24 Anayeachilia Ngurumo Saba

1 Mwenyezi Mungu ni Mungu wa Roho saba! Yule wa macho saba na nyota saba ndiye Yeye pia; Yeye hufungua mihuri saba, na hati nzima ya kukunja imekunjuliwa na Yeye! Amepiga baragumu saba, na vitasa saba na mapigo saba yako mikononi Mwake, yatakayofunguliwa kwa mapenzi Yake. Ee, ngurumo saba ambazo daima zimefungwa! Wakati wa kuzifungua umewadia! Yule atakayezifungua ngurumo saba tayari ameshaonekana mbele ya macho yetu! Mwenyezi Mungu! Kila kitu kimekombolewa na kuwa huru na Wewe, hapana ugumu, na kila kitu kinakwenda vizuri! Hakuna kinachothubutu kukupinga au kukuzuia Wewe, vyote hukutii. Chochote kisichotii hufa!

2 Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye macho saba! Vyote viko wazi vikamilifu, vyote ni ng’avu na wazi, vyote vimefunuliwa na kuwekwa wazi. Vyote ni dhahiri kabisa na Yeye, na si tu kuwa Mungu Mwenyewe yuko hivi, lakini pia wana Wake wako hivi vilevile. Hapana yeyote, hakuna kitu chochote, na hakuna hoja yoyote inayoweza kufichwa mbele Yake na wana Wake! Nyota saba za Mwenyezi Mungu ni ng’avu bashashi! Kanisa limefanywa kuwa kamili na Yeye, Yeye huweka imara mitume wa kanisa Lake na kanisa lote liko ndani ya utoaji Wake. Yeye anafungua mihuri yote saba, na Yeye Mwenyewe analeta mpango wa usimamizi Wake na mapenzi Yake hadi tamati. Hati ndiyo kunga ya lugha ya kiroho ya usimamizi Wake na Amekifungua na kukifunua! Watu wote wanapaswa kusikiliza baragumu Zake saba zinazopigwa kwa sauti. Kwake, vyote vinajulishwa, kamwe visifichike tena, na hakuna huzuni tena. Vyote vinafunuliwa, na vyote vinashinda!

3 Baragumu saba za Mwenyezi Mungu ziko wazi, baragumu adhimu na zenye ushindi! Pia ni baragumu zinazowahukumu adui Zake! Katikati ya ushindi Wake, baragumu Yake inatukuzwa! Yeye hutawala ulimwengu mzima! Yeye amevitayarisha vitasa saba vya mapigo na vyote vinafunguliwa kwa nguvu kabisa kwa adui Zake kwa kiwango cha juu, na watateketea kwa miale ya moto Wake wenye ghadhabu. Mwenyezi Mungu huonyesha uwezo wa mamlaka Yake na adui Zake wote wanaangamia. Ngurumo saba za mwisho hazitafichwa tena mbele ya Mwenyezi Mungu, zote ziko wazi! Zote ziko wazi! Yeye huwaua adui Zake kwa ngurumo saba, Akiimarisha dunia, Akiifanya imtolee huduma, kamwe kutokuwa isiyofaa! Mwenyezi Mungu mwenye haki! Tunakutukuza milele! Unastahili sifa zisizoisha, kuhimidiwa kusikoisha na kutukuzwa!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 34” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 23 Mungu Atawala Katika Ufalme

Inayofuata: 25 Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp