863 Mungu Mwenye Mwili Ameishi Muda Mrefu Kati ya Wanadamu

1 Wakati Mungu alikuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa muda mrefu, baada ya kupitia na kushuhudia hali ya maisha mbalimbali ya watu, kile Alichofikiria kilikuwa si namna ya kuwa na maisha mazuri au namna ambavyo Angeishi kwa uhuru zaidi au kwa utulivu zaidi. Yeye binafsi aliweza pia kushuhudia namna ambavyo watu waliokuwa wakiishi ndani ya upotovu walivyokuwa wasioweza kujisaidia, na Akawaona kupitia ile hali duni ya wale walioishi katika dhambi, wale waliopotea katika mateso ya Shetani, ya mwovu. Binadamu Aliyaona haya na kila kitu Alichokiona kilimfanya kuhisi umuhimu na haja ya kazi Aliyokuwa Ameamua kuifanya wakati huu akiwa mwili.

2 Wakati wa mchakato huu, unaweza kusema kwamba Bwana Yesu alianza kuelewa waziwazi kazi Aliyohitajika kufanya na kile Alichokuwa Ameaminiwa kutekeleza. Alikuwa pia mwenye hamu kubwa zaidi ya kukamilisha kazi ambayo Alikuwa Aichukue—kushughulikia dhambi zote za mwanadamu, upatanisho wa Mungu na binadamu ili wasiishi tena katika dhambi naye Mungu Angeweza kusahau dhambi za binadamu kwa sababu ya sadaka ya dhambi, na hivyo basi kumruhusu kuendeleza kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu. Yaweza kusemwa kwamba katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya mwanadamu, kujitoa Mwenyewe. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja.

3 Alipokuwa na hisia hii ya dharura, Alikuwa hafikirii namna ambavyo maumivu Yake binafsi yangekuwa wala hakufikiria kwa muda wowote zaidi kuhusu ni kiwango kipi cha udhalilishaji ambacho Angevumilia—Alishikilia azimio moja tu moyoni Mwake: Mradi tu Alijitoa Mwenyewe, mradi tu Angesulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi, mapenzi ya Mungu yangetendeka na Angeweza kuanza kazi mpya. Maisha ya wanadamu katika dhambi, hali yao ya kuwepo katika dhambi ingebadilika kabisa. Imani yake na kile Alichoamua kufanya vyote vilihusiana na kumwokoa binadamu, na Alikuwa na lengo moja tu: kufanya mapenzi ya Mungu ili Aweze kuanza kwa ufanisi hatua ambayo ingefuata katika kazi Yake. Haya ndiyo yaliyokuwa katika akili ya Bwana Yesu wakati huo.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 862 Mungu Mwenye Mwili Anapendeza Sana

Inayofuata: 864 Ni Maumivu Magani Makubwa Apitiayo Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp