Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

0

Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan

Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia “Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha,” jambo ambalo lilinielekeza kuelewa kwamba ni wale tu wanaotenda ukweli wanaoweza kupata ukweli na hatimaye kuwa wale ambao wanaomiliki ukweli na ubinadamu hivyo kupata kibali cha Mungu. Kuanzia hapo kwendelea, kwa makusudi nilifanya jitihada za kuunyima mwili wangu na kutenda ukweli katika maisha yangu ya kila siku. Wakati fulani baadaye, nilitambua kwa furaha kwamba ningeweza kutenda ukweli kiasi. Kwa mfano, siku za nyuma niliogopa kuonyesha upande wangu mwovu kwa wengine. Sasa kwa makusudi nilikuwa wazi na ndugu wa kiume na wa kike, nikichangua tabia yangu potovu. Kabla, wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, ningetoa udhuru na kukwepa wajibu. Sasa nilifanya jitihada makusudi kujikana badala ya kujaribu kuhalalisha tabia yangu mbaya. Katika siku za nyuma, nilipopata msuguano na wenzangu kazini, nilikuwa na mawazo finyu, uchwara na wa kuelekea kununa. Sasa nilipokabiliwa na hali hizo ningeunyima mwili wangu na kutumia stahamala na subira na wengine. … Kila wakati nilipofikiria maendeleo yangu katika kutenda ukweli, ningejihisi kuwa na furaha mno. Nilidhani kuwa uwezo wangu wa kutenda ukweli kiasi ulimaanisha kwamba nilikuwa mweledi halisi wa ukweli. Kwa njia hii, bila kujua nikawa mwenye maringo na wa kujipongeza.

Siku moja, niliona maneno yafuatayo ya Mungu: “Watu wengine husema: ‘Ninahisi kuwa nina uwezo wa kuweka ukweli fulani katika matendo sasa, sio kwamba siwezi kuweka ukweli wowote katika matendo. Katika mazingira mengine, ninaweza kufanya mambo kulingana na ukweli, ambako kumaanisha nahesabika kama mtu anayeweka ukweli katika matendo, na nahesabika kama mtu mwenye ukweli.’ Kwa kweli, kinyume na hali za zamani, au kinyume na wakati ulipomwamini Mungu mara ya kwanza, kuna mabadiliko machache. Katika siku za nyuma, hukuelewa chochote, na hukujua ukweli ulikuwa nini au tabia potovu ilikuwa nini. Sasa unajua mambo fulani na unaweza kuwa na matendo fulani mazuri, lakini hii ni sehemu ndogo tu ya mabadiliko hayo; sio mabadiliko ya tabia yako kwa kweli, kwa sababu huwezi kutekeleza ukweli mkomavu na wa kina ambao unahusisha asili yako. Tofauti na siku zako zilizopita, kwa kweli una mabadiliko fulani, lakini mabadiliko haya ni mabadiliko machache tu ya ubinadamu wako; yakilinganishwa na hali ya juu ya ukweli, wewe bado uko mbali sana na lengo. Hii ni kusema kwamba hujafikia lengo wakati unaweka ukweli katika matendo” (“Kuifahamu Asili na Kuutia Ukweli Katika Vitendo” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusoma maneno haya, sikuweza kujizuia kushtuka. Yote ambayo nimefanikisha yalikuwa ni tabia chache nzuri? Bado niko mbali na kutenda ukweli kwa uhalisi? Je, nini basi, nilifikiri, inamaanisha kutenda ukweli kwa uhalisi? Nilianza kuchunguza jibu halisi la swali hili. Baadaye, nilisoma mahubiri yanayosema: “Wale ambao kwa shauku hutenda ukweli wanaweza kumudu gharama na wako tayari kuzikubali shida zinazohusika. Kwa dhahiri, mioyo yao imejaa furaha na raha. Wale ambao wako tayari kutenda ukweli hawatawahi kufanya kitu tu kwa namna isiyo ya dhati kamwe kwa sababu hawafanyi tu kwa sababu ya maonyesho lakini kwa sababu wana dhamiri na mantiki ya ubinadamu wa kawaida, na wanatekeleza wajibu wao kama viumbe wa Mungu. Kwao, kutenda ukweli ni muhimu katika kuwa binadamu, na ni sifa ambayo yule aliye na ubinadamu wa kawaida anapaswa kumiliki” (Ushirika kutoka kwa Aliye Juu). Baada ya kusoma hili, hatimaye nilielewa: Wataalamu halisi wa ukweli wanaweza kutenda ukweli kwa sababu wanaelewa kusudi la kufanya hivyo. Wao hujua kwamba kutenda ukweli ndiyo maana ya kuwa binadamu, sifa ambayo wanadamu wanapaswa kuwa nayo. Kwa hiyo, hawafanyi hivyo kwa maonyesho; huwa wanauona kama wajibu wao. Wako tayari kuvumilia shida na kulipa gharama; hawana malengo ya kibinafsi na tamaa. Lakini nilitendaje ukweli? Wakati nikifichua tabia zangu potovu, huenda nilikuwa wazi na kuzifunua kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike, lakini katika moyo wangu nilikuwa nikifikiria, “Mnaona jinsi ninavyotenda ukweli? Ninaweza kuweka wazi tabia zangu potovu. Hilo linanifanya kuwa bora kuliko ninyi, naam?” Wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, naweza kuwa sikutoa udhuru kwa sauti, lakini ndani nilikuwa nikisema “Ona? Huwa sitoi udhuru tena. Nimekuwa mzuri sana. Labda ninastahili kama mtu ambaye yuko tayari kuukubali ukweli sasa, naam?” Wakati nilipokuwa na msuguano na wenzangu kazini, huenda kwamba nilijaribu kwa makusudi kujizuia mwenyewe na kuepuka mlipuko wowote, lakini moyoni mwangu nilikuwa nikifikiria, “Mnaona? Mimi si kama nilivyokuwa kabla, kuwa uchwara na mwenye mawazo finyu. Nimebadilika, naam?” … Wakati nilipofikiri jinsi nilivyokuwa nikitenda ukweli, hatimaye niligundua kuwa sikuwa kwa kweli natenda ukweli. Nilikuwa nimejaa nia zangu na tamaa zangu. Nilikuwa nikilifanya kwa sababu ya maonyesho. Nilitaka watu wengine kunipenda na kunisifu. Ningewezaje kusema kwamba nilikuwa nikitenda ukweli kwa sababu nilielewa umuhimu wake? Nilikuwa nikifanyaje hili ili kumridhisha Mungu wangu? Nilikuwa nikifanya hili ili kujiridhisha na kujionyesha kwa wengine. Nilikuwa nikimshutumu na kumlaghai Mungu. Kwa uhalisi, nilikuwa nausaliti ukweli. Kanuni yangu inayodaiwa kuwa “kutenda ukweli” ilikuwa tu kufuata desturi. Lilikuwa ni zoezi la kizuizi, kukoma kwa tabia fulani mbaya. Lilikuwa tu badiliko la nje. Nilikuwa na bado niko mbali sana na kufikia viwango vinavyotakiwa kwa mweledi wa ukweli. Hata hivyo, sio tu kuwa nilifikiri kwa kujipujua kwamba nilikuwa mweledi wa ukweli, hata nilikuja kuwa wa kujipongeza kama matokeo. Tabia yangu ilikuwa kweli iliyovuka mpaka!

Mungu, asante kwa nuru Yako na mwongozo Wako. Asante kwa kunionyeshea kwamba sikuwa mweledi wa kweli wa ukweli na kwamba utekelezaji wangu wa ukweli haukufikia viwango Vyako. Kuanzia siku hii kwendelea, niko tayari kuchunguza nia zangu mwenyewe na kushikilia viwango vinavyohitajiwa kutenda ukweli. Nitajiondolea uchafu na kuwa mweledi wa ukweli.

Maudhui Yanayohusiana

 • Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

  Asante Mungu kwa kunurishwa huku, ambako kumeniinua kutoka kwa upofu. Kama sivyo, ningekuwa bado ningehadaiwa na udanganyifu wangu mwenyewe—nikiinuka mbele na tamaa pofu kwelekea kwa mauti yangu ya karibu sana. Ni gutuko lililoje la kushangaza!

 • Roho ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

  Katika Biblia, Kitabu cha Mithali husema, “Kiburi huja kabla ya maangamizo, na roho ya majivuno hutangulia maanguko” (Mithali 16:18). Nilipoanza tu kazi yangu bila kusita na kwa matumaini makubwa, nilihisi kwamba, moyoni mwangu, nilikuwa napoteza mawasiliano na Mungu. Kazi yangu haikukosa tu kufanikiwa, lakini pia ufanisi wa kazi yetu ya Injili uliacha kupanda sana hadi kuanza kushuka. Nilianguka katika hali ya uchungu zaidi, lakini sikuwa na uhakika nilichokitenda vibaya. Kwa hiyo, nikaenda mbele ya Mungu kwa sala ili nitafute mwongozo.

 • Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu

  Nikiangalia maneno ya Mungu na nikifikiri juu yangu mwenyewe, niligundua kuwa kile nilichokuwa nikifuatilia hakikuwa ukweli kamwe, wala sikuwa nikitafuta kumtosheleza Mungu, lakini badala yake ilikuwa sifa, faida na hadhi. Nikiwa na hadhi, kujiamini kwangu kuliongezeka mara mia moja; bila hadhi, nilikuwa mwenye harara na wa huzuni sana hivi kwamba singeweza kujisumbua kufanya kazi. Kwa kweli nilijisahau kwa hadhi yangu nikiharakisha pote nikijihusisha mchana kutwa na mambo haya yasiyo na maana na yasiyo na thamani na kupoteza wakati mwingi; na nilipata nini mwishowe? Tabia ya aibu niliyoionyesha leo?

 • Mazungumzo Mafupi Kuhusu Chanzo cha Giza na Uovu wa Dunia na Uovu

  Yang Le Mji wa Wuhai, Eneo Huru la Mongolia la Ndani Nilipokuwa bado shuleni, baba yangu alikuwa mgonjwa na akafa. Baada ya kufa, wajomba wa pande zo…