968 Tabia ya Mungu ni Takatifu na Bila Dosari

1 Mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo ya gunia pamoja na jivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa angali na ghadhabu na wao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ikabadilika kwa utaratibu kuwa huruma na uvumilivu kwao.

2 Mungu huonyesha hasira kali kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina kosa. Moyo wa Mungu unavutiwa na toba ya watu, na ni toba hii ambayo hubadilisha moyo Wake. Kuguswa kwake, mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote havina kosa kabisa; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu ni uvumilivu mtupu; Huruma Yake ni huruma tupu.

3 Tabia Yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; kiini Chake ni tofauti na chochote kile katika uumbaji. Kanuni za matendo ambazo Mungu huonyesha, fikira na mawazo Yake, au uamuzi wowote maalum, pamoja na kitendo chochote kimoja, vyote havina dosari wala doa.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 967 Kiini cha Mungu ni kitakatifu

Inayofuata: 969 Asili ya Mungu Haina Ubinafsi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp