1. Ni kwa Nini Mungu Hufanya Kazi ya Kumuokoa Mwanadamu?

Maneno Husika ya Mungu:

Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake. Iwapo Mungu hatamshinda Shetani na kuokoa binadamu, ambao wamepotoshwa, Mungu hatawahi tena kuweza kuingia rahani. Mungu anakosa pumziko akosavyo mwanadamu. Wakati Mungu ataingia rahani tena, mwanadamu pia ataingia rahani. Maisha ya pumziko ni yale bila vita, bila uchafu, bila udhalimu unaoendelea. Hii ni kusema kwamba hayana unyanyasaji wa Shetani (hapa “Shetani” inamaanisha nguvu za uhasama), upotovu wa Shetani, na pia uvamizi wa nguvu yoyote inayompinga Mungu. Kila kitu kinafuata aina yake na kuabudu Bwana wa uumbaji. Mbingu na dunia ni shwari kabisa. Haya ni maisha matulivu ya binadamu. Mungu aingiapo rahani, hakuna udhalimu wowote utakaoendelea duniani, na hakutakuwa na uvamizi wowote wa nguvu za uhasama. Binadamu pia wataingia ulimwengu mpya; hawatakuwa tena binadamu waliopotoshwa na Shetani, lakini badala yake binadamu ambao wameokolewa baada ya kupotoshwa na Shetani. Siku ya pumziko ya binadamu pia ni siku ya pumziko ya Mungu. Mungu alipoteza pumziko Lake kwa sababu wanadamu hawakuweza kuingia rahani; haikuwa kwamba Hakuweza awali kupumzika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Huu ndio ukweli: Wakati dunia haikuwepo bado, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, yeye ndiye aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba binadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya Mungu duniani. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka kuwasimamia binadamu na kuzidi mamlaka ya Mungu. Ni malaika mkuu ambaye alimjaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuanzisha ufalme wake duniani na kuwafanya binadamu wamsaliti Mungu na kumtii yeye badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu wa dunia walivyomtii. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na vitu vyote vilivyo duniani vilikuwa chini ya utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu mbalimbali. Je, maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo hayajasababishwa na upotovu wa malaika mkuu? Binadamu wako tu namna walivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuwapotosha binadamu. … Binadamu na vitu vyote vilivyomo duniani sasa hivi vinamilikiwa na Shetani na katika umiliki wa waovu. Mungu anataka kuvifichua vitendo Vyake kwa vitu vyote ili watu waweze kumjua Yeye, na hivyo kuishia kumshinda Shetani na kuwaangamiza kabisa adui Zake. Uzima wa kazi hii unakamilishwa kupitia kufichua matendo Yake. Viumbe Vyake vyote vimemilikiwa na Shetani, na hivyo basi Angependa kuufichua uweza Wake kwa viumbe hivyo, na hivyo kumshinda Shetani. Kama Shetani asingekuwepo, Asingehitaji kuyafichua matendo Yake. Kama usingekuwa usumbufu wa Shetani, Angewaumba binadamu na kuwaongoza kuishi katika Bustani ya Edeni. Kwa nini Hakuwahi kufichua vitendo Vyake vyote kwa malaika au malaika mkuu kabla ya kusalitiwa na Shetani? Kama malaika na malaika mkuu wangalimjua Yeye, na pia kumtii Yeye pale mwanzoni, basi Asingetekeleza vile vitendo vya kazi visivyo na maana. Kwa sababu ya uwepo wa Shetani na mapepo, watu humpinga na wanajazwa hadi pomoni na tabia ya uasi, na hivyo basi Mungu angependa kufichua vitendo Vyake. Kwa sababu Angependa kupigana vita na Shetani, lazima Atumie mamlaka Yake kumshinda Shetani na kutumia vitendo Vyake vyote kumshinda Shetani; kwa njia hii, kazi Yake ya wokovu Anayotekeleza miongoni mwa binadamu itawafanya watu waone hekima na uweza Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake, ni matope na imejaa mashimo makubwa, ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Na katika pembe zenye baridi na giza magenge ya mapepo yameshika makazi. Na kila mahali katika dunia ya binadamu, mapepo yanakuja na kwenda katika magenge. Kizazi cha wanyama wa aina yote, waliojawa na uchafu, wanapigana mkono kwa mkono katika mapambano ya kikatili, sauti ambayo huleta hofu moyoni. Nyakati kama hizo, katika dunia kama hiyo, “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kupata hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa tangu mwazo mwigizaji akitenda kwa mfano wa Shetani—hata zaidi, kuwa na mwili wake, wakitumika kama shahidi wa kushuhudia kwa Shetani, kwa uwazi. Aina hii ya jamii ya binadamu, aina hii ya watu wachafu walioharibika tabia, na watoto wa aina hii wa familia hii ya binadamu potovu, inawezaje kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Mtu anaweza kuanza wapi kuongea juu ya shahidi Wangu? Kwa adui ambaye, baada ya kupotosha mwanadamu, anasimama dhidi Yangu, tayari amemchukua mwanadamu—mwanadamu ambaye niliumba kitambo sana na ambaye alikuwa amejawa na utukufu Wangu kuishi kulingana na Mimi—na kumchafua. Amepokonya utukufu Wangu, na yote ambayo imetia moyoni mwa mwanadamu ni sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alijaliwa na umbo na sura, mwenye kujawa na uhai, kujawa na nguvu ya maisha, na isitoshe, pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, naye alikuwa pia babu wa binadamu, na hivyo watu niliowaumba walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu. Adamu kiasili aliumbwa kutoka kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha mfano Wangu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilikuwa kiumbe kilichoumbwa na Mimi, kilichojawa na nishati Yangu ya uhai, kilichojawa utukufu Wangu, kinacho sura na umbo, kinacho roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee, aliyemilikiwa na roho, ambaye aliweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu, na kupokea pumzi Yangu. Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi ambaye uumbaji wake nilikuwa nimeamuru, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe ambaye angeendeleza utukufu Wangu, aliyejazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo aliyejawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana ya asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe hai, mwenye roho, mwili na mifupa, ushuhuda Wangu wa pili na pia mfano Wangu wa pili miongoni mwa mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina safi na ya thamani ya binadamu, na, kutoka awali, viumbe hai waliojaliwa na roho. Hata hivyo yule mwovu alikichukua kizazi cha mababu wa wanadamu na kukikanyaga na kukiteka nyara, kutosa ulimwengu wa binadamu katika giza totoro, na kuifanya kwamba kizazi chenyewe hakiamini tena katika uwepo Wangu. Kilicho cha chukizo zaidi ni kwamba, hata yule mwovu anapowapotosha watu na kuwakanyagia chini, anapokonya kwa ukatili utukufu Wangu, ushuhuda Wangu, nguvu Yangu Niliyowatolea watu, pumzi na maisha Niliyopuliza ndani yao, utukufu Wangu wote katika dunia ya binadamu, na damu yote ya roho ambayo nimetumia kwa mwanadamu. Mwanadamu hayupo tena katika mwanga, na amepoteza kila kitu Nilichompa, akiutupilia mbali utukufu ambao nimeutoa. Wanawezaje kukiri kwamba Mimi ndiye Bwana wa viumbe vyote? Wanawezaje kuendelea kuamini kuwepo Kwangu mbinguni? Wanawezaje kugundua udhihirisho wa utukufu Wangu duniani? Hawa wajukuu wa kiume na kike wanaweza kumchukua vipi Mungu ambaye mababu zao walimcha kama Bwana Aliyewaumba? Hawa wajukuu wenye kuhurumiwa “wamewasilisha” kwa ukarimu kwa yule mwovu utukufu, mfano, na vile vile ushahidi ambao Nilikuwa nimewatolea Adamu na Hawa, na pia maisha Niliyompa binadamu na ambayo ategemea ili kuwepo, na, bila kujali hata kidogo uwepo wa yule mwovu, amempa utukufu Wangu wote. Je, si hiki ni chanzo cha jina la “uchafu”? Jinsi gani aina hii ya mwanadamu, mapepo mabaya, aina hii ya maiti inayotembea, aina hii ya umbo la Shetani, na aina hii ya maadui Wangu zinaweza kumilikiwa na utukufu Wangu? Nitaumiliki tena utukufu Wangu, niumiliki ushuhuda Wangu ambao huwa miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyowahi kuwa mali Yangu na Nilivyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—nitamshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo, unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na dalili hata kidogo ya sumu yake. Na hivyo, Niliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kile kilichoumbwa na mkono Wangu, wale watakatifu ambao nawapenda na wasio wa mwingine yeyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu cha asili tena. Kwa sababu Ninanuia kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika kumshinda Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kusudi la starehe Yangu. Haya ndiyo mapenzi Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Iliyotangulia: Swali la 8: Unashuhudia kwamba Mungu kujipatia mwili Mwenyewe katika siku za mwisho kumeanza Enzi ya Ufalme, kuimaliza enzi nzee ya utawala wa Shetani. Tunachotaka kuuliza ni, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imemaliza vipi enzi ya giza ya imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini, na ya utawala wa Shetani? Tafadhali shiriki ushirika wenye maelezo.

Inayofuata: 2. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp