

262. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu anayechukia uovu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo Kwangu Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kwa kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

263. Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, hata zaidi Mimi pekee ndimi nafsi ya Mungu, na Mimi, ukamilifu wa mwili, ni hata zaidi dhihirisho kamili la Mungu. Yeyote anayethubutu kutonicha, yeyote anayethubutu kunionyesha uasi katika macho yake, yeyote anayethubutu kuyasema maneno ya uasi dhidi Yangu hakika atakufa kutokana na laana Yangu na ghadhabu (kutakuwa na kulaani kwa sababu ya ghadhabu Yangu). Na yeyote anayethubutu kutokuwa mwaminifu au na upendo Kwangu, yeyote anayethubutu kujaribu kunifanyia hila hakika atakufa katika chuki Yangu. Haki Yangu, uadhama na hukumu vitadumu milele na milele. Mwanzoni, Nilikuwa mwenye upendo na rehema, lakini hii si tabia ya uungu Wangu kamili; haki, uadhama na hukumu ni tabia Yangu tu—Mungu Mwenyewe mkamilifu. Wakati wa Enzi ya Neema Nilikuwa mwenye upendo na rehema. Kwa sababu ya kazi Niliyopaswa kumaliza Nilikuwa na fadhila na rehema, lakini baadaye hakukuwa na haja ya fadhila yoyote au rehema (hakujakuwepo na yoyote tangu wakati huo). Yote ni haki, uadhama na hukumu na hii ni tabia kamili ya ubinadamu Wangu wa kawaida pamoja na uungu Wangu kamili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 79

264. Ninatawala vitu vyote, mimi ndiye Mungu mwenye hekima ambaye ana mamlaka kamili, na Sina huruma kwa mtu yeyote; Mimi ni katili kabisa, sina hisia za kibinafsi kamwe. Ninamtendea mtu yeyote (haijalishi anaongea vizuri namna gani, Sitamwachilia) kwa haki, uadilifu na uadhama Wangu, wakati huohuo Nikimwezesha kila mtu kuona maajabu ya matendo Yangu vizuri zaidi, na vilevile maana ya matendo Yangu. Mmoja baada ya mwingine, Niliwaadhibu pepo wabaya kwa kila aina ya matendo wanayotenda, nikiwatupa kila mmoja ndani ya shimo lisilo na mwisho. Kazi hii Niliimaliza kabla ya wakati kuanza, nikawaacha bila nafasi, nikiwaacha bila mahali pa kufanya kazi yao. Hakuna hata mmoja wa watu Wangu wateule—wale waliojaliwa na kuchaguliwa na Mimi—anayeweza kupagawa kamwe na roho waovu, na badala yake atakuwa mtakatifu daima. Lakini kwa wale ambao Sijawajalia na kuwachagua, Nitawakabidhi kwa Shetani, na sitaruhusu wabakie tena. Katika vipengele vyote, amri Zangu za kiutawala zinajumuisha haki Yangu na uadhama Wangu. Sitamwachilia hata mmoja wa wale ambao Shetani anatenda kazi kwao, lakini nitawatupa pamoja na miili yao kuzimuni, kwa maana namchukia Shetani. Sitamwachilia kwa urahisi hata kidogo, lakini nitamwangamiza kabisa, nisimruhusu hata fursa ndogo kabisa kufanya kazi yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 70

265. Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. Ndani Yangu kila kitu ni cha wazi; chochote Ninachosema kukamilisha kinakamilika na chochote Ninachosema kuanzisha kinaanzishwa, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuiga mambo haya kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa pekee.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 96

266. Nitawaadhibu waovu na kuwatuza wazuri, Nitaleta mamlakani haki Yangu nami Nitatekeleza hukumu yangu. Nitatumia maneno Yangu kukamilisha kila kitu na kumfanya kila mtu na kila kitu kipitie mkono Wangu unaoadibu. Nitawafanya watu wote wauone utukufu Wangu mzima, waione hekima Yangu nzima, wauone ukarimu Wangu mzima. Hakuna mtu yeyote atathubutu kusimama kutoa hukumu kwani yote imekamilika nami. Katika hili, kila mtu ataiona heshima Yangu yote na wote watapata uzoefu wa ushindi Wangu wote kwa kuwa kila kitu kimewekwa wazi nami. Kutokana na haya, mtu anaweza kuuona uwezo Wangu mkubwa vizuri, na kuyaona mamlaka Yangu. Hakuna mtu atathubutu kunikosea Mimi, hakuna mtu atathubutu kunizuia Mimi. Yote yamewekwa waziwazi nami, nani angethubutu kuficha kitu chochote? Nina uhakika wa kutomwonyesha huruma! Mafidhuli mno kama wao lazima waipokee adhabu Yangu kali na watu wabaya kabisa kama wao lazima waondolewe kutoka machoni Pangu. Nitawatawala kwa fimbo ya chuma nami Nitayatumia mamlaka Yangu kuwahukumu, bila huruma yoyote na bila kutowaudhi kabisa, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe Nisiye na hisia na ambaye ni mwadhimu na Siwezi kukosewa. Hii inapaswa kueleweka na wote na kuonekana na wote ili kuepuka “bila kusudi au sababu” kuangushwa nami, kuangamizwa nami, wakati utakapofika, kwa kuwa fimbo Yangu itawaangusha wote ambao wananikosea. Sitajali kama wanajua amri Zangu za utawala au la; hilo halitakuwa muhimu Kwangu kwa kuwa nafsi Yangu haiwezi kuvumilia kosa la mtu yeyote. Hii ndiyo sababu imesemwa kwamba Mimi ni simba; yeyote Ninayemgusa, Nitawaangusha. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa sasa kusema kwamba Mimi ni Mungu wa huruma na wema ni kunikufuru. Kwa asili Mimi si Mwanakondoo bali ni simba. Hakuna mtu anayethubutu kunikosea na yeyote anayenikosea Nitamwadhibu mara moja kwa kifo, bila hisia hata kidogo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 120

267. Sauti Yangu ni hukumu na ghadhabu, nami si mpole kwa yeyote na simwonei mtu yeyote huruma, kwa kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki Mwenyewe, na Mimi ni mwenye ghadhabu, Nina kuchoma, utakaso, na maangamizo. Ndani Yangu, hakuna kitu kilichofichika, au chenye mhemuko, lakini badala yake, kila kitu kiko wazi, chenye haki, na kisicho na upendeleo. Kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza tayari wako nami katika kiti cha enzi, wakitawala mataifa yote na watu wote, yale mambo na watu walio dhalimu na waovu wanaanza kuhukumiwa. Nitawafanyia uchunguzi mmoja baada ya mwingine, bila kukosa kitu chochote, Nikiwafichua kabisa. Kwa kuwa hukumu Yangu imefichuliwa kikamilifu na imefunguliwa kikamilifu, na hakuna chochote ambacho kimebakizwa; Nitatupa chochote kisichokubaliana na mapenzi Yangu na kukisababisha kiangamie kuzimu milele; Nitakisababisha kiungue kuzimu milele. Hii ni haki Yangu; huu ni uaminifu Wangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha hili, na lazima kinitii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 103

268. Kila sentensi Ninayotamka huwa na mamlaka na hukumu na hakuna mtu anayeweza kuzibadilisha. Mara tu maneno Yangu yanapotoka, mambo yatafanyika kwa mujibu wa maneno Yangu, na hii ndiyo tabia Yangu. Maneno Yangu ni mamlaka na yeyote anayeyarekebisha hukosea kuadibu Kwangu na ni lazima Nimwangamize. Hali ikiwa mbaya hayo husababisha uharibifu katika maisha yao wenyewe nao huenda kuzimu, au huenda jahanamu. Hii ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo Ninawashughulikia wanadamu na mwanadamu hawezi kuibadilisha—hii ni amri Yangu ya utawala. Kumbuka hili! Hakuna mtu anayeruhusiwa kuikosea amri Yangu; lazima hili lifanyike kulingana na mapenzi Yangu! Zamani Nilikuwa mpole sana kwenu nanyi mlikabiliwa na maneno Yangu tu. Maneno Niliyonena kuhusu kuwaangamiza watu hayajatokea bado. Lakini kuanzia leo, majanga yote (haya yanayohusiana na amri Zangu za utawala) yatatokea moja baada ya lingine ili yawaadhibu wale wote wasiotii mapenzi Yangu. Lazima kuwe na ujio wa ukweli, vinginevyo watu hawataweza kuona ghadhabu Yangu lakini watapotoshwa tena na tena. Hii ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi nayo ni njia ambayo kwayo Mimi kushughulikia hatua inayofuata ya kazi Yangu. Nawaambieni hivi mapema ili muweze kuepuka kufanya makosa na kupitia mateso milele. Hiyo ni kusema, kuanzia leo Nitawafanya watu wote ila wazaliwa Wangu wa kwanza kuchukua nafasi zao halisi kwa mujibu wa mapenzi Yangu, nami Nitawaadibu mmoja baada ya mwingine. Sitamsamehe hata mmoja wao. Hebu thubutu tu kuwa wapotovu tena! Hebu thubutu tu kuwa mwasi tena! Nimesema mbeleni kuwa Mimi ni mwenye haki kwa wote bila hisia yoyote, na huu ni mfano kwamba tabia Yangu haipaswi kukosewa. Hii ni nafsi Yangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha jambo hili. Watu wote husikia maneno Yangu na watu wote huuona uso Wangu mtukufu. Watu wote wanapaswa kunitii kabisa na kwa ukamilifu—hii ni amri Yangu ya utawala. Watu wote katika ulimwengu mzima na katika miisho ya dunia wanapaswa kunisifu na kunitukuza, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, kwa maana Mimi ni nafsi ya Mungu. Hakuna mtu anayeweza kubadili maneno na matamshi Yangu, usemi na mwenendo Wangu, kwa kuwa haya ni mambo Yangu peke Yangu, na kile ambacho Nimemiliki tangu milele na kile ambacho kitakuwepo milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 100

269. Yote yatakamilika na maneno Yangu; hakuna mwanadamu atakayekula, na hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ambayo Nitaifanya. Nitaifanya hewa ya nchi yote iwe safi na Nitatoa madoadoa yote ya mapepo duniani. Tayari Nimeanza, na Nitaanza hatua ya kwanza ya kazi Yangu ya kuadibu katika makazi ya joka kuu jekundu. Hivyo inaweza kuonekana kuwa kuadibu Kwangu kumeifikia dunia nzima, na lile joka kuu jekundu na mapepo yote machafu yatashindwa kuepuka kuadibu Kwangu, kwa kuwa Ninaziangalia nchi zote. Kazi Yangu duniani itakapokamilika, hapo ndipo, kipindi cha hukumu Yangu kitakamilika, Nitamuadibu kirasmi lile joka kuu jekundu. Watu Wangu wataona kuadibu Kwangu kwa haki kwa lile joka kuu jekundu, watamwaga sifa mbele kwa sababu ya haki Yangu, na milele watalisifu jina Langu takatifu kwa sababu ya haki Yangu. Hivyo basi, mtatenda wajibu wenu kirasmi, na mtanisifu kirasmi kotekote katika nchi, milele na milele!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28

270. Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, bali si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya lingine, njia ambayo kwayo wameitumia kunifuata, sifa zao asilia, na hatimaye jinsi ambavyo wamejistahi. Kwa njia hii, haijalishi ni mtu wa aina gani, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu, na wote watakuwa pamoja na wa aina yake kama Nilivyopanga. Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili. Sharti mtambue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa pia. Huu ni ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

271. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima iwe kuwa mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, ila badala yake imeingiza njia zako ovu ndani ya asili yako, na huna maono maradufu ya uwongo kuhusu fahari kuliko awali pekee lakini kutonielewa kwako kumeongezeka pia, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako mdogo wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya juujuu tena, lakini yamepenya ndani kwa mifupa yako. Yote yaliyosalia ni wewe kusubiri matayarisho ya mazishi yako kufanywa. Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini lile lililo kubwa sana kiasili. Wakati utakapofika, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha mbeleni. Yote yanarudia haya: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, yaani, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

272. Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha watu ambao wanafikiria kama Mimi. Wale ambao hawana fikira sawa na Zangu, wakati ule ule, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

273. Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakataza maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui Wangu wote waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni, hasira imechanganywa, Nitaukanyaga ulimwengu wote sawasawa, bila kumwacha yeyote, na kuwatia maadui Wangu hofu kubwa. Naiangamiza dunia nzima, na kuwafanya maadui Wangu waanguke katika maangamizo hayo, ili kuanzia sasa na kuendelea wasiwapotoshe wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeubadilisha. Ninapotembeatembea kwa fahari kuu ulimwenguni, wanadamu wote watafanywa wapya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwanadamu hatalia tena, hatanililia tena akitaka msaada. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 27

274. Sayuni! Salamu! Sayuni! Ita kwa sauti! Nimerudi kwa ushindi, Nimerudi nikiwa mshindi! Watu wote! Harakisheni mpange foleni kwa utaratibu! Vitu vyote! Mtakuja kusimama kabisa, kwa sababu nafsi Yangu inaukabili ulimwengu mzima na nafsi Yangu inaonekana katika Mashariki ya dunia! Nani anayethubutu kutopiga magoti katika ibada? Nani anayethubutu kutoniita Mungu wa kweli? Nani anayethubutu kutoangalia juu kwa kumcha? Nani anayethubutu kutotoa sifa? Nani anayethubutu kutangaza kwa shangwe? Watu wangu wataisikia sauti Yangu, Wanangu watasalia ndani ya ufalme Wangu! Milima, mito, na vitu vyote vitashangilia bila kukoma, na kurukaruka bila kupumzika. Wakati huu, hakuna atakayethubutu kurudi nyuma, hakuna atakayethubutu kusimama katika upinzani. Hili ni tendo Langu la ajabu, na hata zaidi ni nguvu Yangu kuu! Nitafanya kila kitu kiniche Mimi katika moyo wake na hata zaidi Nitafanya kila kinisifu Mimi. Hili ni lengo la msingi la mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, nami Nimeamua hili. Hakuna hata mtu mmoja, hakuna hata kitu kimoja wala jambo moja, linathubutu kusimama kunipinga Mimi, au linathubutu kusimama kushindana na Mimi. Watu wangu wote wataelekea mlimani Kwangu (hili linaonyesha dunia ambayo Nitaiumba baadaye) nao watatii mbele Zangu kwa sababu Ninao uadhama na hukumu, nami Nina mamlaka. (Hili linahusu wakati Niko katika mwili. Pia Ninayo mamlaka katika mwili lakini kwa sababu upungufu wa muda na nafasi hayawezi kuzidi kiwango katika mwili, kwa hiyo haiwezi kusemwa kwamba Nimepata utukufu kamili. Ingawa Nawapata wazaliwa wa kwanza katika mwili, bado haiwezi kusemwa kwamba Nimepata utukufu. Ni wakati tu Nitakaporudi Sayuni na kubadilisha sura Yangu ndipo inaweza kusemwa kwamba Nina mamlaka, yaani, Nimepata utukufu.) Hakuna kitu kitakuwa kigumu Kwangu. Kila kitu kitaharibiwa kwa maneno kutoka kinywani Mwangu, na ni kwa sababu ya maneno kutoka kinywani Mwangu ndipo yatatukia na kufanyika kamili, hiyo ni nguvu Yangu kuu na hayo ni mamlaka Yangu. Kwa sababu Nina nguvu tele na nimejawa na mamlaka, hakuna mtu anayeweza kuthubutu kunizuia Mimi. Tayari Nimepata ushindi juu ya kila kitu na Nimewashinda wana wote wa uasi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 120

275. Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake wanaothaminiwa zaidi—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si kama vikaragosi Wake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi. Wala Hahisi kwamba kuokoa binadamu, kuwatosheleza, na kuwapatia kila kitu, ni kutoa mchango mkuu kwa binadamu. Anamkimu tu mwanadamu kimyakimya na kwa unyamavu, kwa njia Yake mwenyewe na kupitia kwa kiini Chake na kile Anacho na alicho. Haijalishi ni toleo kiasi kipi na ni msaada kiasi kipi ambao wanadamu wanapokea kutoka kwa Yeye, Mungu siku zote hajawahi kufikiri kuhusu au kujaribu kutaka sifa yoyote. Hii inaamuliwa na kiini cha Mungu, na pia hasa ni maonyesho ya kweli pia ya tabia ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

276. Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amestahili vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kumlaumu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[1] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haijakuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso haya na kunyanyaswa na nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (9)

277. Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utuu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Je, si kazi Yake yote ni kwa ajili yenu, wanadamu hawa? Kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeishi na kuteswa pamoja na wenye dhambi kwa miaka mingi sana baada ya kuzaliwa horini? Na kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeurudia mwili kwa mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Je, si Mungu ni mwaminifu? Ni aina gani ya kazi Yake ambayo haijakuwa kwa ajili ya wanadamu? Ni aina gani ambayo haijakuwa kwa ajili ya kudura yako? Mungu ni mtakatifu. Hili haliwezi kubadilika! Yeye hanajisiwi na uchafu, ingawa Amekuja katika nchi yenye uchafu; yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana! Hamjui kwamba Yeye hupitia aibu kubwa sana kwa ajili yenu wote na kwa ajili ya kudura yenu? Je, hamjui hivyo? Yeye hawaokoi watu wakuu au wana wa familia tajiri na zenye uwezo, lakini Yeye huwaokoa hasa wale ambao ni wa hali za chini na wanaodharauliwa na wengine. Je, si haya yote ni utakatifu Wake? Je, si haya yote ni haki Yake? Afadhali Azaliwe katika nchi yenye uchafu na kuteseka aibu yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote. Mungu ni halisi sana—Hafanyi kazi ya uwongo. Je, si kila hatua ya kazi Yake imefanyika kwa utendaji hivi? Ingawa watu wote wanamkashifu na kusema kuwa Anakaa mezani pamoja na wenye dhambi, ingawa watu wote wanamdhihaki na kusema kuwa Anaishi na wana wa uchafu, na watu wa hali ya chini sana, bado Anajitolea bila ubinafsi, na bado Anakataliwa kwa njia hii kati ya wanadamu. Je, si mateso Anayoyahimili ni makubwa zaidi kuliko yenu? Je, si kazi Yake ni zaidi ya gharama ambayo mmelipa? Mlizaliwa katika nchi ya uchafu lakini mmepata utakatifu wa Mungu. Mlizaliwa katika nchi ambako mapepo hukusanyika lakini mmepokea ulinzi mkubwa. Je, mna uchaguzi gani mwingine? Ni malalamiko yapi mliyo nayo? Je, si mateso ambayo Amevumilia ni makubwa zaidi kuliko mateso ambayo mmevumilia?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

278. Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katika watu hawa wachafu na wapotovu, na kukikamilisha kikundi hiki cha watu. Mungu hakupata mwili tu ili kuishi na kula kati ya watu, kuwalisha watu, kutoa wanachohitaji watu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Yeye hufanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi kwa watu hawa walio na upotovu usiovumilika. Alikuja katika kiini cha joka kubwa jekundu ili kuwaokoa watu hawa wapotovu mno, ili watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Tatizo kubwa ambalo Mungu huvumilia siyo tu shida ambayo Mungu mwenye mwili huvumilia, lakini hasa ni kwamba Roho wa Mungu hupitia udhalilishaji uliokithiri—Yeye hujinyenyekeza na kujificha Mwenyewe sana kiasi kwamba Yeye huwa mtu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua mfano wa mwili ili watu waone kwamba Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kwamba Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu hufanyika katika mwili. Roho Wake ni wa juu sana na mkuu, lakini Yeye huchukua mfano wa mwanadamu wa kawaida, wa mwanadamu asiye muhimu ili kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, umaizi, hisi, ubinadamu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kwamba hamfai kweli kupokea kazi ya Mungu ya aina hii. Hakika hamfai kumruhusu Mungu kuvumilia shida kama hiyo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni duni sana na wa hali ya chini, lakini Yeye bado huwafanyia kazi. Yeye hakupata mwili tu ili kuwaruzuku watu, kuzungumza na watu, Yeye hata huishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, wa hupendeka sana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

279. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni cha vitendo, na hakuna Anachofanya ambacho ni kitupu. Mungu huja kati ya wanadamu, Akijinyenyekeza kuwa mtu wa kawaida. Haondoki baada ya kufanya tu kazi kidogo na kunena maneno machache; badala yake, kwa kweli Yeye huja kati ya wanadamu ili kupitia mateso ya ulimwengu. Analipa gharama ya uzoefu Wake mwenyewe wa kuteseka ili kulipia hatima ya wanadamu. Je, si hii ni kazi ya vitendo? Wazazi wanaweza kulipa gharama ya dhati kwa ajili ya watoto wao, na hii inawakilisha uaminifu wao. Kwa kufanya hivi, Mungu mwenye mwili bila shaka anakuwa mnyoofu na mwaminifu kabisa kwa wanadamu. Kiini cha Mungu ni uaminifu; Yeye hufanya Anachosema, na chochote Afanyacho hutimizwa. Kila kitu Anachowafanyia wanadamu ni cha kweli. Yeye haneni tu maneno; Anaposema kuwa atalipa gharama, Yeye kwa kweli hulipa gharama. Anaposema kwamba Atapitia mateso ya wanadamu na kuteseka badala yao, kwa kweli Yeye huja kuishi kati yao, Akihisi na kupitia mateso haya Yeye binafsi. Baada ya hapo, vitu vyote ulimwenguni vitakiri kuwa kila kitu ambacho Mungu hufanya ni sahihi na chenye haki, kwamba vyote ambavyo Mungu hufanya ni halisi: Hiki ni kipande cha ushahidi chenye nguvu. Wanadamu watakuwa na hatima nzuri katika siku zijazo, na wale wote watakaobaki watamsifu Mungu; watasifu sana kwamba matendo ya Mungu kweli yalifanywa kutokana na upendo Wake kwa wanadamu. Mungu anakuja miongoni mwa wanadamu kwa unyenyekevu, kama mtu wa kawaida. Hafanyi tu kazi fulani, kunena maneno fulani na kisha kuondoka; badala yake, Anakuja kweli miongoni mwa wanadamu na kushuhudia uchungu wa duniani. Ni baada tu ya Yeye kupitia uchungu huu ndipo Ataondoka. Hivi ndivyo Mungu alivyo wa kweli na wa vitendo; wote watakaosalia watamsifu kwa ajili ya jambo hilo, na watauona uaminifu wa Mungu na wema Wake kwa mwanadamu. Asili ya Mungu ya uzuri na wema inaweza kuonekana katika umuhimu wa kupata mwili Kwake. Lolote Afanyalo ni la kweli; lolote Asemalo ni la dhati na halisi. Vitu vyote Anavyokusudia kuvifanya hufanywa kwa vitendo, na Yeye huvilipia gharama halisi; Yeye haneni tu maneno. Kwa hiyo, Mungu ni Mungu mwenye haki; Mungu ni Mungu mwaminifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kipengele cha Pili cha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

280. Mungu anazingatia tukio hili la usimamizi Wake wa binadamu, la wokovu Wake wa binadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi binadamu ni wanyonge jinsi gani, au binadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake za bidii za kazi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha na kuachilia kwa wanadamu bila kuficha juhudi Zake nyingi, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anaachilia na kuonyesha haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

281. Unapoweza kutambua kwa kweli fikira na mtazamo wa Mungu kwa wanadamu, wakati unapoweza kuelewa kwa kweli hisia na kujali kwa Mungu kwa kila kiumbe, utaweza kuelewa kule kujitolea na upendo unaotumika kwa kila mmoja wa watu walioumbwa na Muumba. Haya yanapofanyika, utatumia maneno mawili kufafanua upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Baadhi ya watu husema “mwenye kujitolea” na baadhi ya watu wakasema “kuwa na huruma nyingi ya kutoa msaada.” Kati ya kauli hizi mbili, “kuwa na huruma nyingi ya kutoa msaada” ndiyo kauli ambayo inafaa kwa kiasi kidogo zaidi kuufafanua upendo wa Mungu. Hii ni kauli ambayo watu hutumia kufafanua fikira na hisia za mtu kwa upana wa akili zake. Naichukia kweli kauli hii kwa sababu inarejelea ule utoaji wa msaada bila mpango na bila ubaguzi, bila kujali kanuni zozote. Ni maelezo ya kihisia za ziada za watu wajinga na waliochanganyikiwa. Wakati neno hili linatumika kufafanua upendo wa Mungu, bila shaka kuna nia ya kumaanisha kukufuru. Nina maneno mawili ambayo yanafafanua kwa usahihi zaidi upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Neno la kwanza ni “kubwa.” Je, si neno hili huamsha na kuleta hisia? Neno la pili ni “pana.” Kunayo maana halisi katika maneno haya mawili mbili Ninazotumia katika kufafanua upendo wa Mungu. Kama yatachukuliwa kwa njia ya moja kwa moja, “kubwa” linafafanua ukubwa au wingi wa kitu, lakini haijalishi kitu hicho kina ukubwa gani—ni kitu ambacho watu wanaweza kugusa na kuona. Hii ni kwa sababu kipo, si kifaa cha kidhahania na kinapatia watu hisia kwamba kwa kiasi fulani kina usahihi na hali ya kimatendo. Haijalishi kama unakiangalia kutoka katika mtazamo bapa au wa pande zote tatu; huhitajiki kufikiria uwepo wake, kwa sababu ni kitu ambacho kwa kweli kipo. Hata ingawa kwa kutumia “kubwa sana” kufafanua upendo wa Mungu kunaweza kuhisiwa kana kwamba tunataka kupima wingi wa upendo Wake, lakini hata hivyo linatoa hisia kwamba hauwezi kupimwa. Nasema kwamba upendo wa Mungu unaweza kupimwa kwa sababu upendo Wake si aina fulani ya kitu kisichojulikana, wala hauchipuki tu kutoka kwa ngano yoyote. Badala yake, ni kitu cha kutumiwa kwa pamoja na vitu vyote katika utawala wa Mungu, na ni kitu cha kufurahiwa na viumbe vyote hadi kwa viwango tofauti na kutoka katika mitazamo tofauti. Ingawa watu hawawezi kukiona au kukigusa, upendo huu huleta maendelezo na maisha katika vitu vyote kwani kinafichuliwa hatua kwa hatua katika maisha yao, na wanahesabu na kushuhudia upendo wa Mungu wanaofurahia kila wakati. Nasema kwamba upendo wa Mungu hauwezi kuhesabiwa kwa sababu fumbo la Mungu la Yeye kukidhi na kuimarisha vitu vyote ni kitu ambacho ni kigumu kwa wanadamu kuelewa, kama vile tu zilivyo fikira za Mungu katika vitu vyote na hasa vile vya mwanadamu. Hivyo ni kusema hakuna anayejua damu na machozi ambayo Muumba ametoa kwa sababu ya wanadamu. Hakuna anayeweza kufahamu, hakuna anayeweza kuelewa kina au uzito wa upendo ambao Muumba anao kwa ajili ya wanadamu, aliowaumba kwa mikono Yake binafsi. Kufafanua upendo wa Mungu kama mkubwa sana ni kuwasaidia watu kutambua na kuelewa upana wake na ukweli wa uwepo wake. Iko hivyo ili watu waweze kufahamu kwa kina zaidi maana halisi ya neno “Muumba,” na ili watu waweze kupata ufahamu wa kina zaidi wa maana ya “uumbaji.” Neno “pana” kwa kawaida huwa linafafanua nini? Linatumika kwa ujumla kumaanisha bahari au ulimwengu kama vile ulimwengu mpana au bahari pana. Ule mtanuko na kina kitulivu cha ulimwengu unazidi ufahamu wa binadamu na ni kitu ambacho kinanata fikra za binadamu, ambacho kwacho wamejawa na upendezwaji. Fumbo lake na umuhimu wake vyote vimo katika uwezo wa kuonekana lakini haviwezi kufikika. Unapofikiria kuhusu bahari, unafikiria kuhusu upana wake—yaonekana isiyo na mipaka, na unaweza kuhisi ile hali ya bahari hiyo kuwa fumbo na ujumuishwaji wake pia. Ndiyo maana Nimetumia neno “pana” kufafanua upendo wa Mungu. Ni kuwasaidia watu wahisi namna neno hilo lilivyo na thamani, na ili wahisi ule urembo wa kipekee wa upendo Wake, na kwamba nguvu za upendo wa Mungu haziishi na zimeenea. Ni kwa minajili ya kuwasaidia kuhisi utakatifu wa upendo Wake, na heshima pamoja na hali ya kutoweza kukosewa ya Mungu ambayo inafichuliwa kupitia upendo Wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

282. Kuna kitu katika kiini na tabia ya Mungu ambacho ndicho rahisi zaidi kupuuza, kitu ambacho kinamilikiwa tu na Mungu na wala si mtu yeyote, wakiwemo wale wengine wanafikiria kwamba ni watu wakubwa, watu wazuri, au Mungu wa kufikiria kwao. Kitu hiki ni nini? Ni kule kutokuwa na nafsi kwa Mungu. Tunapozungumzia kutokuwa na nafsi, unaweza kufikiria kwamba pia wewe huna nafsi, kwa sababu inapokuja kwa watoto wako, haujadiliani juu ya bei na wao na wewe ni mkarimu sana kwao, au unafikiria kwamba wewe huna nafsi sana inapokuja kwa wazazi wako. Haijalishi ni nini unafikiria, angaa unayo dhana ya neno “kutokuwa na nafsi” na unalifikiria kama neno zuri, na kwamba kuwa mtu asiye na nafsi ni jambo la kipekee. Wakati huna nafsi, unafikiri kuwa wewe ni mkubwa. Lakini hakuna mtu anayeweza kuona kutokuwa na nafsi kwa Mungu miongoni mwa viumbe wote, miongoni mwa watu, hafla, na vitu, na kupitia kazi ya Mungu. Kwa nini hali iko hivi? Kwa sababu binadamu ni mchoyo sana! Kwa nini Ninasema hivyo? Mwanadamu anaishi katika ulimwengu wa uyakinifu. Unaweza kumfuata Mungu, lakini huoni wala kushukuru namna ambavyo Mungu anakukimu, anavyokupenda na anavyoonyesha kwamba anakujali. Kwa hivyo unaona nini? Unaona watu wako wa ukoo wanaokupenda au kukupenda sana. Unayaona mambo ambayo ni ya manufaa kwa mwili wako, unajali kuhusu watu na vitu unavyopenda. Huku ndiko kutokuwa na nafsi kwa binadamu kunakodaiwa. Watu kama hao “wasiokuwa na nafsi” hata hivyo, huwa hawajali katu kuhusu Mungu anayewapa maisha. Kinyume na Mungu, kutokuwa na nafsi kwa binadamu kunakuwa cha nafsi na yenye uchoyo. Kutokuwa na nafsi ambako binadamu anasadiki katika ni ulio mtupu na usio halisi, uliotiwa madoa, usiolingana na Mungu, na usiohusika na Mungu. Kutokuwa na nafsi kwa binadamu ni kwa ajili yake, huku kutokuwa na nafsi kwa Mungu ni ufunuo wa kweli wa kiini Chake. Ndipo hasa kutokana na kujitolea nafsi kwa Mungu ndipo binadamu anapokea mfululizo usiosita wa ujazo kutoka kwake. Huenda msiathirike sana na mada hii Ninayozungumza kuhusu leo na unaweza kuwa tu unatikisa kichwa chako kwa kukubaliana nami, lakini wakati unapojaribu kufurahia moyo wa Mungu katika moyo wako, utaweza kwa kutojua kugundua: Miongoni mwa watu wote, masuala, na mambo unaweza kuhisi katika ulimwengu huu ni kutokuwa na nafsi tu kwa Mungu ambako ni kweli na dhabiti, kwa sababu ni upendo wa Mungu tu kwako ndio ambao hauna masharti na hauna madoa. Mbali na Mungu, kutokuwa na kile kinachodaiwa kutokuwa na nafsi wa mtu mwingine ni bandia, cha juujuu, kisicho na msingi; kina kusudio, nia fulani, kinatekeleza shughuli ya masikilizano, na hakiwezi kupimwa kamwe. Mnaweza hata kusema kwamba ni ki chafu, na cha kudharauliwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

283. Mungu alikuwa amemdharau binadamu kwa sababu binadamu alikuwa na uadui na Yeye, lakini ndani ya moyo Wake, utunzaji Wake, kujali Kwake, na huruma Yake kwa binadamu vilibakia vilevile. Hata wakati alipowaangamiza wanadamu, moyo Wake hukubadilika. Wakati binadamu walikuwa wamejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake, na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza binadamu hao. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi. Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwaangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu. Hivyo ni nini ambacho Mungu alifanya kwenye kipindi hiki kabla ya kuangamiza wanadamu? Mungu alifanya kiwango kikubwa cha kazi ya kukumbusha na kazi ya kusihi. Haijalishi ni maumivu kiasi kipi na huzuni ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Mungu, Aliendelea kufanyisha zoezi utunzaji Wake, wasiwasi, na huruma nyingi juu ya binadamu. Tunaona nini kutoka kwa haya? Bila shaka, tunaona kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kweli na si tu jambo ambalo Analizungumzia tu bila matendo. Ni jambo hakika, linaloweza kushikika na kutambulika, si bandia, halijatiwa najisi, halidanganyi wala halisingizii. Mungu kamwe hatumii uongo au kuunda taswira za bandia ili kufanya watu kuona kwamba Yeye anapendeka. Kamwe hatumii ushuhuda wa uongo ili kuwafanya kuona uzuri Wake, au kuringia uzuri wake na utakatifu Wake. Je, dhana hizi za tabia ya Mungu zinastahili upendo wa binadamu? Kwani nazo hazistahili kuabudiwa? Kwani nazo hazistahili kupendwa sana? Kwa sasa, Ningependa kuwauliza: Baada ya kuyasikia maneno haya, mnafikiri kwamba ukubwa wa Mungu ni maneno matupu tu kwenye kipande cha karatasi? Je, uzuri wake Mungu ni maneno matupu tu? La! Bila shaka la! Mamlaka ya juu, ukubwa, utakatifu, uvumilivu, upendo, wa Mungu na kadhalika—kila utondoti wa kila mojawapo ya vipengele vya tabia ya Mungu na kiini Chake unapata maonyesho ya vitendo kila wakati Anapoanza kazi Yake, zikiwa katika mapenzi Yake kwa binadamu, na pia zikitimizwa na kuonyeshwa kwa kila mtu. Licha ya kama umewahi kuzihisi awali, Mungu anamtunza kila mtu katika kila njia inayowezekana, kwa kutumia moyo Wake wa dhati, hekima, na mbinu mbalimbali ili kupashana mioyo ya kila mtu, na kuzindua roho ya kila mmoja. Huu ni ukweli usiopingika.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Tanbihi:

1.“Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

a. Maandishi asilia yanasema “ni ishara ya kutoweza.”

b. Maandishi asilia yanasema “na vilevile ishara ya kutoweza kukosewa kuwa (na kutovumilia kukosewa).”

Iliyotangulia: VI. Maneno Juu ya Biblia

Inayofuata: VIII. Maneno Juu ya Kuijua Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp