Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

14/01/2018

Siqiu Mji wa Suihua, Mkoa wa Heilongjiang

Wakati wowote ninapoona kifungu kinachofuata cha neno la Mungu, “Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana, ukinipenda sana, ilhali unateseka na ugonjwa, umaskini, na kutengwa na marafiki na jamaa zako, au ikiwa unavumilia taabu nyingine zozote maishani, bado uaminifu na upendo wako Kwangu utaendelea?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)). Ninahisi hasa nisiye na furaha—hisi ya huzuni hunyatia ndani yangu na moyo wangu husema malalamiko yake yasiyoghuna: Ewe Mungu, Unawezaje kuruhusu wale walio waaminifu Kwako na wanaokupenda Wewe kukutana na msiba wa jinsi hiyo? Matokeo yake, nimekuwa na wakati mgumu kuelewa maana ya mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu ambaye alisema, “Mahitaji ya mwisho ya Mungu ya mtu ni ya kupenda na ya kweli.”

Hivi karibuni, dada ambaye nilikuwa nikiratibu naye alishikwa na ugonjwa wa tezi dundumio kufanya kazi kupita kiasi. Hatua kwa hatua, hali yake ilifikia kiwango ambapo ilimbidi ale milo sita kwa siku. Kwa sababu ya msongo wa ugonjwa huu, nguvu zake polepole zilipungua, na aliishi kila siku katika mfadhaiko, udhaifu na uchovu. Mwili wake haukuweza kutimiza tamaa yake ya kutekeleza majukumu yake na ugonjwa wake ukaongezeka zaidi na zaidi. Sikuweza kuelewa ni kwa nini hili lilikuwa linatokea: “Dada huyu alikuwa ameacha familia yake na kazi iliyokuwa na mshahara wa juu na faida nzuri ili kujitolea kwa utimizaji wa majukumu yake na alikuwa mwaminifu sana. Inawezekanaje kuwa, kwa yote aliyotoa, angetwishwa mateso ya ugonjwa huu kama malipo? ...” Sikufichua hisia zangu kwa nje, lakini moyo wangu ulikuwa katika mfadhaiko—wakati wowote mtu yeyote alipoleta suala hili ningekasirika.

Muda mfupi baadaye, mimi na dada yangu tuliachana, lakini sikusahau kamwe kumhusu. Siku moja, nilimuuliza kiongozi wangu jinsi dada yangu huyo alivyokuwa. Kiongozi huyo akasema: “Mwanzoni alikuwa na hali mbaya sana na alikataa kuitambua kazi ya Mungu. Baadaye, kwa ufahamu alirekebisha hali yake, akitafuta nia ya Mungu ndani ya mateso ya ugonjwa wake. Kupitia maneno ya Mungu, alianza kujijua na kutambua kwamba hakuwa na imani ya kweli. Ndani ya imani yake bado kulikuwa na dalili ya “kubadilishana,” bado hamu ya kupata baraka kupitia imani yake kwa Mungu. Pia alitambua dalili zingine nyingi za uasi ndani yake. Mara alipotambua mambo haya kujihusu mwenyewe, afya yake iliboreka sana. Anapona siku kwa siku, amerudia kula milo mitatu kwa siku na hali yake ni bora zaidi. Anaweza hata kuwasaidia ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji wake kurekebisha hali zao….” Niliposikia habari hii njema, nilishtuka kweli. Nilikuwa nimedhani kwamba mateso ya ugonjwa yangechakaza azimio la dada yangu na kumsababishia mateso makubwa. Akiwa ameumizwa sana na ugonjwa, niliamini kuwepo kwake kwa njia ya kusonga mbele ingekuwa ya giza zaidi na zaidi. Hata nilishuku kwamba hangeweza kuendelea. Leo, akikabiliwa na uhalisi wa hali yake, nilibaki kusimama nikiduwaa. Sio tu kwamba hakuwa amepoteza imani yake, lakini, kwa njia ya kusafishwa kwa ugonjwa wake, kwa kweli alikuwa amekuja kuelewa kazi ya Mungu na kutambua upotovu wake. Alijifunza kutoka kwa uzoefu wake na alikuwa amefanya maendeleo kwa maisha yake. Je, si ugonjwa huu ulikuwa dhihirisho la upendo wa kweli wa Mungu na wokovu wa kweli wa mwanadamu?

Baadaye, nilisoma fungu lifuatalo kutoka katika mahubiri: “Tano, Mungu asema, ‘Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana, ukinipenda sana, ilhali unateseka na ugonjwa, umaskini, na kutengwa na marafiki na jamaa zako, au ikiwa unavumilia taabu nyingine zozote maishani, bado uaminifu na upendo wako Kwangu utaendelea?’ Hitaji hili sio jaribio dogo kwa wanadamu. ... Uaminifu na upendo wa mtu kwa Mungu umejengwa kwenye msingi upi? Inawezaje kuthibishwa kwamba mtu kwa kweli ana uaminifu kwa Mungu? Inawezaje kuonyeshwa kwamba mtu kwa kweli anamiliki upendo kwa Mungu? Haya yanahitaji kuthibitishwa kupitia majaribio na usafisho. ... Unapokumbana na aina hii ya majaribio, lengo la kwanza la Mungu ni kukufunua kuona ikiwa uaminifu na upendo wako hakika ni wa kweli au la. Lengo Lake la pili ni kukusafisha kwa sababu kuna uchafu katika uaminifu na upendo wako. Ikiwa unatambua uchafu huu, ambao unafichuliwa unapokumbana na aina nyingi za majaribio, basi utasafishwa na uchafu huu kuondolewa. Watu wakimiliki uaminifu na upendo wa kweli kwa Mungu, basi haijalishi kitakachowafikia au majaribio watakayokumbana nayo, hawataanguka chini, lakini badala yake wataendelea kuwa waaminifu na kumpenda Mungu bila kuyumbayumba. Kwa wale ambao uaminifu na upendo wao una uchafu na tamanio la kupata faida, haitakuwa rahisi kusimama imara wanapojiwa na majaribio, na itakuwa rahisi kwao kuanguka. Watu kama hawa watafichuliwa kwa urahisi, sio?” (“Ni kwa Kuridhisha Mahitaji ya Mungu ya Mwisho tu Ndio Mtu Anaweza Kuokolewa” katika Mahubiri na Ushiriki Kuhusu Kuingia Katika Maisha). Ni baada tu ya kusoma kifungu hiki cha ushirika nilipotambua kwamba siku zote niliihukumu kazi ya Mungu kulingana na mawazo yangu yaliyounganishwa na mwili. Kwa makosa niliamini kuwa upendo wa Mungu una zawadi nyingi za neema na hakikisho la furaha ya kimwili na amani. Sikuwahi kufikiri kuwa mateso ni aina ya baraka za Mungu. Ni baada tu ya kupata habari ya uzoefu wa dada yangu, nilipoelewa kwamba usafishwaji wa mateso ni dhihirisho la kweli la upendo wa Mungu. Mungu husababisha hali fulani na kutoa maafa kwa watu Wake—iwe kwa njia ya ugonjwa wa kimwili, shida ya kifedha, au matatizo mengine yoyote—sio kwa sababu ya uadui lakini kwa sababu ya wema Wake. Ili kukabiliana na upotovu na upungufu wa mwanadamu, Mungu husababisha kila aina za hali kumjaribu na kumsafisha. Yeye hufanya kazi kupitia mateso haya ili kumsafisha, kumbadilisha na kumpa mwanadamu uzima. Ingawa mwili wa mwanadamu lazima upitie shida ya ajabu katika mchakato wa usafishaji, ambayo inaweza kuonekana kama taabu au vitu vibaya, hili linafichua uchafu mwingi, nia na mitazamo mibaya, tamaa badhirifu, na malengo mabaya ya ufuatiliaji ambayo mwanadamu anayo katika imani yake kwa Mungu ili kwamba aweze kujijua mwenyewe na aweze kuwa na uhusiano wa kawaida zaidi na zaidi na Yeye ili apate polepole kuukuza upendo kwa Mungu ndani ya moyo wake. Faida hizo haziwezi kupatikana kupitia maisha ya burudani. Wakati mtu anapopata masomo yaliyopatikana kutoka kwa mateso ya majaribu yake na huakisi nyuma kwa njia ambayo amechukua, hatimaye yeye huelewa kwamba hukumu za Mungu na kuadibu, kupiga Kwake na kufundisha nidhamu vyote vilikuwa vimesambazwa na upendo Wake usio na kikomo. Upendo wa Mungu sio tu wenye kustawisha na wenye huruma. Sio tu kuhusu kutoa manufaa ya kimwili, lakini pia kusafisha kwenye kutia uchungu, kupiga na kufundisha nidhamu.

Ewe Mungu, asante kwa kufanya kazi kupitia vipengele vyote vya mazingira yangu ili kurekebisha njia yangu ya kufikiria iliyo ya upuuzi na iliyopotoka na kuniruhusu kuona kwamba hata kama upendo Wako hauambatani na mawazo yetu, dhihirisho lake daima hulenga kutuboresha na kutuokoa. Matendo Yako ya upendo daima yamejaa kazi ya bidii ya moyo Wako na hekima isiyoelezeka. Nilitambua pia kwamba hapo awali sikuwa na ufahamu juu Yako hata kidogo na sikuelewa kuwa upendo Wako mara nyingi umefichwa katika hali. Ewe Mungu, kwa heshima ya upendo Unayoshiriki na wanadamu, nakupa Wewe sifa na shukrani! Pia ninatumaini kwamba siku moja mimi pia nitapokea aina hii ya upendo. Upendo huu ukiletwa kwangu, naapa kukubali kiwango chochote cha mateso, ili nipate kupitia na kushuhudia upendo Wako.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ni Nini Husababisha Uongo

Xiaojing Jijini Heze, Mkoani Shandong Kila mara nilipoona neno la Mungu likituomba kuwa watu waaminifu na kuzungumza kwa usahihi,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp