882 Mungu ametoa upendo Wake wote kwa watu

1 Bila kujali kama Yeye ni mwenye haki au Mwenye utukufu, au Yeye Huonyesha hasira kali, Yeye huokoa watu na hutekeleza mpango Wake wa usimamizi wote kwa sababu ya upendo. Kwa nini Yeye anachukua mwili? Imesemekana awali kuwa Mungu hakusita kulipa gharama yote ili kumwokoa binadamu. Kupata mwili ni pamoja na upendo kamili, na hii inawaruhusu nyinyi kuona kuwa binadamu huasi dhidi ya Mungu mno, washafika katika hali ambayo hawawezi kuokolewa; kwa hivyo, Mungu hakuwa na njia nyingine ila kuchukua mwili na kujitoa Mwenyewe kwa binadamu. Mungu ametoa upendo Wake wote.

2 Kama Asingempenda binadamu, kwa hakika Asingechukua mwili. Mungu anaweza kungurumisha radi na moja kwa moja kuonyesha utukufu Wake na ghadhabu na binadamu angeanguka juu ya ardhi; hakungekuwa na haja ya Yeye kuchukua mwili na kutarajia juhudi kubwa sana na kulipa gharama kubwa kama hiyo na kupata fedheha kubwa namna ile. Huu ni mfano ulio wazi. Ni afadhali Yeye Mwenyewe ateseka, kufedheheshwa, kutelekezwa, na kudhulumiwa ili kuokoa binadamu. Yeye bado Angeona afadhali akuje kwa mazingira ya aina hii ili kumwokoa binadamu. Je, huu sio upendo?

Umetoholewa kutoka katika “Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 881 Mungu Apitia Maumivu Makubwa Kumwokoa Mwanadamu

Inayofuata: 883 Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Alipata Mwili Ndipo Mwanadamu Akawa na Nafasi ya Wokovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp