Swahili Christian Testimony Video | "Toba ya Afisa"

14/05/2020

Mhusika mkuu katika Toba ya Afisa wakati mmoja alikuwa mwana wa mkulima wa kawaida. Baada ya kujiunga na jeshi, anaanza upesi kukubaliana na sheria za mila na desturi katika kitengo chake katika juhudi ya kupata hadhi, sifa na kupandishwa vyeo, akijipendekeza kwa wakuu wake na kuwafurahisha, akiwanunulia vyakula na kuwanunulia zawadi. Anapandishwa ngazi na kuwa kamanda wa batalioni na anaanza kutembea kwenye njia ya upotovu. Anajirekebisha na kuanza upya baada ya kupata imani katika Mungu na kuondoka jeshini, lakini anatambua kuwa bado amefungwa na falsafa na sheria za Shetani. Ili kuwa kiongozi wa kanisa, kwa mara nyingine anatumia njia za hila, lakini anaishia kufunuliwa na kushughulikiwa na ndugu. Anaachwa akiwa mwenye huzuni na maumivu kwa kushindwa kupata cheo kile. Kupitia hukumu na ufunuo wa maneno ya Mungu, anakuja kuelewa polepole kiini na matokeo ya kutafuta hadhi, na anaanza kufuatilia ukweli na kutembea kwenye njia sahihi maishani.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp