872 Mungu Huvumilia Aibu Kubwa
1 Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Na kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeurudia mwili kwa mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana!
2 Hamjui kwamba Yeye hupitia aibu kubwa sana kwa ajili yenu wote na kwa ajili ya kudura yenu? Afadhali Azaliwe katika nchi yenye uchafu na kuteseka aibu yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote. Mungu ni halisi sana—Hafanyi kazi ya uwongo. Je, si kila hatua ya kazi Yake imefanyika kwa utendaji hivi? Ingawa watu wote wanamkashifu na kusema kuwa Anakaa mezani pamoja na wenye dhambi, ingawa watu wote wanamdhihaki na kusema kuwa Anaishi na wana wa uchafu, na watu wa hali ya chini sana, bado Anajitolea bila ubinafsi, na bado Anakataliwa kwa njia hii kati ya wanadamu. Je, si mateso Anayoyahimili ni makubwa zaidi kuliko yenu? Je, si kazi Yake ni zaidi ya gharama ambayo mmelipa?
Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu” katika Neno Laonekana katika Mwili