Je, Kauli “Yule Amwaminiye Mwana Ana Uzima wa Milele” Inamaanisha Nini Hasa?

23/07/2020

Tamanio kubwa kabisa la kila mmoja wetu anayemwamini Bwana ni kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Biblia inasema, “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele: na yule asiyemwamini Mwana hatauona uzima; ila ghadhabu ya Mungu hukaa juu yake(Yohana 3:36). Watu wengi hufikiria kwamba kumwamini Mwana kunamaanisha kuamini katika Bwana Yesu Kristo, na kwamba njia ya Yesu ndiyo njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, mtu anaposhuhudia kwao kwamba ni Kristo wa siku za mwisho pekee Anayeweza kumpa mwanadamu uzima wa milele, hawawezi kukubali hilo. Wanafikiria wanaweza kupata uzima wa milele kwa kumwamini Bwana Yesu, hivyo kuna haja gani ya kukubali maneno na kazi ya Kristo wa siku za mwisho? Ili kuelewa suala hili, lazima kwanza tuelewe kauli “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele” inamaanisha nini hasa na jinsi tunaweza kweli kupata uzima wa milele. Mambo haya ni muhimu kwa kuwa yana athari ya moja kwa moja kwa majaliwa na hatima zetu, kwa hivyo acha tufanye ushirika na tuyachunguze sasa kwa pamoja.

Imani ya Kweli Katika Mwana ni Nini? Je, Tunaweza Kupata Uzima wa Milele kwa Kumwamini Bwana Yesu?

Sote tunajua ya kwamba kumwamini Mwana kunamaanisha kuamini katika Kristo mwenye mwili, na tunafikiria kwamba kumwamini Mwana kunamaanisha kumwamini Bwana Yesu. Lakini hii si sahihi kikamilifu, na hii siyo maana ya kweli ya imani katika Mwana. Biblia inatabiri wazi kwamba Bwana atakaporudi, Atarudi tena katika mwili kama Mwana wa Adamu: “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja(Luka 12:40). “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17: 24-25). “Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa(Mathayo 24:37). Maneno “Mwana wa Adamu anakuja” na “kuja kwa Mwana wa Adamu” hurejelea mtu aliyezaliwa kutoka kwa mwanadamu ambaye ana ubinadamu wa kawaida. Mwili wa kiroho wa Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hauwezi kuitwa Mwana wa Adamu, na kwa hivyo Bwana atakaporudi, Atapata mwili tena kama Mwana wa Adamu. Maneno yaliyonenwa na Bwana Yesu, “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele,” hayarejelei tu imani katika Bwana Yesu, lakini pia yanamaanisha imani katika Kristo mwenye mwili katika siku za mwisho. Hii tu ndiyo imani ya kweli katika Mwana.

Watu wengine hawaelewi hili, na wanaamini kwamba Bwana Yesu aliposema, “Ila yeyote akunywaye maji ambaye nitampa hatawahi kuwa na kiu; lakini maji hayo ambayo nitampa yatakuwa chemichemi ya maji ambayo yanachipuka katika uhai wa daima(Yohana 4: 14), hii ilionyesha ya kwamba Bwana Yesu alikuwa na njia ya uzima wa milele. Wanauliza: “Kwa nini hatuwezi kupata uzima wa milele kwa kuamini katika Bwana Yesu tu? Je, ni lazima tumwamini Mwana wa Adamu katika siku za mwisho? Je, inawezekana kwamba Bwana Yesu hana uwezo wa kutupa uzima wa milele?” Hatupaswi kusema mambo kama hayo, lakini badala yake lazima tuelewe suala hili vizuri kabisa: Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili; Alikuwa na utambulisho na kiini cha Mungu; Alikuwa ukweli, njia na uzima, na kiasili Alikuwa na njia ya uzima wa milele. Hivyo kwa nini tusiweze kupata uzima wa milele kwa kumwamini tu Bwana Yesu, lakini pia lazima tumwamini Kristo wa siku za mwisho kabla tuweze kupata njia ya uzima wa milele? Hili linahusiana moja kwa moja na kazi ya Mungu na matokeo ya kila hatua ya kazi ya Mungu. Kila mtu anajua kwamba mwishoni mwa Enzi ya Sheria, binadamu wote walikuwa katika hatari ya kuuawa kwa kukiuka sheria, na walihitaji toleo la dhambi la milele. Hiyo ndiyo sababu Bwana Yesu alifanyika mwili na Akaja duniani, na Alisulubiwa binafsi kwa ajili ya wanadamu, Akawa sadaka ya dhambi kwa ya mwanadamu. Baada ya hayo, watu walipaswa tu kutubu na kumwomba Mungu, na dhambi zao zilisamehewa. Hata hivyo, kile kisichoweza kukanwa ni kwamba bado tunaishi katika dhambi na tunashindwa kufuata mafundisho ya Bwana; hatuwezi kujizuia ila kutenda dhambi na kisha kukiri daima, tukiishi katika mzunguko mbaya wa dhambi. Dhambi zetu bado hazijatakaswa kabisa na kiini cha dhambi yetu hakijatatuliwa. Mpaka hilo lifanyike, bado hatustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele.

Kama neno la Mungu linavyosema, “Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Tumepotoshwa sana na Shetani na asili yetu ya kishetani imekita mizizi sana ndani yetu. Tunatawaliwa na tabia za kishetani kama vile ubinafsi, kiburi na udanganyifu. Tunaendelea kutenda dhambi na kukiri bila kukoma, tusiweze kujinasua kutoka kwa minyororo ya dhambi. Ili kuridhisha masilahi yetu ya kibinafsi katika hali mbali mbali, sisi daima husema uwongo na kuwadanganya wengine; tunapomfanyia Bwana kazi na kuhubiri, sisi huringa na kujionyesha, tukitumaini kwamba wengine watatustahi na kutuheshimu sana; kuhusu jinsi tunavyomtendea Mungu, sisi humshukuru Anapotubariki, lakini tunamwelewa visivyo na kumlaumu Mungu majaribu yanapotujia. Hii ni mifano michache tu. Na kwa hivyo ikiwa sisi, ambao hutenda dhambi mara nyingi, ambao humpinga Mungu na kumsaliti Mungu, tunakubali tu wokovu wa Bwana Yesu na kusamehewa dhambi zetu, lakini tabia zetu potovu hazijatakaswa, basi tunawezaje kupata uzima wa milele? Tunaweza kuona kutoka kwa matokeo yaliyopatikana kwa kazi ya Mungu kwamba kazi ambayo Bwana Yesu alifanya katika Enzi ya Neema iliwawezesha watu kusamehewa dhambi zao tu, na kuwafanya wasiwe na dhambi tena, lakini hawawezi kupata uzima wa milele kwa kumwamini Bwana Yesu tu. Bwana aliposema, “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele,” kwa kweli Alikuwa akishuhudia ukweli kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe akionekana katika mwili. Alikuwa akiyashuhudia mamlaka ya Mungu, kwamba ni Mungu pekee Anayeweza kumpa mwanadamu uzima wa milele. Hata hivyo, Bwana hakuwahi kusema kwamba Atampa mwanadamu njia ya uzima wa milele katika Enzi ya Neema, na kwamba kwa kukubali wokovu Wake, watu wataweza kupata uzima wa milele. Ikiwa tunataka kupata njia ya uzima wa milele na tabia zetu potovu zitakaswe kabisa, basi lazima tukubali maneno na kazi ya Mwana wa Adamu mwenye mwili katika siku za mwisho. Tukiamini tu katika Bwana Yesu na tusimkubali Mwana wa Adamu ambaye amerudi katika siku za mwisho, basi “imani yetu katika Mwana” ni imani nusu tu na haiwezi kuitwa imani ya kweli katika Mwana, sembuse sisi kuweza kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele.

Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Wengine sasa wanaweza kuuliza, “Kwa kuwa hatuwezi kupata uzima wa milele kwa kumwamini Bwana Yesu tu, na tunaweza tu kupata uzima wa milele kwa kumkubali Kristo wa siku za mwisho, basi Kristo wa siku za mwisho Anatupaje njia ya uzima wa milele?” Bwana Yesu alitabiri, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16: 12-13). “Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5: 27). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12: 47-48). Tunaweza kuona kutoka katika unabii wa Bwana Yesu kwamba Mungu atakapokuwa mwili katika siku za mwisho, Atanena maneno zaidi, Atafanya kazi ya kuhukumu na kumtakasa mwanadamu, kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kutuwezesha kupata uzima wa milele. Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi Yake, mwanadamu alikuwa mwenye kimo kidogo na hangeweza kustahimili kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu. Hiyo ndiyo maana Mungu huonyesha ukweli kutekeleza hatua hii ya kazi katika siku za mwisho, kwa maana kila wakati Mungu hufanya kazi kwa hatua kulingana na kimo cha mwanadamu. Sasa, Bwana Yesu ambaye tumemngojea kwa hamu sana Amerejea katika mwili—Yeye ni Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote ambao unaweza kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu; Yeye hutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu, Akituletea njia ya uzima wa milele. Hii inatimiza kabisa unabii wa Bwana Yesu.

Hebu tusome maneno ya Mungu: “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu.” Maneno ya Mungu yanaeleweka kabisa: Njia ya uzima wa milele inatoka kwa Kristo wa siku za mwisho, na ni kwa kukubali hukumu na utakaso wa Kristo wa siku za mwisho tu ndiyo tunaweza kupata uzima wa milele. Kwa kupitia hukumu ya Mungu ya siku za mwisho, mwenendo na shughuli zetu na wengine zinaweza kulingana na maneno ya Mungu, na tunaweza kuwa na uwezo wa kushughulikia mambo kwa maadili, ili tusitende dhambi tena au kumpinga Mungu, na tuweze kumtii Mungu. Yaani, ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ambao hututakasa na kutuokoa unakuwa maisha yetu halisi, na ni hapo tu ndipo tunaweza kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni na kuwa wale wanaopata uzima wa milele. Lakini sasa tumepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba, kulingana na mahitaji yetu, Mungu anaonyesha ukweli wote ambao unaweza kutuwezesha tuondokane kabisa na ushawishi wa Shetani na tupate wokovu kamili, na ni ukweli huu ndio njia ya uzima wa milele ambao Mungu anampa mwanadamu. Mungu huonyesha maneno ambayo yanafunua asili na kiini cha mwanadamu, maneno ambayo humfundisha mwanadamu jinsi ya kumtii na kumpenda Mungu, maneno ambayo hushuhudia kile Mungu anacho na alicho, na zaidi. Tunaposoma maneno ya Mungu na kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tunapata kuwa na ufahamu kiasi wa kweli wa asili yetu ya kishetani. Tunaweza kuona kwamba, ingawa tunaweza kuonyesha tabia nyingi nzuri za juu juu, ndani tumejawa na tabia potovu za kishetani, kama vile kiburi na majivuno, ambapo hatumsikilizi mtu yeyote, ambapo tunatamani kujitokeza katika umati, bila kujali ni nani tuliye pamoja naye, ambapo tunataka kila wakati kuwa wa kwanza, na kuwafanya wengine watustahi na kutuheshimu sana; tukiwa wasio wanyoofu na wadanganyifu kupindukia, wabinafsi na wenye kustahili dharau, wenye ulafi na waovu, ambapo tunajali tu masilahi yetu, ambapo tunafanya kazi na kujitumia kwa ajili ya Mungu ili tufanye majadiliano na Yeye ili tuweze kuingia katika ufalme wa mbinguni na tupate uzima wa milele. Vitu hivi siyo kwa ajili ya kumridhisha Mungu hata kidogo. Kazi ya Mungu inapopingana na mawazo yetu wenyewe, tunaweza hata kwenda kiasi cha kumkana Mungu, kumhukumu Mungu, na kumpinga Mungu. Wakati majanga ya asili au yasababishwayo na mwanadamu yanapotupata, tunapokumbana na majaribu na dhiki, tunamlaumu Mungu na kumsaliti Mungu. Ni katika nyakati kama hizi tu ndipo tunaweza kuona wazi sura mbaya ya kupotoshwa kwetu na Shetani. Kisha tunakubali kwamba asili yetu hakika ni ya Shetani, na tunaanza kujichukia na kujikirihi kutoka katika vina vya mioyo yetu. Tunatubu kwa Mungu, tunalenga kufuatilia na kutenda ukweli, tunaishi kwa kudhihirisha mfano kiasi wa binadamu, na tabia zetu potovu zinatakaswa na kubadilishwa polepole. Bila ukweli huu uonyeshwao na Kristo wa siku za mwisho, hakuwezi kuwa na toba au mabadiliko ya kweli ndani yetu. Kwa kuipitia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho na kutakaswa, tunaweza kisha kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu. Tukipitia hata hukumu na kuadibu kwa Mungu zaidi tabia zetu potovu zibadilishwe, basi tutaweza kumtii Mungu na kusikiza maneno Yake—kisha tunapatwa na Mungu, kama “watoto wadogo” wasio na lawama na walio waaminifu. Wale watakaswao kupitia hukumu, wale wasio na lawama na walio waaminifu, wataingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Hii ni ahadi ya Mungu, kama vile inavyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: “Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake(Ufunuo 22:14). Kinyume na hilo, tusipokubali hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho, basi haitawezekana dhambi zetu kutakaswa au sisi kuingia katika ufalme wa Mungu. Ni kama tu vile Bwana Yesu alisema: “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele: na yule asiyemwamini Mwana hatauona uzima; ila ghadhabu ya Mungu hukaa juu yake(Yohana 3:36).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp