6 Kristo wa Siku za Mwisho, Wokovu wa Mwanadamu

1

Mwanga wa umeme unaangaza kutoka Mashariki, ukiwaamsha wale wanaolala gizani.

Tunasikia maneno yaliyonenwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa,

kwa kweli ni sauti ya Mwana wa Adamu.

Watu wote wanaokaa gizani wanaona nuru ya kweli na wanasisimukwa, wanashangilia na kusifu kurudi kwa Mkombozi.

Wateule wa Mungu wanaisikia sauti ya Mungu, kufurahia maneno ya Mungu

na kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo.

Kristo wa siku za mwisho, wokovu wa wanadamu.

Kuja Kwako kunawaletea binadamu mwanga. Maneno Yako huangaza kama mwanga mkali,

wokovu Wako ni mkubwa na wa kweli sana.


Kristo wa siku za mwisho, wokovu wa wanadamu.


2

Hukumu Yako inatutakasa na kutuokoa, ili tuishi tena na kushuhudia matendo Yako.

Binadamu wamepotoshwa na Shetani kwa miaka elfu sita,

wakihangaika katika dhambi, wakikaribia kifo,

na hatimaye wameuona mwanga.

Haki inatokea ulimwenguni,

ukweli unatawala,

na wateule wa Mungu katika siku za mwisho wana bahati

ya kushuhudia kuonekana kwa Mungu.


Kristo wa siku za mwisho, wokovu wa wanadamu.


3

Katika ulimwengu wa giza, mfalme wa pepo anachukua mamlaka,

na binadamu wapotovu wanakanyagwa na kuumizwa vibaya sana na Shetani.

Mungu anaonyesha ukweli na kufichua ukweli

wa Shetani kuwapotosha wanadamu.

Baada ya kuelewa ukweli na kung’amua chanzo cha ulimwengu mwovu,

watu wa Mungu wanalichukia sana joka kubwa jekundu na kumfuata Mungu kikamilifu.

Tunatupilia mbali ushawishi wa giza wa Shetani,

na kupata wokovu mkuu wa Mungu.


Kristo wa siku za mwisho, wokovu wa wanadamu.


4

maneno Yako yana mamlaka makubwa

na yanashinda maadui wote.

Maneno Yako ni ukweli na uzima, yamekuwa msingi wa kusalia kwa binadamu.

Unawaleta binadamu katika nuru, na sasa binadamu wana hatima nzuri.

Kazi ya Mungu ya usimamizi ya miaka elfu sita imekamilika,

kupata mwili Kwake kunaleta ufalme wa Kristo.

Ufalme unakuja, Jua la haki linaonekana,

watu wa Mungu wanakusanyika kando ya kiti cha enzi na kumsifu Mungu kwa hamu!


Kristo wa siku za mwisho, wokovu wa wanadamu.

Kristo wa siku za mwisho, wokovu wa wanadamu.

Iliyotangulia: 5 Mwenyezi Mungu Ameonekana Mashariki ya Dunia

Inayofuata: 7 Ufalme Mtakatifu Umeonekana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

64 Upendo wa Kweli

1Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao,nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini.Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki