956 Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu

1 Wakati watu wanapotekeleza vitendo viovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itakoma. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa ukaidi, hasira Yake kali haitakoma; hasira Yake itawalemea hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hiki ndicho kiini cha tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na wema, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinaamrisha kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu.

2 Kama Mungu anaendelea kumfanya mtu apitie hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Kwa sababu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu hupokea utunzaji wa Mungu mara nyingi na hupokea huruma na uvumilivu Wake mara nyingi, basi mtu huyo bila shaka anaamini Mungu kwa kweli ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Yeye kwa mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 955 Malengo na Kanuni za Matendo ya Mungu ni Wazi

Inayofuata: 957 Mungu Atumai Mwanadamu Atubu kwa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp