1013 Mungu Hawaokoi Waovu

1 Katika taifa la joka kubwa jekundu, Nimetekeleza hatua ya kazi isiyoeleweka kwa wanadamu, kuwafanya kuyumba katika upepo, ambapo baadaye wengi wanabebwa kwa siri na upepo unaovuma. Kweli, huu ni “uwanja wa kupura” Ninaotaka kuusafisha; ni kile Ninachotamani na pia ni mpango Wangu. Kwa maana wengi waovu wameingia ndani kimya wakati Niko kazini, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakuwa chemchemi ya uzima, kuwakubalia wanaonipenda kweli wapokee kutoka Kwangu tunda la mtini na harufu ya yungiyungi.

2 Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi iliyobaki, ila ni mchanga tu, na kwa hiyo, Nikikabiliwa na hali hizi, Nafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni dhahabu safi, iliyosafishwa, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea ndani ya paradiso Yangu? Natumia kila mbinu inayoweza kufikiriwa kuvifukuza vitu hivi. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Nikichukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wanalazimika kuondoka machoni Pangu. Hili ndilo Mimi huwafanyia waovu.

Umetoholewa kutoka katika “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1012 Wanaoamini na Wasioamini Hawalingani Kabisa

Inayofuata: 1014 Uzuri wa Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp