938 Tabia Ya Mungu Ni Ya Juu na Tukufu

1 Raha ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa wanadamu; raha Yake ni raha ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi, ishara ya fadhili.

2 Hasira ya Mungu inatokana na uharibifu ambao kuwepo na kuingilia kwa dhuluma kunaleta kwa wanadamu Wake, kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na chema. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake.

3 Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule mwanadamu mzuri lakini mwenye upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu.

4 Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu hupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kutoka wakati huu kuendelea, na ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wa mwangaza.

5 Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote huibuka kwa ajili ya masilahi yake mwenyewe, na wala si kwa ajili ya haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, sembuse neema inayotolewa na Mbinguni. Hisia za wanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa hapohapo.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 937 Maisha ya Mwanadamu Hayawezi Kuwa Bila Ukuu wa Mungu

Inayofuata: 939 Ishara ya Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp