Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 166

03/10/2020

Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu. Haijalishi jinsi imani Yake ilivyokuwa kabla ya hii—labda wakati mwingine ilikuwa dhaifu, au wakati mwingine ilikuwa na nguvu—hayo ndiyo yalikuwa maisha Yake ya kawaida ya binadamu kabla Afanye huduma Yake. Baada ya kubatizwa (kuteuliwa), mara moja Alikuwa na nguvu na utukufu wa Mungu pamoja Naye, na hivyo Akaanza Kufanya huduma Yake. Angetenda ishara na maajabu, Atende miujiza, Alikuwa na nguvu na mamlaka, kwani Alifanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe; Alifanya kazi ya Roho badala Yake na kuonyesha sauti ya Roho Mtakatifu; kwa hivyo Alikuwa Mungu Mwenyewe. Hili halina pingamizi. Yohana alitumiwa na Roho Mtakatifu. Hangemwakilisha Mungu, na hakungekuwa na uwezekano wa yeye kumwakilisha Mungu. Kama angetaka kufanya hivyo, Roho Mtakatifu hangelikubali, kwani hangeweza kufanya kazi ambayo Mungu Mwenyewe alinuia kukamilisha. Labda kulikuwa na mengi ndani yake yaliyokuwa ya mapenzi ya mwanadamu, ama kitu kilichokuwa cha mwacha maadili; hakuna hali yoyote ambapo angemwakilisha Mungu moja kwa moja. Makosa Yake na mambo yasiyo sahihi yalimwakilisha yeye pekee, lakini kazi Yake ilikuwa uwakilishi wa Roho Mtakatifu. Ilhali, huwezi kusema kuwa yeye mzima alimwakilisha Mungu. Je upotovu na kuwa kwake na makosa kungemwakilisha Mungu pia? Kuwa na makosa katika kumwakilisha mwanadamu ni kawaida, lakini kama alikuwa na upotovu katika kumwakilisha Mungu, basi si hiyo ingekuwa kutomheshimu Mungu? Je hilo halingekuwa kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu? Roho Mtakatifu hawezi kumruhusu mwanadamu asimame mahali pa Mungu anavyotaka, hata kama anasifiwa na wengine. Kama yeye si Mungu, basi hataweza kubaki akiwa amesimama mwishowe. Roho Mtakatifu hamkubali mwanadamu amwakilishe Mungu vile mwanadamu atakavyo! Kwa mfano, Roho Mtakatifu alimshuhudia Yohana na pia kumtambulisha kuwa mmoja wa wale watakaomwandalia Yesu njia, lakini kazi iliyofanywa ndani Yake na Roho Mtakatifu ilikuwa imepimwa vizuri. Kilichotakiwa kwa Yohana ilikuwa awe wa kutayarisha njia ya Yesu tu, kumtayarishia Yesu njia. Hiyo ni kusema, Roho Mtakatifu Aliiunga mkono kazi yake katika kutengeneza njia na kumruhusu afanye kazi ya aina hiyo pekee, hakuna mwingine. Yohana alimwakilisha Eliya, na alimwakilisha nabii aliyetengeneza njia. Hili liliungwa mkono na Roho Mtakatifu; bora kazi yake iwe kutengeneza njia, Roho Mtakatifu aliiunga mkono. Hata hivyo, kama angeweka madai kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe na amekuja kumaliza kazi ya ukombozi, Roho Mtakatifu lazima amwadhibu. Haijalishi ukuu wa kazi ya Yohana, na ingawa iliungwa mkono na Roho Mtakatifu, kazi Yake ilibaki katika mipaka. Ni ukweli hakika kuwa kazi yake iliungwa mkono na Roho Mtakatifu, lakini nguvu aliyopewa katika wakati huo iliwekewa mipaka tu katika kutengeneza njia. Hangeweza, hata kidogo, kufanya kazi nyingine, kwani alikuwa tu Yohana aliyetengeneza njia, ila si Yesu. Kwa hivyo ushuhuda wa Roho Mtakatifu ni muhimu, lakini kazi ambayo mwanadamu anaruhusiwa kufanya na Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi. Je, Yohana hakushuhudiwa sana? Kazi yake haikuwa kuu pia? Lakini kazi aliyofanya haingeshinda ile ya Yesu, kwani alikuwa mwanadamu tu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu na hangeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja, na kwa hiyo kazi aliyofanya ilikuwa yenye mipaka. Baada ya yeye kuimaliza kazi ya kuandaa njia, Roho Mtakatifu hakuthibitisha ushuhuda wake tena, hakuna kazi mpya iliyomfuata yeye tena, na aliondoka kazi ya Mungu Mwenyewe ilipoanza.

Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, “Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu!” Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp