4 Mwenyezi Mungu, Kristo wa Siku za Mwisho

Kama umeme uwakavyo kutoka Mashariki hadi Magharibi,

ndivyo itakavyokuwa Mwana wa Adamu atakapokuja.

Na sasa Ameonekana Mashariki,

Yeye ndiye Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu.


Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli kamili

ili mwanadamu aokolewe na kutakaswa.

Neno laonekana katika mwili, latoa nuru.

na hii inaangazia enzi ya giza.


Hukumu inaanza na nyumba ya Mungu,

ni kazi inayoanza katika siku za mwisho.

Neno la Mungu laleta hukumu na kufunua

chanzo cha upotovu wa binadamu na uso wa kweli.


Maneno ya Mungu kama upanga yanachambua na kufichua

asili ya kishetani ambayo mwanadamu anamiliki.

Kuadibu na hukumu vyatakasa na kuokoa

wale wanaoinuliwa mbele ya kiti cha Mungu.


Vyote huzaliwa na kufanywa na maneno ya Mungu.

Mamlaka ya maneno ya Mungu ni makuu.

Kila neno la Mwenyezi Mungu

ndilo ukweli na litatimizwa.

Mwenyezi Mungu, Mfalme mshindi,

ameketi kwenye kiti cha utukufu.

Mataifa, watu wote wameshindwa na maneno ya Mungu,

wamekuja kumwabudu Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho,

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho.


Kwa haki, uadhama na ghadhabu,

kwa ulimwengu mwovu Mungu atoa hukumu.

Mungu sio huruma na upendo tu,

lakini Yeye ndiye uadhama na haki.


Maneno ya Mungu yatimiza yote katika siku za mwisho,

Anaonyesha hekima, uweza Wake.


Kwa kunena ukweli, Mungu anamshinda Shetani,

na binadamu wote wanaokolewa na kutakaswa.


Kristo wa siku za mwisho ananena sauti ya Mungu,

Neno limeonekana katika mwili.

Mungu ananena kwa binadamu wote,

hii ndiyo hukumu kuu ya kiti cheupe cha enzi.


Mwenyezi Mungu ndiye tumaini la pekee la mwanadamu,

Yeye huleta njia ya uzima wa milele.

Maneno Yake ni ukweli, uzima, njia,

na yanawaokoa binadamu wote.


Vyote huzaliwa na kufanywa na maneno ya Mungu.

Mamlaka ya maneno ya Mungu ni makuu.

Kila neno la Mwenyezi Mungu

ndilo ukweli na litatimizwa.

Mwenyezi Mungu, Mfalme mshindi,

ameketi kwenye kiti cha utukufu.

Mataifa, watu wote wameshindwa na maneno ya Mungu,

wamekuja kumwabudu Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho,

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho.


Mungu alipanga kabla kundi la watu wafanywe washindi.

Nguvu za uovu za joka kubwa jekundu 

zinashindwa, lakini bado zinapambana.

Maafa makuu yanaangamiza uovu wote,

hukumu ya siku za mwisho imefanyika.

Duniani ufalme wa Kristo umeonekana,

ufalme wa Kristo umeonekana.

Iliyotangulia: 3 Mwenyezi Mungu, wa Kwanza na wa Mwisho

Inayofuata: 5 Mwenyezi Mungu Ameonekana Mashariki ya Dunia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki