Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 168
12/10/2020
Yohana alizaliwa kwa ahadi, kama vile Isaka alivyozaliwa kwa Abrahamu. Alimwandalia Yesu njia na alifanya kazi nyingi, lakini hakuwa Mungu. Badala yake, anafikiriwa kuwa ni nabii kwa sababu alimwandalia tu Yesu njia. Kazi yake ilikuwa kuu pia, na ni baada ya yeye kuandaa njia tu ndipo Yesu akaanza kazi Yake kwa urasimu. Kimsingi, yeye alimfanyia tu Yesu kazi, na kazi yake ilikuwa katika huduma ya kazi ya Yesu. Baada ya yeye kuiandaa njia, Yesu akaanza kazi Yake, kazi iliyokuwa mpya zaidi, dhahiri zaidi, na katika utondoti mkubwa zaidi. Yohana alifanya tu kazi ya mwanzo; nyingi ya kazi mpya ilifanywa na Yesu. Yohana alifanya kazi mpya pia, lakini sio yeye aliyeianzisha enzi mpya. Yohana alizaliwa kwa ahadi, na jina lake kupewa na malaika. Katika wakati huo wengine walitaka kumpa jina la baba yake Zakaria, lakini mama yake alinena akisema, “Mtoto huyu hawezi kuitwa kwa jina hilo. Anapaswa kuitwa Yohana.” Haya yote yalielekezwa na Roho Mtakatifu. Jina la Yesu pia lilikuwa limeelekezwa na Roho Mtakatifu, na Alizaliwa wa Roho Mtakatifu, na kwa ahadi ya Roho Mtakatifu. Yesu Alikuwa Mungu, Kristo, na Mwana wa mtu. Kazi ya Yohana ilikuwa kuu pia, lakini mbona hakuitwa Mungu? Ni nini tofauti kati ya kazi iliyofanywa na Yesu na ile iliyofanywa na Yohana? Je, sababu pekee ni kwa kuwa Yohana ndiye aliyetengeneza njia ya Yesu? Au ni kwa sababu ilikuwa imepangwa na Mungu? Ingawa Yohana alisema kuwa, “Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu,” na kuhubiri pia injili ya ufalme wa mbinguni, kazi yake haikuwa yenye kina na ilijumuisha tu mwanzo. Kinyume, Yesu Alikaribisha enzi mpya na kuikamilisha enzi ya kitambo, lakini pia Alitimiza sheria ya Agano la Kale pia. Kazi Aliyofanya ni kubwa kuliko ile ya Yohana, na Alikuja kuwakomboa wanadamu wote—Alifanya hatua hii ya kazi. Yohana alitayarisha tu njia. Ingawa kazi yake ilikuwa kubwa, maneno yake mengi, na wale wafuasi waliomfuata wengi, kazi yake haikufanya kitu kingine ila kuletea mwanadamu mwanzo mpya. Mwanadamu hakupokea maisha, njia, ama ukweli wa ndani kutoka kwake, wala mwanadamu hakupata kupitia kwake ufahamu wa mapenzi ya Mungu. Yohana alikuwa nabii mkuu (Eliya) aliyeanza msingi mpya wa kazi ya Yesu na kutayarisha aliyeteuliwa; alikuwa mtangulizi wa Enzi ya Neema. Mambo kama haya hayawezi kutambuliwa kirahisi kwa kuchunguza kuonekana kwao kwa kawaida. Hasa sana, Yohana alifanya kazi kubwa; zaidi ya hayo, alizaliwa kutoka kwa ahadi ya Roho Mtakatifu, na kazi yake ikashikiliwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, kutofautisha kati ya utambulisho wao inaweza kufanywa tu kupitia kazi yao, kwa kuwa sura tu ya nje ya mwanadamu haiwezi kuonyesha dutu yake, na mwanadamu hawezi kuhakikisha ushuhuda wa kweli wa Roho Mtakatifu. Kazi iliyofanywa na Yohana na ile iliyofanywa na Yesu si sawa na ilikuwa ya asili tofauti. Hii ndiyo inafaa kuonyesha kama yeye ni Mungu ama sio Mungu. Kazi ya Yesu ilikuwa kuanza, kuendelea, kuhitimisha na kukamilisha. Kila moja ya hatua hizi zilichukuliwa na Yesu, ilhali kazi ya Yohana haikuwa zaidi ya kuanzisha. Hapo mwanzo, Yesu Alieneza injili na kuhubiri njia ya kutubu, na Akaendelea mpaka kumbatiza mwanadamu, kuponya magonjwa, na kukemea mapepo. Mwishowe, Alimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi na kukamilisha kazi Yake ya enzi yote. Alimhubiria mwanadamu na kueneza injili ya ufalme wa mbinguni katika sehemu zote. Hii ilikuwa sawa na Yohana, tofauti ikiwa kwamba Yesu Alikaribisha enzi mpya na kuleta Enzi ya Neema kwa mwanadamu. Kutoka kwa Mdomo Wake lilitoka neno jinsi mwanadamu anavyopaswa kutenda na njia mwanadamu anayopaswa kufuata Enzi ya Neema, na mwishowe, Akamaliza kazi ya Wokovu. Kazi kama hiyo haingeweza kutekelezwa na Yohana. Kwa hivyo, ni Yesu ndiye Aliyefanya Kazi Ya Mungu Mwenyewe, na ni Yeye ndiye Mungu Mwenyewe na Anamwakilisha Mungu moja kwa moja. Dhana za mwanadamu zinasema kwamba wale wote waliozaliwa kwa ahadi, waliozaliwa kwa Roho, waliothibitishwa na Roho Mtakatifu, na waliozifungua njia mpya ni Mungu. Kwa kadri ya fikira hii, Yohana pia angekuwa Mungu, na Musa, Abrahamu, na Daudi…, wao pia wangekuwa Mungu. Je, huu sio mzaha mkubwa?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video