Mimi Sistahili Kumwona Kristo

13/01/2018

Huanbao Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning

Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike ambao wanaweza kupokea huduma ya kibinafsi ya Kristo, ambao wanaweza kusikia mahubiri Yake kwa masikio yao wenyewe. Katika moyo wangu, nimewaza jinsi ingekuwa vizuri sana kama siku moja katika siku zijazo ninaweza kusikia mahubiri ya Kristo, bila shaka kumwona Yeye kungekuwa kwa ajabu hata zaidi. Lakini hivi karibuni, kwa njia ya kusikiliza ushirika Wake, nimekuja kuhisi kwa undani moyoni mwangu kwamba mimi sifai kumwona Kristo.

Ilikuwa wakati ambapo Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha Juzuu ya 1 hadi 3 zilipotolewa. Niliposikia juzuu ya kwanza, nikahisi mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu alizungumza vizuri mno. Niliposikia ushirika wa Kristo katika toleo la pili (hii ilikuwa kabla mtu yeyote kuniambia huu ulikuwa ushirika wa Kristo), nilidhani dada huyu alikuwa ni kiongozi tu chini ya mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, na hasa wakati Kristo alifanya ushirika kuhusu shida kuhusu jinsi ya kutazama maarifa, sikusikia mijibizo ya shauku ya ndugu zangu wa kiume na wa kike, kwa hiyo nilikuwa na hakika kuwa dhanio langu lilikuwa sahihi, na nilihisi kuwa huyu mzungumzaji hakuzungumza vyema kama yule mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, sikuwa nikisikiliza kwa uangalifu. Baada ya kusikia juzuu ya tatu, baada ya ushirika wa mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, nilimsikia Kristo akisema, “Kuhusu ushirika wa ndugu huyu…,” na nilikuwa na uhakika zaidi kwamba mzungumzaji huyu alikuwa kiongozi chini ya mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, kwa sababu katika ulimwengu wetu, viongozi daima huzungumza kwanza, na wasaidizi wao huzungumza baadaye. Kwa hiyo nikazima kpaaza sautii, nikifikiri, “Nitaisikiliza hii baadaye nitakapokuwa na nafasi.” Siku ambayo nilipata habari kuwa kwa kweli ulikuwa ushirika wa Kristo, nilishtuka, na hatimaye nikasikiliza kwa makini kila neno la mahubiri.

Baada ya hapo, nikaanza kutafakari: Kwa nini nilitamani sana hivyo kusikia ushirika wa Kristo mimi mwenyewe, lakini wakati alipozungumza nasi, sikuweza kuutambua? Nilianza kula na kunywa maneno ya Mungu yaliyofungamana na hali yangu, na kuona kwamba Mungu alisema, “Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna anayemchukulia kama mwanadamu wa kawaida mwenye kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida…. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao humtendea kikawaida wanapokuwa pamoja naye…. Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu). Ikilinganishwa na maneno ya Mungu, na kisha nilifikiri juu ya vile tabia yangu mwenyewe potovu ilivyojidhihirisha wakati hatimaye niliusikia ushirika wa Kristo. Nilipenda kusikia mahubiri ya Kristo na ushirika kwa masikio yangu mwenyewe, lakini wakati hatimaye niliusikia ushirika wa Kristo sikujali. Nilimwona Kristo kama mwanadamu wa kawaida tu. Hii ni kwa sababu sikuelewa kiini cha Kristo, sikuelewa yote ambayo Kristo huifanya kuendelea kuwa duni na huficha, na nilikuwa na mawazo mengi mno na fikira kumhusu Kristo. Ushirika wa Kristo, niliwaza, lazima uwe unawapendelea wale ndugu wa kiume na wa kike walio na njia yamara moja ya kumfikia Yeye, na wengine wakikosa kuruhusiwa kuusikia ushirika Wake na masikio yao wenyewe; Ushirika wa Kristo, niliwaza, ungeandamana na Kristo kutangaza hadharani utambulisho Wake; ushirika wa Kristo, niliwaza, ni lazima uongewe kwa sauti tofauti na ya wengine na katika zamu nyingi sanifu za msemo, kama aina fulani ya mtu wa ajabu; Ushirika wa Kristo, niliwaza, ungeandamana na vifijo vya msisimko, vyenye shauku vya ndugu zangu wa kiume na wa kike; na ikiwa ilikuwa mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu na Kristo wakiongea kwa zamu, kwamba Kristo angeongea kwanza, na mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu angeongea mwisho…. Niliizuia kazi na maneno ya Kristo kwa mipaka ya mawazo yangu, kwa sababu nilimuwaza Kristo kwa namna fulani. Wakati ukweli ulitofautiana na jinsi nilivyoufikiria, nilimchukua Kristo kama mtu wa kawaida na maneno ya Kristo kama yale ya mtu wa kawaida, na wakati wengine walipata mengi kutoka kwa ushirika, sikupata chochote, na badala yake nilifichua kabisa asili yangu ya kishetani ya kiburi, ya majivuno, ya kuchukia ukweli, na nikajifanya mtu anayemkataa na kumpinga Kristo.

Baadaye, niliona katika neno la Mungu: “Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu). “Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? … Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya). Maneno ya Mungu yalinifanya nielewe kwamba sikuweza kutambua sauti ya Mungu kwa sababu nilikuwa na kiburi mno, mwasi mno, na pia mwenye kupenda makuu mno, wa kujaribiwa kwa urahisi mno kusikiliza kwa makini na kukubaliana na wale walio na uwezo na hadhi, huku nikiwaangalia kwa dharau wale bila uwezo na hadhi, hivi kwamba hata kama wangesema kulingana na ukweli singeusikia. Niliposikiliza ushirika sikuwa nimelenga ukweli na sikutamani kupata ukweli, na badala yake nilijitolea mawazo yangu kwa kisio na uchunguzi. Sikufichua chochote isipokuwa kiburi na uasi, fikira na mawazo. Mtu aliye na kiburi, mwasi, na asiyekubali ukweli kama mimi, mtu asiye na uchaji Mungu au shauku mbele ya ukweli kama mimi, ningewezaje kusikia na kujua sauti ya Mungu? Nilikuwaje wa kufaa kumwona Kristo?

Kupitia ufunuo huo hatimaye nilielewa kuwa ingawa nilitaka kumwona Kristo, sikuwa ninafaa kumwona Kristo kwa sababu upotovu wa Shetani kwangu ni wa kina sana, nina kiburi na ni mwasi kwa asili, sina ukweli na sina upendo wa ukweli, sielewi kiini cha Kristo, mimi huhukumu kwa ubaguzi wa upuuzi, nina fikira nyingi mno na mawazo, na Mungu ninayemwamini bado ni Mungu asiye yakini, mfano wa umbo lenye nguvu na umbuji. Na wakati kwa hakika ninapomwona Kristo, mawazo yangu yanaweza kukita mizizi na kiburi changu kinaweza kuchipua wakati wowote, asili yangu mwenyewe ya uasi kwa njia hiyo ikiniangamiza. Sasa ni lazima nijiandae na ukweli, nijitahidi kuelewa tabia yangu potovu na kiini cha Kristo katika maneno ya Mungu, na kuwa mtu anayemwelewa na kumwabudu Kristo.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Utajiri wa Maisha

Wang Jun Mkoa wa Shandong Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili...

Ni Upendo wa Mungu Tu Ulio Halisi

Xiaodong Mkoa wa Sichuan Mungu alisema, “Taifa la China, likiwa limepotoshwa kwa miaka mingi, limesalia hadi leo, kila aina ya ‘virusi’...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp