Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

7

Yifan Jiji la Shangqiu, Mkoa wa Henan

Katika siku za nyuma, mimi mara nyingi niliwapima watu kwa sura zao, nikiwachukua watu wachangamfu, wajuzi na wenye umbuji hasa kwa heshima sana. Niliamini kwamba watu kama hao walikuwa wa busara, hodari kwa kuwaelewa wengine na kwa ujumla wema na wakarimu. Ni hivi majuzi tu, kama ambavyo uhalisi umejifichua, nimekuja kurekebisha njia hii ya upuuzi ya kufikiri.

Usiku mmoja karibu na magharibi, nilirudi nyumbani kwa familia yangu mwenyeji na kumwona mwanamume mbichi aliyevalia suti na viatu vya ngozi ambaye alizungumza na kujichukua kwa utulivu wa madaha. Pia alikuwa amevaa jozi ya miwani iliyofuliwa kwa uzuri, ambayo ilitia mkazo tabia yake ya kustaarabika na ya kisomi. Mwenyeji wangu alitutambulisha sote wawili na akaniarifu kuwa huyo mwanamume mbichi alikuwa mwanawe na kwamba sasa alikuwa akifanya kazi kama afisa katika serikali ya manispaa ya jiji fulani kubwa. Nikiwa nimetoka kwa usuli wa umaskini na kuacha shule nilipokuwa na umri mdogo, nilihisi wivu mno kwa ajili ya mavazi yake sanifu, uzuri wenye elimu na adabu njema, bila kutaja shahada yake ya juu kutoka chuo maarufu na ajira stahiki. Kwa hakika ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu kumuona mtu mwenye uzuri kama huo na usomi. Nilifikiria mwenyewe, mtu aliyestaarabika na mwenye hadhi ya juu jinsi hiyo na mwenye elimu na adabu njema atakuwa maridhia kwa hakika, mwenye ubinadamu na razini. Nikiwa na fikra hiyo katika mawazo, nilianza kujaribu kujadili mambo ya imani na mwanamume huyo mbichi, lakini majibizo yake yalikuwa kinyume kabisa na matarajio yangu. Alisimama kwa makelele na kubamiza ngumi yake juu ya meza akisema kwa sauti kubwa, “Ondoka hapa hivi sasa! Kama hutatoka mara moja nitawaita polisi!” Baada ya kumaliza kuzungumza, mara moja alitoa simu yake ya mkono na akaanza kupiga simu nambari 110. Nilijaribu kwa haraka kutengeneza mambo, nikisema, “Rafiki yangu, nina hakika kuwa kwa kweli hutawaita polisi, ni lazima una unacheza.” Hata hivyo, aliendelea kuwa mkaidi na akasisitiza kuwa niondoke mara moja. Nilipigwa na bumbuazi kabisa na sikujua cha kufanya tena. Kuangalia saa yangu niliona kuwa ilikuwa karibu saa nne usiku, kama ningeondoka sasa ningelala wapi? Wakati huo huo, mwenyeji wangu akasema, “Kumechelewa tayari, unaweza kuondoka kesho.” Mara tu mwana wa mwenyeji alipoona kwamba nilikuwa napanga kulala, aliongeza juhudi zake, akinisukuma hasa nje ya mlango, na wakati wa mchakato huo akisema kwa sauti kubwa, “Ningewezaje, ofisa wa serikali na mfadhiliwa wa fedha za umma, kumruhusu mmisionari nyumbani kwangu? Ondoka hapa sasa!” Kwa hayo, kwa ghadhabu akaiinua baiskeli yangu na kunitupia na kisha akanisukuma mimi na baiskeli yangu hadi nje ya mlango. Mwenyeji wangu alinifuata kwa nia ya kunipeleka kwa nyumba ya familia nyingine mwenyeji, lakini mwanawe hangemruhusu, akimvuta kumrudisha nyuma ndani na kuufunga mlango. Nilipokuwa nikienda, nikasikia mwenyeji huyo akilia, “Unatarajia msichana kwenda wapi usiku mkuu akiwa peke yake?” “Mwache aende anakokwenda—akiwa na ulinzi wa Mungu hana kitu cha kuogopa sio?” Alisema kwa sauti kubwa kwa kujibu, akimrudisha mwenyeji nyuma hadi ndani.

Nikitumbulia macho nyota zilizopepesa za anga ya usiku bila kuonyesha hisia na taa za mbele za magari zilizomulika kwenye barabara kuu, nilihisi huzuni na kuwa na moyo mzito. Malalamiko yalidondoka kutoka moyoni mwangu: Kama hutaki niishi nyumbani kwako basi ni sawa, lakini hakuna sababu ya kumzuia mwenyeji wangu anipeleke kwa familia nyingine mwenyeji. Unawezaje kuwa mkatili jinsi hiyo, mwovu mno! Hata mwombaji hastahili kutendewa kwa njia hii! Sijui ambapo familia nyingine mwenyeji ilipo na nimekwama bila mahali pa kwenda usiku wa manane. Napaswa kufanya nini? … Mawazo haya yakiwa yanagongagonga kichwani mwangu, machozi yalikuja machoni mwangu. Wakati huo, picha angavu niliyokuwa nayo ya uzuri wa mwana wa mwenyeji, maarifa, hadhi na elimu na adabu njema zilifutwa kabisa. Nilifikiria maneno katika mahubiri, “Tunawezaje kuwaita wale wanaompinga au kumtesa Mungu watu wema kwa hakika? Tangu mwanadamu alipopotoshwa na Shetani, amekuwa mtaalam wa kujificha na kujifunika kwa falsafa ya maisha. Kwa nje, yeye huonekana kama mtu, lakini wakati mtu anapoanza kumshuhudia Mungu, asili yake ya pepo mbaya huwa inafichuliwa. Sio watu wengi huelewa jambo hili, kwa hivyo mara nyingi hupofushwa na kudanganywa na mambo ya kawaida mno na mambo madogo madogo ya wengine. Maneno na kazi za Mungu zinaweza kumfichua mwanadamu vizuri mno. Wale ambao hawana ukweli ni wanafiki tu. Wale ambao huelewa ukweli wataona kwa dhahiri kuhusu suala hili. Wale ambao hawauelewi ukweli hawawezi kuona chochote kwa dhahiri na matokeo yake ni kuwa mitazamo yao ni ya upuuzi” (“Mabadiliko ya Msingi Katika Mitazamo Ni Ishara ya Kuuelewa Ukweli Kwa Hakika” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Nikitafakari maneno haya, nilikuwa na ufahamu wa haraka. Hakika, ushirika ulikuwa kweli kabisa: Wote waliopotoka wanajua vizuri kujifanya, na kwa sababu tu wanaonekana wenye elimu na adabu njema na wapole kwa nje, haimaanishi ni wazuri kiasili. Ni wale tu wanaopenda ukweli na wawezao kuubali ukweli ndio watu wazuri, wenye ukarimu. Ikiwa mtu anaonekana mzuri kwa nje, lakini hamtambui Mungu au kuukubali ukweli unaoonyeshwa na Mungu—na hata ana uwezo wa upinzani, uchokozi na chuki—basi hawezi kuitwa mtu mzuri. Lakini, nilitumia mawazo yangu mwenyewe na maoni ya kidunia kuwapima wengine. Daima nilidhani kuwa wale walio na maarifa, hadhi na elimu na adabu njema walikuwa wema kila wakati, wenye razini na ufahamu wa wengine. Mtazamo wangu ulikuwa wa upuuzi zaidi. Sikujua hata kidogo, kwamba wale ambao hawamwamini Mungu ni mapepo ambao humpinga Mungu. Kwa nje wanaweza kuonekana wastaarabu na wa kuchangamsha, lakini kwa ndani wamechoshwa na ukweli na wanauchukia ukweli. Mtazamo wa ofisa huyu wa serikali kuhusu imani na waumini ulikuwa mfano kamili. Kwa juu, alikuwa na uzuri, umbuji, na hali ya maendeleo ya maarifa, lakini mara tu nilipoleta masuala ya imani, alishindwa kudhibiti mihemko yake kabisa. Kwa kunishutumu, kunifukuza na kunitisha, alifichua kabisa asili yake ya kishetani ambayo ni yenye uadui kwa Mungu. Nikiwa nimekabiliwa na ukweli huu, nilitambua kwamba sharti niwachunguze watu sio tu kwa kile kilicho nje; cha muhimu ni kutazama mtazamo wao kuelekea kwa Mungu, na kuelekea kwa ukweli. Ikiwa hawaupendi ukweli na kuukubali ukweli, basi haijalishi ujuzi wao au hadhi yao ni kubwa kiasi gani, haijalishi wanavyoonekana wa kupendeza kwa nje, haijalishi jinsi wana elimu na adabu njema, wao bado si wazuri kwa kweli.

Kupitia uzoefu huu, nilitambua kuwa sikuwa nikiwaona watu walikuwa ni akina nani kwa kweli, lakini badala yake nikitegemeza kupima kwangu kwa sura yao. Jinsi nilivyosikitisha, jinsi nilivyokuwa mjinga. Ilifunuliwa kuwa licha ya kumfuata Mungu kwa miaka mingi, bado sikuelewa ukweli na kwa hakika bado sikuwa nimemiliki ukweli. Kwa kuwa, ni wale walio na ukweli pekee wanaoweza kutofautisha watu na kuona asili halisi ya hali; wale ambao hawaelewi ukweli hawawezi kuona asili ya kweli ya chochote. Katika siku zijazo nimeapa kujitolea kutafuta kuuelewa ukweli na kuumiliki ukweli, kujifunza jinsi ya kutofautisha watu na hali kwa njia ya neno la Mungu, kurekebisha maoni yangu yote ya upuuzi na kufuatilia kuwa mtu ambaye analingana na Mungu.

Maudhui Yanayohusiana

 • Roho ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

  Katika Biblia, Kitabu cha Mithali husema, “Kiburi huja kabla ya maangamizo, na roho ya majivuno hutangulia maanguko” (Mithali 16:18). Nilipoanza tu kazi yangu bila kusita na kwa matumaini makubwa, nilihisi kwamba, moyoni mwangu, nilikuwa napoteza mawasiliano na Mungu. Kazi yangu haikukosa tu kufanikiwa, lakini pia ufanisi wa kazi yetu ya Injili uliacha kupanda sana hadi kuanza kushuka. Nilianguka katika hali ya uchungu zaidi, lakini sikuwa na uhakika nilichokitenda vibaya. Kwa hiyo, nikaenda mbele ya Mungu kwa sala ili nitafute mwongozo.

 • Huyu Ni Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

  Kutoka leo, napenda kuchukua kirai “tafuta ukweli na kuwa na hisi ya haki” kama vigezo vya mwenendo wangu, kutafuta kuingia ndani zaidi katika ukweli, kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kujitahidi kuwa mtu mwema kwa dhati hivi karibuni ambaye yu dhahiri juu ya upendo na chuki na ambaye ana hisi ya haki.

 • Mazungumzo Mafupi Kuhusu Chanzo cha Giza na Uovu wa Dunia na Uovu

  Yang Le Mji wa Wuhai, Eneo Huru la Mongolia la Ndani Nilipokuwa bado shuleni, baba yangu alikuwa mgonjwa na akafa. Baada ya kufa, wajomba wa pande zo…

 • Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

  Maneno ya Mungu tena yalinileta kwa ufahamu wa jinsi huduma yangu kwa Mungu kwa kweli ilikuwa ni kujishuhudia mwenyewe na kujiinua na yalinisaidia kuona matokeo mabaya ya tabia hii. Maneno ya Mungu yalinisaidia kuona kwamba asili yangu, kama ile ya malaika mkuu, ingeweza kuniongoza kuwa gaidi dhalimu, na kwamba ningeweza kusababisha maangamizi makubwa. Nilifikiria kuhusu jinsi huduma yangu kwa Mungu haikutimizwa kulingana na kanuni sahihi za huduma; haikuwa ikimwinua Mungu na kumshuhudia Mungu, si kufanya wajibu wangu. Badala yake, siku zangu zilitumiwa kujionyeshwa mwenyewe, kujishuhudia mwenyewe, kuwavuta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele yangu. Je, si aina hii ya huduma ni ya kudharauliwa?