293 Mungu Anatarajia Kuwa Binadamu Wataweza Kuendelea Kuishi

1 Mungu alikuwa amemdharau binadamu kwa sababu binadamu alikuwa na uadui na Yeye, lakini ndani ya moyo Wake, utunzaji Wake, kujali Kwake, na huruma Yake kwa binadamu vilibakia vilevile. Hata wakati alipowaangamiza wanadamu, moyo Wake hukubadilika. Wakati binadamu walikuwa wamejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake, na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza binadamu hao. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi.

2 Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwaangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 292 Watu Hawajui Wokovu wa Mungu

Inayofuata: 294 Huruma ya Mungu Imemruhusu Mwanadamu Kusalia Hadi Leo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp