Ni Upendo wa Mungu Tu Ulio Halisi

13/01/2018

Xiaodong Mkoa wa Sichuan

Mungu alisema, “Taifa la China, likiwa limepotoshwa kwa miaka mingi, limesalia hadi leo, kila aina ya ‘virusi’ vikizidi bila kikomo, vikienea kila mahali kama pigo; inatosha tu kuangalia mahusiano ya watu ili kuona jinsi ‘vijidudu’ vingi vimejificha ndani ya watu. Ni vigumu sana kwa Mungu kukuza kazi Yake katika eneo lililobanwa sana na kujawa virusi. Hulka za watu, tabia, jinsi wanavyofanya mambo, kila kitu wanachoonyesha katika maisha yao na mahusiano baina yao—yote yameharibika …(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia … (6)). Ufunuo katika maneno ya Mungu ulinifanya kuona jinsi upotovu wa Shetani huufanya uhusiano wote kati ya watu kutokuwa wa kawaida, kwa sababu wote uko kwa msingi wa falsafa ya Shetani ya maisha, bila kuwa hata na chembe ya ukweli. Bila wokovu wa Mungu, macho yangu yangekuwa bado yamefunikwa na ningekuwa bado nimenaswa na hisia, lakini kuwa na uzoefu wa kazi ya Mungu kumenifanya nielewe kiini cha ni nini maana ya “kusaidiana” na kukanionyesha ukweli wa urafiki, upendo, na upendo wa kifamilia. Niliona kwamba ni maneno ya Mungu tu yaliyo ukweli, na kwamba ni kwa kuishi kwa maneno ya Mungu tu tunapoweza kuepuka ushawishi wa Shetani, na kwamba ni kwa kujistahi mwenyewe tu kulingana na ukweli tu ndiyo mtu angeweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana.

Wazazi wangu wote wawili walikuwa Wakristo, na wakati huo imani yetu kwa Yesu ilituletea neema kubwa. Hasa katika biashara, Mungu alitubariki na maliwazo mengi ya kimwili. Wengi wa jamaa zangu hawakuwa na mali kama familia yetu, na wazazi wangu waliwatunza vizuri kifedha na kinyenzo. Jamaa zangu walikuwa na heshima kubwa sana kwa wazazi wangu, na kwa kawaida walinitazama kwa jinsi hiyo hiyo. Hiyo ndiyo iliyokuwa aina ya mazingira ya manufaa ambayo nilikulia. Nilifikiri marafiki na jamaa zangu walikuwa wa ajabu, na bila kujali familia yetu ilichohitaji, wao wangekuwa radhi kuwasaidia.

Katika mwaka wa 1998, familia yangu nzima ilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu, na kwa sababu ulikuwa uwanja mgumu, tulisimamisha biashara ya familia yetu. Wakati huo, sikuuelewa ukweli, hivyo moyo wangu bado ulitamani dunia hii. Nilishinda siku zangu nikila, kunywa, na kusherehekea na marafiki zangu wa karibu na jamaa, na kwa sababu nilitumia pesa kwa ukarimu, nilipata marafiki zaidi na zaidi, na kurudiana zaidi na zaidi na wanafunzi wenza, karamu, karamu za siku za kuzaliwa na harusi za wanafunzi wenza na marafiki, na sherehe zingine hazingefanywa bila kunialika, kwa sababu mimi nilikuwa “muhimu” mno. Zaidi ya hayo, kila Jumapili ilibidi nimchukue na kumuaga mpenzi wangu wa kike, na mara nyingi tulitembea pamoja. Wakati huo, hata kama sikuwahi kamwe kukosa hata mmoja ya mikutano yangu mitatu kwa wiki katika kanisa, bado sikuwa na ufahamu kabisa wa maneno ya Mungu, moyo wangu bado ulitangatanga katika dunia ya nje, na imani yangu katika Mungu ilikuwa kama utumwa wa sheria. Lakini Mungu alitumia mazingira kunifanya nielewe ukweli. Alionyesha kuwa uhusiano kati ya watu una msingi wake si katika chochote ila maslahi ya wote, na kwamba hakuna kitu kama hisia ya kweli au upendo ndani yao.

Baada ya biashara kusimama, wazazi wangu waliikarabati nyumba yetu na iliwabidi kulipia mafundisho ya dadangu na mimi, hivi kwamba akiba ya familia yetu ilikuwa karibu kuisha baada ya miaka michache. Kama tu msemo unavyoeleza “Vijito hukauka mto unapopunguka maji.” Kwa kuwa niliwategemea kwa mapato yangu, kulikuwa na upungufu katika matumizi yangu mwenyewe. Niliepuka harusi na mikutano, mikubwa au midogo, wakati ningeweza, hivi kwamba jamii yangu ya marafiki walianza kupungua, na hadhi yangu machoni pa marafiki zangu ikawa chini zaidi na zaidi. Hali ya kifedha ya marafiki maskini zaidi na jamaa zangu ilipostawishika, walipunguza uhusiano wao nasi pia. Kipindi hiki kilikuwa cha kusafisha kwangu, kwa sababu nilihisi sikuwa na hadhi katika mioyo ya wengine. Hasa mpenzi wangu wa kike, ambaye alianza kuwa baridi zaidi kwa sababu sikuwa nikitumia fedha kwa ukarimu kama nilivyofanya katika siku za nyuma, na hatimaye akaniacha kwa ajili ya mtu mwingine mwaka 2001. Nilipopata habari kuhusu hilo, singekubali kuwa ilikuwa kweli. Mimi sikulionyesha kwa nje, lakini ufahamu ulikuwa kama kisu katika moyo wangu. Nilikuwa mwaminifu kwa mpenzi wangu, juhudi zangu kwa ajili yake zilikuwa za kweli, hivyo ni kwa nini nilipata usaliti kutoka kwake kama malipo? Hiyo ndivyo uhusiano wetu wa miaka mitano ulivyofika kikomo. Sikujua jinsi ya kumsahau, hivyo nililoweza kufanya tu ni kuyazika maumivu ndani ya moyo wangu. Baada ya hapo, nilichukizwa wakati wengine walipotaja tukio hilo. Singeweza kuelewa jinsi kitu kama hiki kingeweza kunitokea. Kisha siku moja, nikaona kifungu hiki cha neno la Mungu, “Watu wengi wanaishi katika uovu wa Shetani, na kuumizwa na dhihaka zake; anawaudhi kwa njia hii hata hapo watakapokuwa wamelemewa kabisa, wakistahimili kila badiliko, kila ugumu katika ulimwengu wa kibinadamu. Baada ya kuwachezea, Shetani huimaliza hatima yao. Na hivyo watu wanapita katika maisha yao yote wakiwa na mkanganyiko, wala hawajawahi kufurahia hata siku moja vitu vizuri ambavyo Mungu amewaandalia, badala yake wanajeruhiwa na Shetani na kuachwa wakiwa wameharibika kabisa. Leo wamekuwa wadhoofu na walegevu sana kiasi kwamba hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (1)). Ufunuo katika maneno ya Mungu ni taswira halisi ya maisha ya binadamu. Nikitafakari nyuma jinsi nilivyoshinda siku zangu nikizama katika ugonjwa wa mahaba, na kuishi katika ulimwengu wa kufikirika wa “upendo wa kimapenzi.” Nilinaswa bila kuchangulika, na sikujua kabisa kwamba mambo haya yalikuwa ni hila za Shetani kuwadanganya watu, ujanja uliopangwa kuwanasa watu na kuwafanya kuishi bila malengo yoyote na bila mwelekeo wa kuangalia kwa makini kazi ya Mungu. Ingawa nilijiita muumini katika Mungu, nilishinda siku zangu nikihofia na kujitahidi juu ya urafiki na mapenzi, na kama hali yangu haikuwa imebadilika kwangu, bado ningeamini katika zile “ahadi za upendo wa milele” na “marafiki waaminifu,” na singeweza kamwe kuepuka hilo. Kwa sababu ya kuvunjika kwa uhusiano na mpenzi wangu, nilivunja uhusiano wangu wote na wanafunzi wenza; bila mazingira kama hayo yenye kelele ningetuliza moyo wangu na kujitolea mwenyewe kwa imani yangu katika Mungu. Katika mikutano, kupitia ushirika kuhusu maneno ya Mungu na ndugu zangu wa kiume na wa kike, nilikuja kuelewa ukweli fulani na kuweza kuelewa upendo na urafiki kwa kiasi, na kugundua kwamba ni kwa kufuatilia ukweli na kuuelewa ukweli tu ndio mitazamo ya mtu kuhusu mambo inaweza kubadilishwa, na hatawahi kudanganywa na Shetani. Polepole, moyo wangu uliojeruhiwa ukaanza kupona. Nilihisi furaha iliyosahaulika zamani, kutopotea tena au kuishi katika maumivu yangu. Kwa sababu hakukuwa na kuingiliwa kutoka dunia ya nje, niliweza kutuliza mawazo yangu na kulenga mikutano. Nikawa na upendo zaidi na zaidi kwa imani katika Mungu, na kutoka hapo kwendelea nikaanza kutimiza wajibu wangu.

Jamaa zangu walipopata habari kuwa nilimwamini Mungu, hakukuwa na mwisho kwa usumbufu wao. Wao walidhani kuwa sikustahili kumwamini Mungu katika umri mdogo kama huo. Shangazi yangu wa upande wa mama mara nyingi aliniomba fadhila, shangazi yangu wa upande wa baba aliniomba nifanye biashara naye, hata mama mlezi wangu alinihimiza nioe, akisema kuwa angemtunza mtoto wangu baada ya kuzaliwa kwake (kwa sababu hakuwa na mwana wake mwenyewe), na bibi yangu alipaza sauti, akisema, “mimi kabisa sina pingamizi kamwe kwa wazazi wako kuamini katika Mungu, kwa kuwa walifanya kazi nusu ya maisha yao na kutoa kila walicho nacho ili kuwaandalia njia, hivyo ni wakati wa kuwaacha wapumzike. Unapaswa kulenga kuanzisha familia na kazi.” Kisha akaendelea kueleza jinsi baba yangu alikua katika maisha ya umaskini, jinsi alivyoanza bila chochote, ni kiasi gani alichoteseka, jinsi alivyofanya kazi kwa bidii, na kusema kuwa mimi nilikuwa katika mazingira mazuri, na kwamba sikuwa na maadili. “Kujishughulisha” kwao kwa ghafla kwa ajili yangu kulikuwa kunarai sana. Nilikuwa nimechanganyikiwa, kwa sababu ilionekana kama alichokisema kila mmoja wao kilikuwa sawa, wao wote walitaka kilicho bora kabisa kwangu, na kwa vile wao walikuwa ndugu zangu wa karibu, bila shaka hawangenidhuru. Nilikuwa ninaishi katika usafishwaji, na ingawa nilijua hivi vilikuwa vita vya kiroho, sikuwa na nguvu ya kupigana tena. Kwa mkutano fulani, kiongozi fulani alinionyeshea kifungu hiki kutoka neno la Mungu, “Kwa maelfu ya miaka, Wachina wameishi maisha ya utumwa na hii imebana sana fikira, mawazo, maisha, lugha, tabia, na matendo yao kiasi kwamba wamebaki bila uhuru wowote. Maelfu kadhaa ya miaka ya historia imewachukua watu muhimu waliomilikiwa na roho na kuwadhoofisha hadi kuwa kitu kinachofanana na maiti iliyoondokewa na roho. Wengi ni wale wanaoishi chini ya kisu cha kuchinja cha Shetani…. Kwa umbo la nje, wanadamu wanaonekana kuwa ni ‘wanyama’ wa tabaka ya juu; kwa kweli wanaishi na kukaa na mashetani wachafu. Bila mtu yeyote kuwashughulikia, watu wanaishi katika mtego uliojificha wa Shetani, na wamenaswa kabisa katika kazi zake za taabu kiasi kwamba hawawezi kutoroka. Hawakusanyiki na wapendwa wao katika makazi yao ya furaha, kuishi kwa furaha na kuyaishi maisha ya kuridhisha, bali wanaishi Kuzimu, wakishughulika na pepo na kushirikiana na mashetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (5)). Kwa njia ya ufunuo katika neno la Mungu na ushirika na ndugu zangu wa kiume na wa kike, nilitambua kwamba huku wakionekana kuwa jamaa zangu kutoka kwa nje, na maneno yao yanakubaliana na mahitaji ya mwili wangu, mawazo yao, dhana, maisha, lugha, tabia, na matendo vimebanwa kwa sababu ya upotovu wa shetani. Wote ni makafiri, mitazamo yao yote na yote wanayojadili huja hutoka kwa Shetani, na yale ambayo wao huyafuatilia ni tamaa mbovu za mwili, ambapo hakuna yoyote kati yao yanayokubaliana na ukweli. Nikiwasikiza, nitaangukia njama za Shetani. Sina ukweli wowote na sina utambuzi, na mawasiliano zaidi nao yangenifanya tu kupotoka zaidi. Singepata faida yoyote kwalo, wangenileta tu kwa uangamiaji. Wakati huo, nilikuwa na ufahamu kiasi wa maneno ya Mungu “Wote wasioamini, pamoja na wasiotenda ukweli, ni mapepo!” lakini bado sikuuelewa msemo huo kikamilifu. Baadaye, Mungu alipanga mazingira ambayo yalinionyesha asili ya kweli ya mishikamano ya familia.

Familia yetu daima imekuwa familia mwenyeji, na siku moja katika mwaka wa 2005, kutokana na ripoti ya mhalifu fulani, wazazi wangu na ndugu kadhaa wa kike na wa kiume walikamatwa na polisi wa CCP. Dada yangu wa kuzaliwa naye kwa bahati nzuri alinusurika kufa maji alipokuwa akitoroka, akitoroka tu na maisha yake kwa sababu Mungu alimlinda. Wazazi wangu na ndugu zangu wa kike na wa kiume katika nyumba ya familia yangu waliwekwa kizuizini na kufainiwa, na wote waliteswa, wote walitokea na majeraha. Niliposikia habari hizo, sikuweza kuzidhibiti hisia zangu. Sikuwa na upendo wa kutimiza majukumu yangu. Nilifikiria, “Kwa wakati kama huu sina budi kwenda nyumbani lolote litokealo. Wazazi wangu walinilea, na sasa kwa kuwa wako katika matatizo, hata kama siwezi kufanya chochote, ni lazima angalau niwe hapo kuwaangalia na kuwapa faraja.” Kwa hiyo, nilichukua garimoshi na kufululiza hadi nyumbani kwa shangazi wa upande wa baba (ambaye pia huamini katika Mungu) kuwaona wazazi wangu. Wakati huo niliona majeraha yao yalikuwa hayajapona, nilihisi hali ya kuogofya ndani yangu, na machozi yakavuja machoni mwangu. Ilionekana kama wazazi wangu walikuwa wamedhalilishwa. Hapo ndipo wazazi wangu waliniambia: Wakati wa kutoroka kutoka kwa polisi, dada yangu wa kuzaliwa naye alitumbukia katika mto (hili lilitokea mwezi Desemba, baada ya giza). Maji yalikuwa yamemfika kwa shingo yake, na mikondo ya mto ilikuwa na nguvu, mimea pori ilipatikana juu ya mguu wa suruali yake ndefu, viatu vyake vilikuwa vimekwama katika matope, na yeye hakujua jinsi ya kuogelea, hivyo lilikuwa fumbo kabisa jinsi alivyofika upande ule mwingine. Mungu lazima awe alimlinda kimiujiza, ama matokeo yangekuwa ya kuogofya mno kuyatafakari (maji hayo ya kina kirefu na mikondo ya nguvu yalikuwa yamechukua maisha ya mtu wa miaka 40 siku kadhaa kabla). Baadaye, dada yangu wa kuzaliwa alijificha katika nyumba ya dada mzee kumliko ambaye alimpa dadangu nguo za kubadilisha huku akilia alipokuwa akikausha nguo zake zilizolowa maji juu ya moto, na vinginevyo alimtunza vizuri sana. Siku kadhaa baada ya hayo akapata habari kuwa nyumba ya huyu dada mzee kumliko haikuwa salama tena, hivyo dada yangu wa kuzaliwa akaenda kujificha nyumbani mwa shangazi yangu wa upande wa mama. Alitoka nje wakati wa mchana kuleta barua kwa kanisa letu akimjulisha kiongozi wetu hali ya familia yangu, lakini aliporudi, binti mdogo wa shangazi yangu wa upande wa mama akamwambia, “We binamu, kwa nini ulirudi? Nilidhani uliondoka. Tumekunja kitanda tayari” Dada yangu akatambua kuwa shangazi yangu wa upande wa mama aliogopa kujihusisha na hakutaka kumruhusu akae huko, hivyo akilia, aliondoka nyumbani mwao, na akahatarisha kukamatwa kwa kuja nyumbani kwa sababu hakuwa na mahali pengine pa kwenda. Baada ya wazazi wangu kuachiliwa, wakati walipata habari juu ya kisa cha dada yangu wa kuzaliwa kukaribia kuzama na jinsi alivyofukuzwa na shangazi yangu wa upande wa mama, walikuwa na hasira sana, lakini shangazi yangu wa upande wa mama, kwa kutuliza akiamini kuwa alikuwa sahihi, akajibu na, “Hiyo ni kweli, tulikuwa na hofu ya kujihusisha. Mlijiletea kukamatwa huku wenyewe. Mlikuwa na maisha mazuri kabisa, lakini ilibidi mwende na kuharibu mambo, na sasa mlikuwa karibu kumfanya mtu auawe!” Sikuwahi kuwaza kwamba jamaa zangu wa karibu, watu wa karibu na mimi katika siku za nyuma, wakati ambapo chama cha CCP kilikuwa kikiikamata familia yangu na maisha yao yalikuwa hatarini, wakati ambapo faraja inahitajika zaidi, kwa kweli wangesema maneno kama hayo ya kinyama au kufanya mambo ya kikatili kama hayo. Kujua kwamba wangeweza kunifanya kuhuzunika sana. Hakuna watu wowote tuliowasaidia sana katika siku za nyuma walikuja kutuangalia au kutufariji. Wale waliokuwa na uhusiano bora kabisa nasi hawakukosa tu kuzungumza na wazazi wangu walipokutana mitaani, lakini pia waliwaondokea wazazi wangu njiani mwao. Baadhi ya watu waliotuamkia kwa vichwa na kutujulia hali walituonyesha visogo na kupiga domo. Ni ndugu zetu wa kiume na wa kike waliokuja kututembelea na kufanya ushirika nasi nyakati za jioni. Sikuamini kamwe kuwa familia yetu ingeweza kufikwa na hali duni kama hiyo. Nilinaswa tena katika uchungu, na mawazo ya kumsaliti Mungu yakijitunga katika moyo wangu. Baadaye, baada ya kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu, nikapitia yale ndugu zangu wa kiume na kike waliyokuwa wamefanya ushirika kuyahusu, “Uhusiano kati ya watu una msingi wake si katika kitu ila mapatano, familia na marafiki husaidiana tu juu ya msingi wa matumizi ya mapatano.” Pia niliwaza nyuma kwa mazungumzo ya wazazi wangu kuhusu walichokipata kutokana na uzoefu wao wa kukamatwa, kwa mfano: Wakati polisi walipotumia mjeledi wa ngozi kumpiga baba yangu, alisema hakuhisi maumivu mengi mno, na kwamba mshipi ulikatika vipande vitatu wakimpiga. Dada yangu alisema hakuhisi hofu yoyote kamwe wakati wa uzoefu wake, na ingawa kulikuwa Desemba, alisema hakuhisi baridi akitoka nje ya maji. Mungu alimpa nguvu ya ziada na imani. Kukamatwa na chama cha CCP kwa kweli kuliifanya imani yao iwe thabiti zaidi. Kuliwafanya kuwa na nguvu zaidi. Baba yangu alisema kwamba hakuyaamini maneno ya Mungu kuhusu jinsi Mungu hufichua chuki mbovu ya CCP kuhusu ukweli katika siku za nyuma, na kwamba alikuwa ashikiwa mfalme wa mashetani, lakini tukio hili ilimwonyesha kwamba CCP kilikuwa kundi la majambazi tu, magaidi ambao wangechukua kitu chochote nyumbani mwetu chenye thamani ya fedha na afadhali wangewakamata waumini katika Mungu wenye kutii sheria kuliko kuwashika wauaji na wachomaji mali. Niliaibika nilipofahamu kwamba sisi wote huishi chini ya uongozi wa Mungu, kila kitu tunachokipitia ni sehemu ya ukuu wa Mungu na mpangilio Wake, hakuna mtu aliye na nguvu za kumsaidia mwingine, upendo wa kifamilia utatupeleka tu mbali na Mungu, na kwamba mambo ambayo watu wanaweza kusaidiana nayo hukubaliana na mwili tu, siyo na ukweli. Mawazo kama “bila kutaka mwili wa wazazi wangu kuteseka” hayakosi tu kutoleta faida kwa maisha yao, pia hayaleti faida kwa wokovu wao. Ni Mungu pekee anayejua mtu huhitaji nini, na Mungu humpenda mtu zaidi. Niliona kifungu cha neno la Mungu kilichosema, “Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipia gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake(“Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kwa njia ya maneno ya Mungu na uhalisi, niliona umaajabu na ukuu wa nguvu ya uhai ya Mungu, kwamba Yeye huishi miongoni mwa watu wakati wote, wakati wote huwaongoza wanadamu na huonyesha nguvu Yake, na kwamba kila mtu huishi katika mipango iliyoanzishwa na Mungu. Nikilikabili neno la Mungu, niliona jinsi nilivyokuwa mdogo na jinsi uhusiano wa jazba ulivyokosa thamani. Je, ni nini ambacho ningefanya dhidi ya matatizo yaliyoikabili familia yangu? Si Mungu ndiye aliyewalinda, akawatunza, na akawaongoza kupitia tatizo hilo? Je, upendo wa mtu kwa mtu mwingine unaweza kuwa mkubwa zaidi ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu? Wakati huo huo, maneno ya Mungu yalinihukumu, “Ni nani kati yenu kwa kweli anaweza kabisa kutumia rasilmali kwa ajili Yangu na kutoa yote yao kwa ajili Yangu? Nyinyi nyote mu shingo upande, mawazo yenu yanaenda pande zote, yakifikiria juu ya nyumbani, dunia ya nje, chakula na mavazi. Licha ya ukweli kwamba uko mbele Yangu ukifanya mambo kwa ajili Yangu, katika moyo wako bado unafikiria mke, watoto na wazazi wako walio nyumbani. Je, haya yote ni mali yako? Mbona usiwakabidhi mikononi Mwangu? Je, hunisadiki vya kutosha? Au ni kwamba unahofia Nitafanya mipango isiyofaa juu yako? Mbona daima wewe huwa na wasiwasi kuhusu familia yako ya mwili? Wewe huwatamani sana wapendwa wako! Je, Ninamiliki nafasi fulani moyoni mwako? Na bado unazungumzia kuhusu kuniruhusu Mimi kutawala ndani yako na kumiliki nafsi yako nzima—haya yote ni uongo mdanganyifu! Ni wangapi kati yenu ambao ni wa kanisa kwa mioyo yenu yote? Na ni nani kati yenu hawafikiri juu yao, lakini ni wa ufalme wa leo? Fikiria kwa makini sana kuhusu hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 59). Niliona kwamba kile nilichopenda katika moyo wangu bado kilikuwa ni familia yangu, kwa sababu sikuwa na imani ya kweli katika Mungu, bado singeweza kuwakabidhi kabisa mikononi mwa Mungu; niliona kwamba sikuishi katika ukweli, na hata kama nilikuwa natekeleza wajibu wangu katika nyumba ya Mungu, mara nyingi niliona wasiwasi juu ya familia yangu, na sikumruhusu Mungu kuumiliki moyo wangu. Sikuweza kumheshimu Mungu juu ya wengine wote na kwa uaminifu kutekeleza wajibu wangu. Nilikuwa nimedanganywa na kuteswa na Shetani. Kama si mambo haya “ya kusikitisha” yaliyokuwa yakinitokea, singeweza kuona mambo kwa dhahiri kamwe. Ni kama vile tu wimbo huu wa neno la Mungu unavyosema, “Inapokuja kwa suala la maisha ya mwanadamu, mwanadamu bado hajapata maisha ya kweli, bado hajang’amua hali ya ukiwa na dhiki ya ulimwengu; isingekuwa kwa ajili ya ujio wa maafa, watu bado wangekubali Ulimwengu, na bado wangejihusisha na ladha ya ‘maisha.’ Je, hii si sauti ya wokovu ambao Mungu anazungumza kwa mwanadamu? Kwa nini, kati ya wanadamu, hakuna yeyote aliyewahi kumpenda Mungu kabisa? Kwa nini mwanadamu anampenda Mungu tu kati ya kuadibu, lakini hakuna yeyote anayempenda Mungu chini ya ulinzi Wake?(“Binadamu Hajui Wokovu wa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kama sio kwa kile hali hizi zilinifichulia, singeweza kwa dhati kuelewa kamwe uhusiano kati ya watu, na bado ningekuwa nadhibitiwa na uhusiano wa kifamilia, mapenzi, na urafiki, kama nimenaswa bila kuchangulika katika ufuatiliaji wa mambo haya, kudanganywa na kufanywa niteseke nayo, nikiwa na furaha katika ujinga wangu; isitoshe, singekuwa kamwe nimepokea ukweli, kamwe singekuwa nimechukua njia sahihi ya maisha, na ulikuwa ni wokovu wa Mungu ambao ulinikubalia kutoonja kamwe ladha ya “maisha” tena. Nilipoyaelewa haya yote, niliamua kwamba ningeamini katika Mungu kwa moyo wangu wote na kufuatilia ukweli ili kulipa upendo wa Mungu kwangu.

Mimi sasa nimetekeleza wajibu wangu kwa familia ya Mungu kwa miaka kadhaa, na katika familia ya Mungu nimepitia upendo wa Mungu. Bila kujali ni wapi nitatekeleza wajibu wangu, Mungu daima yuko hapo ili kunitunza. Mimi huelewana vizuri na ndugu zangu wa kike na wa kiume kana kwamba ni familia yangu, hatutumiani vibaya, na hakuna kubadilishana fadhila. Ndugu zangu wa kike na wa kiume ni waaminifu sana kiasi kwamba hata kama upotovu wetu ukionyesha kwa kila mmoja wetu mara kwa mara, kwa njia ya ufunguzi wa mioyo yetu na kuwasiliana kuhusu ufahamu wetu juu yetu, hakuna kinyongo au tahadhari. Huwa tunasaidiana sisi kwa sisi na kupendana sisi kwa sisi, kila mmoja wetu hutazamwa kwa usawa, na hakuna yeyote ambaye hutendewa tofauti kwa sababu ni maskini au tajiri. Nina matatizo ya kiafya, hivyo mimi mara nyingi huwa mgonjwa, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike ni wenye huruma sana na hunitunza vizuri sana, jambo ambalo lilinifanya nipate uzoefu kwamba hata bila uhusiano wa damu kati ya ndugu zangu, wanaweza kuwa hata karibu kuliko jamaa zangu. Naelewana vizuri na ndugu na dada zangu, na kwa mwongozo wa Mungu, sisi wote hufuatilia ukweli na kujitahidi kutekeleza wajibu wetu.

Uzoefu wangu kwa miaka hii kotekote pia umenisaidia hatua kwa hatua kuelewa mapenzi ya Mungu, na pia kuona kwamba kazi ambayo Mungu amenifanyia ni kazi ya wokovu na upendo, maneno yaliyoonyeshwa na Mungu ni ukweli, lakini hata zaidi ni maneno ambayo huyaokoa maisha yetu. Ukweli huu umekuwa huduma na ulinzi bora wa Mungu kwangu. Kama ningeyaondokea maneno haya au sikuyatazama mambo kutoka kwa msingi ambao maneno haya hutoa, ningejiangamiza. Nilikuwa nimepotoshwa na Shetani kabisa na kushindwa kufahamu waziwazi maana ya maneno ya Mungu, hivyo Mungu alipanga hali nyingi tofauti, watu, mambo, na vitu vingi, vilivyobuniwa kwa ajili ya mahitaji yangu, kunifaidi na kunikamilisha, kunisaidia nielewe maneno Yake. Katikati ya matatizo yangu na majaribio, mimi bila kujua nilikuja kuona kwamba maneno haya yaliyoonyeshwa na Mungu yote ni ukweli, kwamba hivyo ni vitu ambavyo watu huhitaji. Siyo tu kwamba hivyo vinaweza kuridhia watu maisha na kumruhusu kuishi kwa kudhihirisha maisha ya mtu wa kawaida, vitu hivi pia huashiria njia sahihi katika maisha, kwa sababu Mungu ni ukweli, njia, na uzima. Ni maneno ya Mungu ambayo yananileta katika siku hii. Niko tayari kuweka maneno yake kama wito wangu, alama ya barabarani kusonga mbele, na mwongozo wa kutenda. Hata kama kuna ukweli mwingi ambao siuelewi, kwa njia ya kuendeleza ufuatiliaji wa ukweli na kutimiza wajibu wangu, Mungu atanipa nuru na kuniangazia ili nipate kuelewa maneno Yake. Bado kuna upotovu mwingi ndani yangu ambao ni lazima utakaswe, na ninahitaji kuwa na uzoefu zaidi sana wa kazi ya Mungu pamoja na hukumu ya Mungu na kuadibu na shida zinazoandamana na kusafishwa. Nitatia bidii kufuatilia ukweli. Haijalishi shida au ugumu utakaonipata siku za usoni, nitamfuata Mungu hadi mwisho!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nimebahatika Kumhudumia Mungu

Na Gensui, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp