132 Yote Ambayo Kazi na Maneno ya Mungu Yamletea Mwanadamu ni Uzima

1 Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi; Anapofanya kazi na kuongea sio njia ya kutilia mipaka kama vile watu wanavyofikiria. Ndani ya Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa, na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye yuko hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake.

2 Kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake. Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona au kukadiria kazi Yake mpya, Ataitekeleza kazi Yake bila hofu. Hatakuwa na wasiwasi kuhusu dhana zozote za yeyote au kazi na maneno Yake kuelekezewa vidole, au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya. Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyote anayeweza kutumia akili ya binadamu, au kufikiria kwa binadamu, maarifa au maadili ya binadamu kupima au kufasili kile ambacho Mungu anafanya, kutia fedheha, au kutatiza au kukwamiza kazi Yake.

3 Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya; na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, tukio, au kitu, wala haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Kwa mjibu wa kazi Yake mpya kuhusika, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uzushi wote na hoja za uwongo za mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu. Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza, ni hakika itaendelezwa na ipanuliwe katika mwanadamu, na hakika itatekelezwa bila kuzuiliwa duniani kote mpaka pale ambapo kazi Yake kubwa imekamilika. Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake. Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake, lakini hakuna kuzuiliwa, kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 131 Mungu Aleta Kazi Mpya Katika Enzi Mpya

Inayofuata: 133 Mungu Hufanya Kazi Mpya katika Kila Enzi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp