891 Mungu Huwajali Sana wale Ambao Atawaokoa

1 Je, haya hayaonyeshi kwamba katika enzi ya sasa, Mungu hawezi kusubiri kukamilisha mpango Wake na kuokoa watu Anaotaka kuokoa? Katika hali hizi, Mungu anajali kuhusu nini zaidi? Si vile wale wasiomfuata Yeye kabisa au wale wanaompinga Yeye kwa vyovyote vile wanamshughulikia Yeye au kumpinga Yeye, au namna ambavyo mwanadamu anamdanganya Yeye. Anajali tu kuhusu kama wale wanaomfuata Yeye, walengwa wa wokovu Wake katika mpango Wake wa usimamizi, wamewekwa kamili na Yeye, na kama wametimiza utoshelezi Wake. Kuhusiana na watu wale wengine bali na wale wanaomfuata Yeye, Anawatolea tu adhabu kidogo mara kwa mara ili kuonyesha ghadhabu Yake. Wakati huohuo, Anawalinda kwa dhati na kuwashughulikia wale wanaomfuata Yeye na karibu wanaokolewa na Yeye.

2 Tabia ya Mungu ni hii: Kwa mkono mmoja, Anaweza kuwapatia watu Anaonuia kutekeleza subira na ustahimilivu kamili wa kupindukia na kuwasubiria wao kwa muda mrefu Anavyoweza; kwa mkono mwingine, Mungu anachukia na kuchukizwa kwa dhati na watu wa aina ya Shetani wasiomfuata Yeye na wanaompinga Yeye. Ingawaje Hajali kama hawa watu wa aina ya Shetani wanamfuata au wanamwabudu Yeye, bado Anawachukia wao huku akiwa na subira na wao katika moyo Wake, na Anapoamua mwisho wa hawa watu wa aina ya Shetani, Yeye pia anasubiria kufika kwa hatua za mpango Wake wa usimamizi.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 890 Kiini cha Kristo ni Upendo

Inayofuata: 892 Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp