754 Mungu Atawapata tu Wale Wanaomshinda Shetani Kabisa

1 Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu.

2 Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani; wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alikuwa amemkabidhi kwa Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 753 Yote Anayofanya Mungu ni Kumwokoa Mwanadamu

Inayofuata: 755 Ni Wale tu Wanaomshinda Shetani Ndio Wanaookolewa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp