345 Kwa Nini Una Majivuno Sana?

1 Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayakutoshelezi wewe kuelewa hata sehemu ndogo kabisa ya mpango Wangu wa usimamizi. Hivyo kwa nini basi unakuwa mwenye kiburi sana? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika na Yesu hata katika sekunde moja ya kazi Yake! Je, una uzoefu kiasi gani hasa? Yale uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako yote na yale uliyoyafikiria ni kidogo kuliko kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko mchwa!

2 Vyote vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la mchwa! Usifikiri kwamba kwa kuwa tu umepata uzoefu na ukubwa kiasi, unaweza kuashiria kiburi na kuzungumza kwa maringo. Je, uzoefu wako na ukubwa wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba yalikuwa mbadala wa kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kuwa nimepata mwili, na kwa sababu ya hili pekee unajawa na dhana nyingi hizo, na kutoka kwalo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Isingekuwa kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta ulizo nazo ni za ajabu kiasi gani, usingekuwa na dhana hizi nyingi; si ni kutoka hapa ndipo fikira zako zinatoka hapa?

3 Kama si kupata mwili kwa Yesu mara hiyo ya kwanza, je, hata ungejua kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako kutoka kwa kupata mwili mara ya kwanza ndio una ufidhuli kuthubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini ukuchunguze badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Wakati umeingia katika mkondo huu na kuja mbele ya Mungu mwenye mwili, je, Angekuruhusu kuchunguza hili? Ni sawa kwako kuchunguza historia ya familia yako, lakini ukijaribu kuchunguza “historia ya familia” ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya uchunguzi kama huo? Je, wewe si kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?

Umetoholewa kutoka katika “Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 344 Yeyote Anayempima Mungu Kwa Fikira Anampinga Yeye

Inayofuata: 346 Hujui Kabisa Hadhi Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp