Jinsi Nilivyobadilisha Tabia Yangu ya Kiburi

25/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu, na inafaa kwa uhalisi. Kotekote katika enzi zote Mungu hajawahi kufanya kazi kama hii; leo, Yeye hufanya kazi ndani yenu ili muweze kufahamu hekima Yake. Ingawa mmepitia maumivu fulani ndani yenu, mioyo yenu inajisikia thabiti na kwa amani; ni baraka yenu kuweza kufurahia hatua hii ya kazi ya Mungu. Haijalishi kile mnachoweza kupata katika siku za baadaye, yote mnayoona kuhusu kazi ya Mungu ndani yenu leo ni upendo. Kama mwanadamu hapitii hukumu na kuadibu kwa Mungu, matendo yake na ari daima yatakuwa nje, na tabia yake daima itaendelea kutobadilika. Je, hii inahesabika kama kupatwa na Mungu? Leo, ingawa bado kuna mengi ndani ya mwanadamu ambayo ni yenye kiburi na yenye majivuno, tabia ya mwanadamu ni imara zaidi kuliko awali. Mungu kukushughulikia wewe ni ili kukuokoa, na ingawa unaweza kuhisi maumivu kidogo wakati huo, siku itafika ambapo kutatokea mabadiliko katika tabia yako. Wakati huo, utakumbuka ya nyuma na kuona vile kazi ya Mungu ni ya hekima, na huo utakuwa wakati ambao utaweza kufahamu kwa kweli mapenzi ya Mungu(Neno Laonekana katika Mwili). Nilikuwa nikifikiri kwamba kuwa na shauku na kuwa tayari kulipa gharama katika wajibu wangu kungepata kibali cha Mungu. Sikulenga kukubali hukumu and kuadibu kwa maneno Yake au kufuatilia mabadiliko ya tabia. Nilifanya tu wajibu wangu nikiwa mwenye kiburi na nikiwa dikteta. Niliwazuia na kuwadhuru kina ndugu, na kuharibu kazi ya kanisa. Mwishowe niliona kwamba bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, tabia yangu potovu isingeweza kutakaswa na kubadilishwa na kamwe nisingeweza kufanya wajibu wangu vizuri ili kumridhisha Mungu. Nimeshuhudia kwa kweli kuwa hukumu and kuadibu kwa Mungu ni wokovu wetu.

Mnamo mwaka wa 2016 nilipewa wajibu wa kusanifu mandhari ya filamu. Nilisisimka, nikifiri, “Nilisomea usanifu wa ndani na nina uzoefu wa zaidi ya miaka minne katika uwanja huu wa kitaaluma. Itanibidi nitumie kikamilifu ujuzi wangu wa kitaalamu kufanya wajibu huu vizuri na kumridhisha Mungu.” Baada ya hayo, nilijifunza ustadi pamoja na kina ndugu na tulishiriki kuhusu kanuni. Nilianza kuona matokeo kiasi katika wajibu wangu baada ya muda fulani. Nilipomsikia mtu akisema, “Mlisanifu vizuri mandhari haya ya filamu. Yana uhalisi kabisa,” ingawa nilijibu kwa kusema kwamba hilo lilitokana na mwongozo wa Mungu, nilifikiri, “Bila shaka, hujui ni nani aliyeyasanifu? Mimi ni mtaalamu!” Nilianza kutembea huku nikijiamini na nilizungumza kwa sauti kubwa zaidi. Nilipoona makosa fulani katika wajibu wa wengine, niliwadharau. Niliacha kujadili nao mipangilio ya mandhari ya filamu. Nilifikiri kwamba kwa kuwa nilikuwa nimesomea usanifu, hakukuwa na haja, kwamba huko kulikuwa kupoteza wakati kwa sababu wangekubaliana na maoni yangu kwa vyovyote vile. Nilibuni mpango wangu mwenyewe na kisha nilikwenda kuuzungumzia na mwelekezi.

Baada ya kupandishwa cheo na kuwa kiongozi wa timu, niliwapuuza kina ndugu hata zaidi. Wakati mmoja tulipokuwa tukiandaa onyesho la mkahawa, Ndugu Zhang aliyekuwa kwenye timu alisema, “Mlango wa mbele si mrefu kiasi cha kutosha, haupendezi.” Sikuyakubali hayo. Niliwaza, “Nimesanifu mandhari mengi sana ya filamu ya mkahawa. Je, unadhani kweli kwamba sijui mlango unapaswa kuwa mrefu kiasi gani? Hujasanifu mandhari mengi ya filamu, hukusomea usanifu, au kuwa na uzoefu wa vitendo, lakini unataka kumfunza samaki jinsi ya kuogelea.” Nilikataa pendekezo lake haraka na kumshurutisha kila mtu auache jinsi nilivyotaka. Mpiga picha alipouona, alisema kwamba mlango huo ulikuwa mfupi sana na ungezuia picha. Hakuweza kupiga picha za sinema kwa njia hiyo. Hatukuwa na lingine ila kutengeneza mlango mpya. Baadaye, tulihitajika kutengeneza kabati, kwa hivyo nilimwambia Ndugu Chen alitengeneze kulingana na mchoro wangu. Alisema, “Sehemu ya katikati ni pana mno. Haipendezi. Je, unaonaje tukilifanya liwe nyembamba zaidi?” Niliwaza, “Niliangalia taarifa za aina yote mtandaoni na hivi ndivyo vipimo sahihi. Ukifanya ninalosema, hutakosea.” Huku nikiendelea kushikilia msimamo wangu, nilisema, “Unazungumzia nini? Litengeneze tu kama nilivyolichora!” Mwishowe, kila mtu alisema kwamba sehemu ya kati ilikuwa pana mno na haikupendeza. Ndugu Chen alilazimika kutumia wakati mwingi zaidi kulirekebisha, jambo ambalo lilichelewesha kuendelea kwa kupiga picha za sinema. Bado sikutafakari au kujaribu kujijua, bali nilipuuza jambo hilo. Niliwaza, “Je, nani asiyekosea wakati mwingine? Muda kidogo tu na vifaa vichache tu vitahitajika kulitengeneza. Si jambo gumu.”

Wakati mmoja baada ya mkutano, Ndugu Zhang alinipa majibu haya: “Nimegundua kwamba hivi karibuni umekuwa ukishikilia sana maoni yako mwenyewe unapofanya kazi na wengine. Hujakuwa ukisikiliza mapendekezo yetu na unakataa mengine ambayo yanawezekana kabisa. Wewe huzungumza kwa njia inayowadhalilisha na unawazuia watu, ukisisitiza daima kwamba tufanye mambo kwa njia yako. Haya yote ni maonyesho ya tabia ya kiburi.” Nilikubali haya kwa kusema lakini nilikuwa nikiwaza, “Mimi ni mwenye kiburi, lakini hilo si tatizo kubwa.” Siku chache baadaye, Ndugu Liu pia alinishughulikia kwa ajili ya kuwa mwenye kiburi, akisema kwamba sikuwasikiliza wengine na niliwazuia. Nilipinga hata kabla ya yeye kuweza kumaliza kuzungumza. Niliwaza, “Hakuna kati yenu aliye bora kama mimi. Mnathubutu vipi kunishughulikia?” Kadiri nilivyozidi kuwaza kuhusu hilo, ndivyo nilivyozidi kukataa kulikubali. Hata nilikuwa nikitoa visingizio nilipomwomba Mungu. Kadiri nilivyozidi kufanya hivyo, ndivyo roho yangu ilivyozidi kuwa mbovu na kuhuzunika zaidi. Nilivurugikiwa katika usanifu wangu wa mandhari ya filamu, lakini bado sikutafakari juu yangu mwenyewe. Siku moja niligongwa mguuni na kiunzi cha kiti cha chuma na nikapata jeraha kubwa sana. Nilipokea mishono saba hospitalini. Nilijua vyema kwamba hii haikuwa ajali, bali mapenzi ya Mungu ndiyo yalikuwa chanzo chake bila shaka. Mwishowe niliutuliza moyo wangu na kutafakari sana. Kila kina ndugu walipokuwa na mapendekezo au vidokezo vya kusaidia sikushawishika na nilipinga. Sikukubali kunyenyekea hata kidogo. Sikushawishika hata kidogo. Nilimwomba Mungu, nikimsihi Aniongoze ili nijue tabia yangu potovu.

Niliyasoma maneno haya ya Mungu katika ibada zangu za asubuhi. “Ukiwaona wengine kuwa chini yako wewe basi ni mwenye haki binafsi, mwenye majivuno ya kibinafsi na huna manufaa kwa yeyote.” “Usifikiri kwamba una kipaji cha asili, uliye chini kidogo ya mbingu lakini juu sana ya dunia. Wewe si mwerevu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote—na hata inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi kuliko watu wowote duniani walio na mantiki, kwani unajiona sana kuwa bora, na hujawahi kujiona kuwa mtu wa chini; inaonekana kwamba unayachunguza matendo Yangu kwa utondoti kabisa. Kwa kweli, wewe ni mtu ambaye kimsingi hana mantiki, kwa kuwa hufahamu kabisa Nitakachofanya sembuse kutambua Ninachofanya sasa. Kwa hivyo Nasema kwamba wewe hata hulingani na mkulima mzee anayefanya kazi kwa bidii shambani, mkulima ambaye hafahamu maisha ya binadamu hata kidogo na bado anategemeabaraka za Mbinguni wakati anapolima shamba. Huyafikirii maisha yako hata kidogo, hujui chochote chenye sifa sembuse kujijua. Wewe ‘una hadhi ya juu’ sana!(Neno Laonekana katika Mwili). Nilisikitika baada ya kusoma haya. Nilihisi kana kwamba nilikuwa nikifunuliwa na kila neno. Tangu nilipoanza kuwa mbuni wa mandhari ya filamu, nilidhani kwamba nilikuwa mtu mwenye kipaji cha maana kwa kuwa nilifahamu tasnia hiyo na nilikuwa na uzoefu. Niliwaringia kina ndugu, nikifikiri kwamba nilikuwa mtaalamu, kwa hivyo hakuna yeyote aliyestahili wakati wangu. Nilitoa kauli ya mwisho kila mara na sikutaka kujadili kazi na wengine. Nilidhani kwamba huko kulikuwa kupoteza wakati kwa kuwa hawakuwa na ujuzi wowote wa usanifu. Nilipojadili kitu kwa kusita, nilidhani kwamba nilikuwa mjuzi zaidi kwa hivyo niliweza kuona mambo kwa ufahamu zaidi. Sikuwahi kutafiti chochote walichokipendekeza, lakini niliwapuuza tu. Sikuwa hata na heshima ya kimsingi kabisa kwa wengine. Ndugu waliposema kwamba nilikuwa mwenye kiburi na kunitia moyo nitafakari, sikukubali hilo pia, lakini nilisalia mwenye upinzani. Niliona kwamba nilifichua tu kiburi. Kwa kuwa niliishi kulingana na tabia yangu ya kiburi, niliwadharau tu wengine na niliwazuia na kuwadhuru kina ndugu. Nilikuwa dikteta na mwenye kiburi katika kazi yangu, nikiwashurutisha wengine wanisikilize, nikiwasababisha wafanye mambo upya kila mara na kuvuruga kazi ya kanisa. Kweli nilikuwa nikitenda maovu! Nilipogundua haya yote, niliogopa kidogo. Nilimwomba Mungu na kutubu Kwake. Sikutaka kufanya mambo kutokana na kiburi tena.

Baada ya hapo, niliacha kujijali kwa makusudi katika wajibu wangu na nilisikiliza zaidi mapendekezo ya wengine ili kufidia kasoro zangu. Wakati mwingine nilibuni mpango na kina ndugu walikuwa na mapendekezo mengi ambayo yalikuwa tofauti na mawazo yangu. Wakati mwingine nilikuwa karibu kuwapuuza, lakini niligundua kwamba nilikuwa mwenye kiburi tena. Nilimwomba Mungu moyoni mwangu, nikimsihi Aniongoze ili nijikane na nisiishi tena kulingana na tabia yangu potovu. Nilitaka kufuata mapendekezo ya mtu yeyote, ambayo yangenufaisha kazi ya nyumba ya Mungu zaidi. Mara nilipoanza kukubali maoni ya wengine, niligundua kuwa vifaa vyetu vya uigizaji vilifanya kazi vyema zaidi, vilifaa zaidi, vilikuwa vya utendaji zaidi, na vingeweza kutengenezwa haraka zaidi. Nilionja utamu wa kuyatenda maneno ya Mungu. Lakini sikuelewa kwa kweli asili yangu ya kiburi na nilikosa kujitambua. Miezi michache baadaye niliona kwamba mandhari yetu ya filamu yalipokelewa vyema na kila mtu na nilikuwa na mafanikio kiasi katika wajibu wangu. Punde si punde, tabia yangu ya kiburi ilikuwa ikiibuka tena.

Wakati mmoja tulipokuwa tukiunda mandhari ya filamu ya nyumba ya mtu tajiri niliwaza, “Mtu kama huyo anapaswa kuwa na vitu vya hali ya juu ili kuakisi hadhi yake.” Niliwaamuru kina ndugu wapange mandhari ya filamu namna tu nilivyotaka. Ndugu Zhang alisema kwamba yalikuwa ya kisasa mno na hayakulingana na kizazi cha mhusika mkuu Sikufurahia sana niliposikia hayo. Niliwaza, “Unajua nini? Huku kunaitwa kuwa na uwezo wa kubadilika. Lazima tuyabuni kulingana na hadhi yake bila kuyawekea mipaka ya wakati fulani. Kama ninavyoona, hujui kabisa nyumba hizi zinapaswa kuwa na mtindo wa aina gani. Mawazo yako ni ya kale sana.” Nilimwambia, “Najua kipindi hiki cha muda. Niamini tu katika jambo hili.” Muda mrefu haukupita kabla ya Ndugu Chen pia kusema kwamba madirisha yalikuwa ya kisasa mno. Nilikerwa sana, nikijiuliza mbona walikuwa nyuma sana kimaendeleo na hawakuweza kubadilisha mawazo. Nilizuia hasira yangu na nilisisitiza mtazamo wangu. Ndugu Chen hakusema lolote tena. Mandhari ya filamu yalipokamilika, nilishangaa mwelekezi aliposema kuwa usanifu wetu haukuwa na uhalisi, kwamba ulikuwa na madoido mengi na haukufaa umri wa mhusika mkuu vizuri. Tulilazimika kuusanifu upya. Hata hivyo, bado sikukubali hayo. Nilihisi kwamba hawakuuthamini kabisa. Lakini kwa kuwa kila mtu alisema kwamba haukufaa, nilikubali shingo upande kusanifu upya mandhari ya filamu.

Wakati fulani baadaye tulihitaji kitanda cha aina ya kang cha enzi ya miaka ya 1980 kwa ajili ya mandhari ya filamu. Nilidhani kwamba tungehitaji kukiwekea bajeti kubwa, lakini Ndugu Zhang alisema kwamba tungepunguza sana gharama iwapo yeye mwenyewe angekitengeneza na alikuwa na plani ya utondoti akilini. Lakini nililidharau wazo hilo kabisa. Tungeweza kukitengeneza wenyewe kwa gharama ndogo zaidi, lakini hakingedumu sana. Je, huko hakungekuwa kupoteza juhudi? Nilimwambia pia mwelekezi kuwa wazo la Ndugu Zhang kwa ufupi halingefaulu. Mwelekezi alisema kwamba bajeti yangu ilikuwa kubwa sana, kwa hivyo alifutilia mbali onyesho lililokuwa na kitanda cha kang. Baadaye, Ndugu Zhang alitoa pendekezo linguine na nilimkaripia, nikifikiri kwamba hakuelewa na alikuwa mbishi. Dada mwingine aliona kwamba alikuwa akizuiliwa nami na alisema kwamba nilikuwa mwenye kiburi. Nilikataa kukubali jambo hilo. Hata nilipokuwa nikijadili na mwelekezi kuhusu mipangilio ya mandhari ya filamu, nilisalia mwenye kiburi na sikukubali kushindwa. Kwa hivyo, wakati mwingine mandhari hayakuwa kile tulichohitaji na hata yalihitajika kusanifiwa upya. Jambo hili lilichelewesha upigaji picha za sinema.

Niliachishwa wajibu huo muda mfupi baadaye. Kiongozi aliniambia, “Ndugu wamesema kwamba una kiburi, wewe hufanya mambo kama utakavyo na wewe hutoa kauli ya mwisho kila mara. Wewe huwakaripia watu kwa njia inayowadhalilisha. Unatenda kana kwamba wewe ndiwe bosi na wao ni wadogo wako. Kila mtu anahisi kwamba amezuiwa nawe.” Nilishangaa niliposikia haya. Sikuwahi kufikiri kwamba niliwaonekania wengine kama mwenye kiburi sana na asiye na mantiki. Nilifadhaika sana kiasi kwamba sikusikia chochote kingine ambacho kiongozi huyo alisema. Nilitaabika kwa siku chache. Sikuweza kula au kupata usingizi mzuri. Mstari wa maneno ya Mungu ulinijia akilini katika kipindi cha kutafakari kwangu: “Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu….(Neno Laonekana katika Mwili). Nilitafakari haya, nikiwaza, “Nimemwamini Mungu kwa muda wa miaka mitano sasa, lakini sijawahi kujitafakari au kujijua kwa kweli. Nimefichua ujeuri mwingi sana bila kujua. Lazima kweli nitafakari juu yangu kabisa.” Nilimwomba Mungu ombi hili: “Ee Mungu, tafadhali niongoze na Unipe nuru ili niweze kuifahamu tabia yangu potovu na niweze kujichukia na kujikana. Niko tayari kutubu.” Siku moja nilienda safari fupi katika eneo la kupigia picha za sinema ambapo niliona kitanda cha kang cha mtindo wa miaka ya 1980 ambacho kilikuwa kimeundwa kama Ndugu Zhanga alivyokuwa amependekeza. Kilikuwa kimegharimu chini ya nusu ya bajeti yangu ya kwanza. Ndugu Zhang na wengine pia walikuwa wametengeneza vifaa vingi vya uigizaji kwa kutumia kadibodi. Vilikuwa vimetokea vizuri, viliokoa muda na juhudi, na vilitumia mali ghafi chache zaidi. Nilihisi aibu nilipoona haya. Niliona jinsi nilivyokuwa mwenye kiburi na jinsi nilivyokuwa nimechelewesha sana kazi yetu ya kupiga picha za sinema. Nilianza kujiuliza, “Mbona nilikuwa mwenye kiburi sana, daima nikiwashurutisha wengine wanisikilize? Je, chanzo cha kweli cha jambo hili ni nini?”

Katika ibada zangu asubuhi iliyofuata, niliyasoma haya katika maneno ya Mungu: “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno!(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilihisi vibaya niliposoma haya. Nilijua kuhusu tabia yangu ya kiburi lakini sikufahamu chochote kuhusu matokeo ya kiburi changu. Hatimaye niliona kutoka katika kile ambacho maneno ya mungu yalifichua na kwa kutafakari kuhusu maneno na matendo yangu kwamba tabia yangu hunishawishi nitende maovu na kumpinga Mungu. Asili yangu ya kiburi ilinifanya nijikweze sana, kwa hivyo sikuwajali wengine kwa sababu nilikuwa na ujuzi kiasi. Nilidhani kwamba mtazamo wangu wa mambo ulikuwa sahihi kila mara na hakuna mtu aliyekuwa kifani changu, na kwamba walilazimika kufanya kama nilivyosema. Kama ningesema “kushoto”, hakuna yeyote angeweza kwenda kulia, na hakuna yeyote ambaye angependekeza vinginevyo. Nilimkaripia yeyote ambaye hakunisikiliza, na nilishikilia maoni yangu na nilikuwa dikteta. Nilipenda kutawala na nilikuwa nikiitembea kwenye njia ya mpinga Kristo. Maneno haya kutoka kwa Mungu, “Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana;” hasa yalinifanya nifikiri zaidi kuhusu jinsi nilivyojionyesha katika wajibu wangu. Sikuwahi kutafuta mapenzi ya Mungu au kanuni za ukweli. Wengine walipokuwa na pendekezo sikuwahi kuzingatia iwapo lilitoka kwa Mungu na iwapo lilikuwa mwongozo wa Mungu. Kama halikuwa wazo langu basi sikulisikiliza hata kidogo. Niliona kwamba sikumcha Mungu hata kidogo. Nilikuwa mwenye kiburi sana kiasi kwamba niliwatendea wengine kwa dharau na sikuwa na nafasi ya Mungu moyoni mwangu. Katika imani, ninapaswa kutii ukweli na kazi ya Roho Mtakatifu. Pendekezo lolote ambalo ndugu yeyote analo, iwapo linalingana na wazo langu mwenyewe au la, pana uwezekano kwamba lilitoka kwa Roho Mtakatifu. Ninapaswa kulikubali na kulichunguza kwa moyo umchao na kumtii Mungu. Kama linakubaliana na ukweli na linaweza kuifaidi kazi ya nyumba ya Mungu, ninapaswa kulitii na kulitekeleza. Nikikataa kitu kinachotokana na nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu, huko ni kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu na kumpinga Mungu. Jambo hilo linaikosea tabia ya Mungu. Nilifanya wajibu wangu kutokana na kiburi na nilikuwa dikteta, nikiwazuia kina ndugu na kupuuza mawazo mazuri sana. Hii ilivuruga kazi ya kanisa. Kuachishwa kazi kulikuwa tabia ya Mungu ya yenye haki iliyokuwa ikinijia. Nilipofikiri kuhusu jinsi nilivyokuwa nimewadhuru kina ndugu na hasara ambayo nilikuwa nimesababishia kazi ya kanisa, nilijuta sana na nilihisi hatia. Nilichukia sana upotovu wangu. Wakati huo huo, nilijawa na shukrani kwa Mungu, kwa sababu nisingehukumiwa na kuadibiwa vikali kwa sababu ya kiburi changu na ukaidi wangu, nisingewahi kujijua. Ningeendelea kumpinga Mungu.

Baadaye nilisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Wakati mwingi, fikira, vitendo na mawazo ya watu walio na vipaji na vipawa hukinzana na ukweli, lakini wao wenyewe hawajui hili. Bado wanawaza, ‘Tazama jinsi nilivyo mwerevu; nimefanya uchaguzi wa busara sana! Maamuzi ya busara yaliyoje! Hakuna hata mmoja wenu anayeweza kulingana na mimi.’ Wanaishi milele katika hali ya kujihusudu na kujithamini. Ni vigumu kwao kuituliza mioyo yao na kutafakari kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwao, ukweli ni nini, na kanuni za ukweli ni nini. Ni vigumu kwao kuingia katika ukweli na katika maneno ya Mungu, na ni vigumu kwao kupata au kufahamu kanuni za kuweka ukweli katika vitendo, na kuingia katika uhalisi wa ukweli(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinionyesha kuwa tukitegemea vipawa na nguvu zetu maishani, tutakuwa wenye majivuno na kiburi zaidi na tutafikiri kwamba mambo hayo ni ukweli bila kutafuta kanuni za ukweli. Nilikuwa nimedhani kwamba nilikuwa na ujuzi kiasi, kwa hivyo wasingemudu bila mimi katika usanifu wa mandhari ya filamu na vifaa vya uigizaji, lakini ukweli ni kwamba, wengine wao walifanya wajibu wao vizuri sana bila uzoefu wowote wa kitaalamu, na hata walitengeneza vifaa vizuri zaidi vya uigizaji kuliko jinsi ambavyo ningevitengeneza. Nilidhani kwamba nilikuwa na umaizi, mwenye ujuzi, na nilikuwa na mawazo mazuri, lakini nilifanya vibaya. Vitu nilivyovitengeneza havikusaidia na mara nyingi vilihitajika kutengenezwa upya, na hivyo kupoteza wakati, juhudi na pesa. Niliona kwamba kwa kutegemea vipaji na nguvu zangu bila kutafuta kanuni za ukweli, nilikosa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa hivyo sikuweza kufanya kazi yangu vizuri. Iwapo mtu ana nia nzuri, Mungu atampa nuru na kumwongoza. Mungu hufadhili hekima ambayo hakuna mtu anaweza kufikiri. Nilitambua kuwa ujuzi na vipaji hivyo nilivyokuwa nikijivunia sana havikuwa na thamani. Kujaribu kuvitumia kwa faida yangu kulikuwa jambo la kiburi sana na lisilo na mantiki. Niliona haya sana nilipolifikiria hilo. Kisha nilimwomba Mungu sala hii: “Sitaki kuishi kulingana na tabia yangu ya kiburi tena. Ningependa kufuatilia na kutenda ukweli kwa uthabiti, na kufanya wajibu wangu vizuri.”

Baadaye, nilianza kufanya wajibu wa kuwanyunyizia waumini wapya na sikujionyesha sana nilipokuwa nikifanya kazi na wengine. Nilitafuta mapenzi ya Mungu kimakusudi kila jambo lilipoibuka na nilisikiliza zaidi mapendekezo ya wengine. Siku moja ndugu mmoja katika kikundi aliniambia, “Mtindo wako wa kunyunyizia na kuwasaidia kina ndugu ni mgumu kidogo. Haufai vile. Ingekuwa bora kama ungelenga kunyunyizia udhaifu wa watu binafsi.” Lakini sikuridhika sana. Nilihisi kwamba nilikuwa nikitumia uzoefu wangu wote, kwa hivyo iliwezekanaje kwamba nilikuwa nikifanya makosa? Nilikuwa tu karibu kukataa pendekezo lake lakini nikagundua kwamba kiburi changu kilikuwa kimeibuka tena. Nilimwomba Mungu kimoyomoyo, kisha kifungu hiki cha maneno Yake kikanijia akilini: “Hatua ya pili hufanyika watu wengine wanapotoa maoni tofauti—unaweza kufanya nini ili kujizuia kuwa mkaidi? Lazima kwanza uwe na mtazamo wa unyenyekevu, upuuze kile unachoamini kuwa ni sahihi, na umwache kila mtu awe na ushirika. Hata kama unaamini kwamba njia yako ni sahihi, hupaswi kuendelea kuisisitiza. Kwanza kabisa, hayo ni maendeleo ya aina fulani; inaonyesha mtazamo wa kutafuta ukweli, wa kujinyima, na wa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unapokuwa na mtazamo huu, wakati huo huo ambapo hushikilii maoni yako, unaomba. Kwa kuwa hujui kutofautisha mema na mabaya, unamruhusu Mungu afichue na kukuambia jambo bora na linalofaa kufanywa ni lipi. Kila mtu anapojiunga katika ushirika, Roho Mtakatifu anawaletea nyote nuru(Ushirika wa Mungu). Nilikuwa mwenye kiburi na mkaidi sana hapo awali, nikiwazuia wengine na kuvuruga kazi ya nyumba ya Mungu. Nilijua kwamba sikupaswa kuendelea hivyo, nikiwazuia watu na kumpinga Mungu, bali nilihitajika kusikiliza mapendekezo ya watu wengine. Ninapaswa kuyakubali na kutii kwanza, kisha nitafute mapenzi ya Mungu. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kupokea mwongozo wa Mungu. Kwa hivyo, nilimsikiliza ndugu huyu kwa subira na nikagundua kweli kwamba kulikuwepo na nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika mbinu zangu. Njia aliyopendekeza ilikuwa na uwezo wa kubadilika zaidi na wa kurekebishika zaidi. Niliitia katika vitendo na nikagundua kwamba ilifaa sana. Ndugu waliponipa maoni baada ya hapo, sikukataa tena bali niliyakubali na kuyatafiti, na nilijadili mambo na wengine ili kupata njia bora zaidi ya kutenda. Baadaye, kila mtu alisema kwamba alikuwa amepata mengi kutoka kwa unyunyiziaji wa aina hiyo. Nilihisi amani halisi. Nilijua kwamba huu ulikuwa mwongozo wa Mungu, na niliweza tu kutoa shukrani zangu na kumsifu. Pia nilishuhudia baraka za Mungu ambazo zilitokana na kutenda kanuni za ukweli badala ya kufanya wajibu wangu kwa kiburi.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kumpa Mungu Moyo Wangu

Na Xinche, Korea ya Kusini Miaka miwili iliyopita, nilifanya mazoezi ya maonyesho ya kwaya ya Wimbo wa Ufalme. Nilihisi kwamba...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp