1024 Ni Wale Tu Waliotakaswa Wataingia Rahani

1 Binadamu wa baadaye bado watakuwa na vizazi vya Adamu na Hawa, lakini hawatakuwa watu wanaomilikiwa na Shetani. Badala yake, watakuwa watu waliookolewa na kutakaswa. Hawa watakuwa binadamu ambao wamehukumiwa na kuadibiwa, na walio watakatifu. Hawa watu hawatakuwa sawa na jamii ya binadamu kama ilivyokuwa awali; mtu anaweza kusema kwamba hao ni watu wa aina tofauti kabisa na Adamu na Hawa wa awali.

2 Hawa watu watakuwa wamechaguliwa kutoka miongoni mwa wote waliopotoshwa na Shetani, na watakuwa ndio watu ambao hatimaye wamesimama imara wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, watakuwa kundi la mwisho la watu miongoni mwa wanadamu potovu. Kundi hili la watu ndilo tu litaweza kuingia katika raha ya mwisho pamoja na Mungu.

3 Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1023 Mahali Tofauti pa Mapumziko kwa Mungu na Mwanadamu

Inayofuata: 1025 Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu Katika Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp