Kuja Nyumbani

14/01/2020

Na Muyi, Korea ya Kusini

Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia, aliye huru kabisa na asiyejali chochote, anayeishi kwa furaha kwa uangalizi wa jicho la Mungu … Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha(“Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila wakati ninapoanza kuimba wimbo huu wa neno la Mungu, ni vigumu kudhibiti hisia zinazosisimka ndani yangu. Hiyo ni kwa sababu hapo awali nilijitenga na Mungu na kuasi dhidi Yake. Nilikuwa kama mwanakondoo aliyepotea, asiyeweza kupata njia ya kurudi nyumbani, na ulikuwa upendo thabiti wa Mungu ambao uliniongoza kurudi katika nyumba ya Mungu. Katika makala yafuatayo, ningependa kushiriki pamoja na ndugu katika Bwana, pamoja na marafiki ambao bado hawajamgeukia Mungu, tukio langu la kurudi katika nyumba ya Mungu.

Niliishi kila siku kwa hofu nilipokuwa mtoto kwa sababu mama na baba yangu walikuwa wakigombana kila wakati. Baada ya kuhitimu kutoka shule ya upili, mama yangu alianza kumwamini Bwana Yesu baada ya jirani kumsihi sana, na nilimfuata kuingia kanisani. Kuanzia wakati huo na kuendelea, nilijua kuwa Mungu ndiye Bwana wa viumbe wote walioumbwa, na kwamba ili kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini, Mungu Mwenyewe mwenye mwili alisulubiwa msalabani ili kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu—upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni mkubwa sana! Huku nikitiwa moyo na upendo wa Bwana, niliazimia kumwamini Bwana kwa dhati na kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake, na kwa hivyo nilipata mwelekeo na kusudi maishani. Baada ya hapo, nilihudhuria mikutano mara kwa mara, nilisoma Maandiko, na kumsifu Bwana, na baada ya muda nilianza kuhisi furaha. Hasa niliposoma katika Biblia kwamba katika siku za mwisho Bwana angekuja tena juu ya wingu na kutukaribisha katika ufalme wa mbinguni, moyo wangu ulijawa na tumaini hata zaidi. Zaidi ya hayo, mchungaji mara nyingi alitueleza kinaganaga kuhusu aya hii ya Maandiko katika mikutano: “Ninyi wanadamu wa Galilaya, mbona mnasimama mkiangalia mbinguni? huyu Yesu, ambaye amechukuliwa kutoka kwa ninyi kwenda mbinguni, atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni” (Matendo 1:11). Nilisadikishwa hata zaidi kuwa Bwana Yesu angeshuka juu ya wingu jeupe ili kutukaribisha nyumbani kwetu mbinguni!

Mnamo mwaka wa 2005, nilikutana na Mkorea mmoja ambaye alianza kuwa mpenzi wangu na nilienda naye nchini Korea. Kwa sababu ya kizuizi cha lugha, nilijaribu kutafuta kanisa la raia wa kigeni wa kutoka nchi ya China lakini sikuweza kupata lolote, na kwa hivyo roho yangu ilizidi kudhoofika. Bila kujua, nilizidi kuwa na uhusiano wa mbali na Mungu. Tulifunga ndoa, lakini kwa sababu tofauti ya kitamaduni ilikuwa kubwa sana hatungeweza kuendelea kuishi pamoja, kwa hivyo muda mfupi sana baadaye tulitalikiana. Kipingamizi hiki katika ndoa yangu kilikuwa mshtuko mkubwa sana kwangu kiroho, na kilinisababishia uchungu mwingi sana. Kwa sababu ya kuwa katika nchi ya kigeni bila marafiki au familia yoyote, nilihisi mpweke hata zaidi. Nilichoweza tu kufanya ni kumwomba Mungu kimoyomoyo na kumweleza mateso yaliyokuwa moyoni mwangu. Nilimsihi Mungu anielekeze katika kanisa la Kichina ili kwamba niweze kurudi katika nyumba ya Mungu.

Mwaka mmoja baadaye nilipata huduma ya Kichina katika kanisa la Presbiteri, na nilifurahi sana. Mwishowe, niliweza kwa mara nyingine tena kumsifu Mungu kanisani. Lakini kilichonisikitisha ni kwamba, kila tulipofanya mkutano, wachungaji wangetusomea tu vifungu vya maandiko na kutueleza kidogo kuhusu maana halisi ya maneno hayo. Mahubiri yao hayakuwa na nuru yoyote au kitu chochote cha kufurahia. Hawakuruzuku chochote hata kidogo kwa maisha yetu, na mikutano ikawa tu kitu cha utaratibu uliozoeleka tu. Wakati wa mikutano, watu wengine wangekuwa wakinong'onezana, watu wengine wangekuwa wakicheza michezo katika simu zao za rununu, wengine wangekuwa wakilala, wengine wangekuwa hapo wakitafuta tu wachumba, na hata kungekuwa na watu wengine waliokuwa wakikumbatiana. Niliwaza: “Kanisa ni hekalu, mahali pa kumtukuza Mungu. Tunakuja hapa kuhudhuria mikutano lakini hakuna yeyote aliye hata na chembe ya moyo unaomcha Mungu. Mungu lazima amechukizwa sana na kile anachokiona! Si Bwana atajitenga na mahali duni kama hapa?” Lakini wachungaji na wahubiri walitenda kana kwamba hawakuona haya yote yakitendeka, na hawakuzingatia jambo hilo hata kidogo.

Kuishi katika jungu hili kubwa la uovu ambalo ni ulimwengu, nilianza kuchukua njia potovu pole pole, na mara nyingi ningekwenda kwenye burudani nikinywa pombe na marafiki katika wasaa wangu, bila kutenda kamwe kama muumini katika Mungu. Hata hivyo, wakati wowote ambapo moyo wangu ungezidi kujitenga na Bwana, maneno Yake yangetokea akilini mwangu: “Pepo mwenye najisi anapomtoka mtu, yeye hupitia pahali pakavu, akitafuta pumziko, na asilipate. Kisha hunena, Nitarudi ndani ya nyumba yangu ambapo nilitoka; na anapokuja, anaipata kuwa tupu, iliyofagiwa na kutiwa mapambo. Kisha anakwenda na kuchukua pamoja na yeye pepo wengine saba waovu zaidi kumshinda, na wanaingia ndani na kuishi hapo: na hali ya mwisho ya mtu huyo inakuwa mbaya zaidi kuliko ya awali(Mathayo 12:43-45). Maneno ya Mungu yaliniwekea mipaka na kunilinda, na yalinizuia kutenganishwa sana na Mungu au kufanya chochote ambacho kilipita mpaka, kwa ajili ya hofu kwamba ningemkasirisha Bwana na kumsababisha Achukizwe nami. Niliogopa kuachwa na Bwana na kuanguka mikononi mwa roho mwovu.

Katika Krismasi mnamo mwaka wa 2016, ili kupandisha ari kanisani, kanisa lilileta kikundi cha ndugu wenye talanta kufanya maonyesho ya burudani vizuri. Kulikuwa na dada mmoja ambaye sikuwahi kumwona hapo awali ambaye alituimba wimbo wa kumsifu Mungu: “Mandhari iliyochorwa katika Biblia ‘Amri ya Mungu kwa Adamu’ ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao, mshangao na uvutiwaji. Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure, upendo wa Mungu umemzunguka. Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru, huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu. Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake. Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo, yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga. Kutoka wakati wa kwanza Mungu alipowaumba wanadamu, Mungu aliwaweka chini ya uangalizi Wake. Ni uangalizi wa aina gani huo? Ni jukumu Lake kumlinda mtu na kumchunga mtu. Anamtumainia mtu kuamini katika, kuamini katika na kuyatii maneno Yake. Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho Mungu alikitarajia kwa wanadamu. … Je, kuna upendo katika moyo Wake? Si kuna utunzaji na dhima? Upendo na utunzaji wa Mungu ni jambo ambalo linaweza kuonekana na kuhisiwa. Kama wewe ni mtu wa dhamiri na una ubinadamu, utajihisi vuguvugu, ukitunzwa na kupendwa, utajihisi mwenye heri na furaha. Unapoyahisi mambo haya, utatenda vipi mintarafu ya Mungu? Utakuwa mwaminifu Kwake? Upendo wa staha, upendo wa staha hutakua katika moyo wako? Moyo wako utasogea karibu na Yeye? Kutokana na haya tunaona, jinsi upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa mtu. Lakini hata muhimu zaidi kuliko hili ni kwamba mtu anaweza kuuhisi na kuuelewa upendo wa Mungu(“Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Kwa kila neno la wimbo, moyo wangu ulipiga hata kwa upesi zaidi na machozi ya mhemuko hayakuacha kutoka machoni pangu. Nilihisi nilikuwa katika picha hii nzuri nikiandamana na Mungu, nikipendwa na Mungu na nikifurahia vitu vyote Anavyovipa vitu vyote vilivyoumbwa. Hewa, nuru, maji na kadhalika—kila kitu kilikuwa kimejawa sana na upendo wa Mungu! Nilikuwa nikifurahia kila kitu ambacho Mungu alikuwa ametupa lakini moyo wangu ulikuwa umejitenga na Mungu, na jinsi gani Mungu hakika alikuwa amehuzunishwa na jambo hili. Nilihisi hasa kwamba maneno “Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha” yalikuwa Mungu akiuita moyo wangu na roho yangu. Mnamo mwaka wa 2007, wakati ambapo singeweza kuendelea kuishi pamoja na mume wangu na sikuwa na mahali pa kuita nyumbani, Mungu alinipatanisha na Kituo cha Korea cha Haki za Binadamu cha Wahamiaji Wanawake. Walinipa chakula na mahali pa kujisetiri bure na kunipatia wakili. Walishughulikia kesi ya talaka yangu kwa niaba yangu bila malipo. Wakati wangu wa kutuma ombi la kuandikisha uraia ulipofika, Mungu alimgusa mhudumu kutoka kanisa la Presbiteri kuwa mfadhili wangu. Kwa kawaida, Wakorea huwa tayari kwa nadra sana kuwa mfadhili kwa mtu, hasa kwa sababu nilikuwa raia wa kigeni na, zaidi ya hayo, nilikuwa nimeenda katika kanisa hilo mara tatu au nne tu. Nilijua kuwa haya yote yalikuwa yamewezekana kupitia usaidizi wa siri wa Mungu. Pia kulikuwa na ukweli kwamba raia wa kigeni wanaoomba kuandikisha uraia lazima wawe na milioni 30 zilizopatwa katika raslimali za kudumu, lakini sikuwa hata na milioni 3. Ofisi ya Uhamiaji ilinitaka nitoe uthibitisho wa ajira kuonyesha kwamba nilikuwa na uwezo wa kukimu mahitaji yangu, na hawakuniwekea vizuizi vyovyote hata kidogo…. Mungu daima alinifanyia miujiza nilipokuwa na mahitaji mengi zaidi, na yote yalikuwa maonyesho ya ukuu Wake! Upendo wa Mungu ni mkubwa na ni mwingi, na bado nilikuwa mwasi sana. Nilikuwa nimemsahau Mungu zamani na kuvunja moyo Wake. Wimbo huu wa sifa uliigusa roho yangu, na niliazimia kupata imani yangu tena na kamwe kutojishughulisha tena na upotovu na kumhuzunisha Mungu.

Mnamo Februari 19, mwaka wa 2017, kichwa changu na macho yangu yalianza kuuma sana. Nilienda hospitalini lakini matibabu niliyopokea hayakufaulu. Dada Li, aliyekuwa kanisani kwetu, alinitambulisha kwa mmoja wa marafiki zake aliyejua dawa za kienyeji za Kichina na alisema kwamba wakati wa matibabu ungechukua muda wa wiki moja tu kuwa wenye matokeo yaliyotarajiwa. Nilienda pamoja naye kutibiwa, na siku hiyo tulikutana na ndugu mmoja mwenye jina la ukoo Jin, aliyekuwa rafiki wa yule mtu ambaye alijua dawa ya Kichina. Sikutarajia kukutana na ndugu katika Bwana, na nilidhani lazima ilikuwa imepangwa na Mungu. Nilipata kuzungumza kuhusu Biblia na Ndugu Jin. Ndugu Jin alitusomea mfano wa mabikira kumi kutoka katika Biblia. Aliniuliza, “Dada, unatarajia kurudi kwa Bwana?” Nilisema, “Hakika!” Ndugu huyo akasema, “Basi Bwana atarudije?” Nilisema bila kusita, “Maandiko yanasema atashuka juu ya wingu!” Ndugu huyo akasema, “Unajua nini? Bwana amerudi tayari.” Nilishangaa kusikia hivyo, na nilisema, “Marko mlango wa 13 mstari wa 32 inasema: ‘Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu.’ Hakuna anayejua wakati Bwana atakuja. Unasema kwamba Bwana amerudi, lakini je, unawezaje kujua?” Ndugu Jin hakunipa jibu la moja kwa moja lakini badala yake alipata unabii fulani katika Biblia kuhusu kurudi kwa Bwana. Luka 12 inasema: “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja.” Luka 17:24-26 inasema: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki. Na jinsi ilivyokuwa katika siku za Nuhu, hivyo ndivyo itakavyokuwa pia katika siku za Mwana wa Adamu.” Ufunuo 3:20 inasema: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi.” Yohana 10:27 inasema: “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata.

Mara alipomaliza kusoma, Ndugu Jin alisema, “Bwana anataka tuwe macho kwa sababu hakuna anayejua siku Atakayokuja. Lakini kulingana na yale yanayosemwa na unabii, Bwana atakapokuja tena itakuwa katika namna ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu ni Mungu kuwa mwanadamu, ambayo inamaanisha Mungu kuwa mwili. Hata ingawa hatujui ni wakati gani hasa Bwana atakapokuja, tutamjua kwa sauti Yake. Hii ni kwa sababu kondoo wa Mungu wataisikia sauti ya Mungu, na watakapoisikia, watamfuata….” Kisha nilifikiria kuhusu mchungaji wangu ambaye alikuwa amesema kwamba mtu yeyote aliyekuwa akishuhudia kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi katika mwili alikuwa mdanganyifu. Sikuweza tena kusikiliza alichokuwa akisema Ndugu Jin, kwa hivyo nilituma ujumbe kwa mchungaji uliosema, “Kuna mtu ananiambia kwamba Bwana amerudi akiwa mwili. Je, yeye ni wa kanisa gani?” Mchungaji alijibu, akisema, “Anatoka katika kanisa la Umeme wa Mashariki.” Aliniambia niondoke mara moja na nisiwasiliane naye tena. Pia alinitaka nisiwahi kuvisoma vitabu vyao na aliendelea kunitumia mahubiri kadhaa ya jinsi ya kujihadhari dhidi ya uvumi. Nilidhani kwamba chochote ambacho mchungaji alisema lazima kiwe sahihi, na kwa hivyo niliamua kutosikiliza tena ushirika wake na nilimpuuza tu.

Kwa mshangao wangu, alasiri ya tarehe 20, Ndugu Jin na dada yake mdogo walikuja mahali nilikokuwa nikipokea matibabu na aliniambia mengi kuhusu kazi ya kurudi kwa Bwana. Hata hivyo, kwa sababu asubuhi hiyo nilikuwa nimepokea tu habari za kufariki kwa mama yangu, na vile vile kuwa na tashwishwi juu ya kile walichokuwa wakihubiri, sikuweza tu kukubali chochote walichokisema. Jambo hili liliendelea kwa muda wa siku tatu, na ilionekana kana kwamba Ndugu Jin hakuwa amekata tamaa kuhusu kunihubiria injili. Lakini kwa sababu ya msukosuko wangu wa ndani, nilimwambia aniache. Nilisema, “Achana nalo. Ukiendelea kunizungumzia, basi usipoondoka, nitaondoka!” Ndugu Jin aliona kwamba kwa kweli sikuwa nikisikiliza na hakuwa na lingine la kufanya ila kuondoka. Nilidhani Ndugu Jin hangejaribu kuja tena, lakini nilishangaa siku iliyofuata aliandamana na mtu aliyeitwa Ndugu Cheng na aliendelea kunihubiria injili. Nilijiwazia: “Kwa nini anaendelea kufanya hivi?” Ili kuepuka aibu, nilichoweza kufanya tu kilikuwa kuvumilia, lakini sikuanza mazungumzo yoyote nao. Ingawa niliwatendea kwa dharau, Ndugu Cheng aliendelea kunizungumzia kwa ustahamilivu. Alisema, “Tayari Bwana amekuja ulimwenguni akiwa mwenye mwili na Anatekeleza kazi ya hukumu na kuadibu….” Nilipoona jinsi alivyokuwa mvumilivu na mwenye upendo na jinsi alivyodhani si tatizo kunihubiria, niliwaza: “Watu katika kanisa letu ni dhaifu. Imani yao na upendo wao umefifia. Je, ni kwa nini imani na upendo wa watu wanaoamini katika kanisa la Umeme wa Mashariki ni mkubwa sana? Je, ni nguvu gani inayowasaidia kuendelea na juhudi zao katika kueneza injili kwangu? Isingekuwa kazi ya Roho Mtakatifu, hawangeweza kamwe kufanya jambo hili kwa nguvu zao wenyewe!”

Katika kipindi hiki, kulikuwa na ndugu mwingine mwenye jina la ukoo Yang ambaye alikuwa akichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kama nilivyokuwa nikifanya. Wakati mbapo mimi nilikuwa na mtazamo wa kutojali na wa usahaulifu, Ndugu Yang alikuwa mwaminifu katika uchunguzi wake wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Ndugu Yang alisema kwamba alikuwa amekataa injili ya Mwenyezi Mungu watu walipokuwa wamemhubiria hapo awali, lakini kwamba kuisikia tena leo lazima hakika ni nafasi iliyotolewa na Mungu, na kwa hivyo alikuwa amekuwa tayari kuichunguza. Ndugu Yang aliona kwamba nilikuwa wa kupenda kusikiliza maneno ya mchungaji tu na sio kutafuta nikiwa na akili ya kuzingatia mawazo mapya. Alinitafutia kifungu, ambacho kilikuwa Mathayo 5:3-6: “Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao. … Wamebarikiwa walio wapole: kwani watairithi dunia. Wamebarikiwa wale walio na njaa na kiu ya haki: kwa kuwa watapewa shibe.” Baada ya kusoma neno la Mungu, nilijiuliza: “Kwa nini siwezi kujituliza mbele za Bwana na kutafuta ukweli? Ikiwa kwa bahati fulani kwa kweli Bwana amerudi tayari, na nisisikilize au kuchunguza mahubiri yao, je, sitaachwa nyuma? Ninapaswa pia kuwa na akili yenye kuzingatia mawazo mapya zaidi, na sharti nisifanye uamuzi kwa kutegemea mawazo yangu mwenyewe.” Nilipokuwa tu nimeamua kutuliza moyo wangu na kuchunguza jambo hilo kwa kweli, mhubiri mmoja kutoka kanisa langu alinipigia simu bila kutegemea kuniuliza ikiwa bado nilikuwa na watu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilisema kwamba nilikuwa nao, na mhubiri huyo alinikumbusha tena niache kuwasiliana nao. Kusihi kwa mhubiri huyo kuliondoa mawazo ambayo nilikuwa nayo kuhusu kuchunguza Kanisa la Mwenyezi Mungu. Niliwaza, “Mchungaji na mhubiri wana ufahamu bora kuhusu Biblia zaidi yangu, na hawatambui kuwa Bwana amerudi. Nina ufahamu mdogo sana kuhusu Biblia na sina utambuzi, kwa hivyo heri nisikilize tu yale mchungaji na mhubiri wanayosema.” Nilipokata simu, nilimwambia Ndugu Cheng, “Ikiwa Ndugu Yang anataka kuchunguza jambo hilo, basi ninyi wawili mnaweza kuendelea na mazungumzo yenu. Siyasikilizi tena.” Hivyo tu, kwa mara nyingine tena nilikataa wokovu wa Mungu kwa ghafla.

Nilirudi kazini baada ya wiki moja ya matibabu. Kwa sababu ya kufariki kwa mama yangu, moyo wangu ulikuwa umejawa na uchungu na sikuweza kuacha kuwaza kumhusu. Kila siku niliporudi nyumbani kutoka kazini, ningetazama picha ya mama yangu na kumzungumzia. Siku moja, niliwaza ghafla: “Mimi ni muumini wa Bwana na kila ninapopitia shida au udhaifu wowote, daima ninaweza kumwambia Bwana mambo haya.” Baada ya hayo, kila nilipokumbana na taabu ningekuja mbele za Bwana na kuomba, nikimsihi Bwana anifariji. Lakini bila kujali jinsi nilivyoomba, sikuwahi kuhisi kuguswa moyoni. Wakati mwingine ningelala nilipokuwa nikiomba. Nilikuwa nikiishi katika hali ya wasiwasi mkubwa kila siku wakati huo, sana kiasi kwamba sauti ndogo kabisa nyuma yangu ilinifanya nisihisi hofu isiyoelezeka. Katika hofu na kutojiweza kwangu, nilimwomba Bwana kwa dhati: “Ee Bwana! Moyo wangu umejawa na giza na ninatetemeka kwa woga. Je, ninaweza kuwa nilifanya makosa mahali fulani? Ee Bwana! Katika siku chache zilizopita watu wamekuwa wakiniambia kuwa umerudi kama Mwenyezi Mungu. Ee Bwana! Ikiwa kwa kweli Umerudi na kwa kweli ndiwe Mwenyezi Mungu waliyeniambia kuhusu, ninakuomba Uweke wakati na Uandae hali sahihi kwa ajili ya Ndugu Yang ili anipigie simu au anitumie ujumbe mfupi. Atakaporudi, bila kujali anayosema, nitakuwa na moyo unaokubali kazi Yako mpya na maneno Yako kwa utiifu na kwa hamu. Ikiwa siyo kazi Yako, na ikiwa ujumbe ambao wananihubiria ni wa uwongo na danganyifu, basi tafadhali zuia njia zao na Usiwaruhusu warudi tena.”

La kushangaza ni kwamba, baada ya kuomba hivi, Mungu alitimiza hususa kile nilichokuwa nimekiombea. Ndugu Yang kwa kweli alinipigia simu, na nilimwambia kuhusu kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea katika siku chache zilizopita. Ndugu Yang alisema kwamba moyo wangu ulikuwa umefifizwa kwa sababu nilikuwa nimekataa kazi ya Mungu ya siku za mwisho na nilikuwa nimeasi dhidi Yake. Alitumaini kwamba ningeendelea kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na wakati huu sikukataa pendekezo lake.

Muda mfupi baadaye, Ndugu Yang alinitumia filamu ya injili. Kulikuwa na mstari wa mazungumzo katika filamu hii ambao ulinishtua nikagutuka: “Kwa kuwa tunaamini katika Mungu tunapaswa kumsikiliza Mungu, siyo watu.” “Hiyo ni kweli!” Niliwaza. “Ni Mungu ninayemwamini, na ni neno la Mungu ndilo ninapaswa kulisikiliza! Lakini katika kipindi hicho Ndugu Jin na Ndugu Cheng walipokuwa wakiniambia kuhusu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, niliendelea kumuuliza mchungaji kuhusu jambo hilo. Nilikubaliana na kile ambacho mchungaji na mhubiri walisema na sikutaka kuchunguza kwa bidii kazi mpya ya Mwenyezi Mungu au kusikiliza neno la Mungu. Nilikuwa nimemwamini Bwana lakini sikuwa nimeomba au kutafuta kutoka kwa Bwana, na badala yake nilikuwa nimeamini pasipo kufikiria kile ambacho mchungaji na mhubiri walikuwa wamekisema. Nilikuwa mjinga sana! Biblia inasema: ‘Tunapaswa kumtii Mungu badala ya wanadamu’ (Matendo 5:29). Nilimwamini Bwana lakini sikumtii. Badala yake, niliwatii watu, kwa hivyo, je, sijakuwa mtu anayewaamini na kuwafuata watu? Je, si hivyo ni kumpinga na kumsaliti Bwana? Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na nimeasi dhidi Yake na kumpinga namna hii, nisiyetaka kumkubali Mwenyezi Mungu, je, basi sijakuwa mpumbavu kipofu? Je, sijakuwa nikimzuia Bwana?” Nikiwa na jambo hili akilini, nilitubu sana moyoni mwangu na machozi yalijaa machoni pangu.

Nilikuja tena mbele za Bwana na kuomba: “Bwana Yesu Kristo! Mtu fulani alihubiri injili akisema kwamba Umerudi tayari ukiwa mwenye mwili, na kwamba Wewe ndiwe Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Nashindwa kuwa na uhakika kuhusu jambo hili, lakini niko tayari kuja mbele Zako kutafuta na kukuomba Unipe nuru, ili niweze kutambua sauti Yako. Ikiwa kwa kweli umerudi na Wewe ndiwe Mwenyezi Mungu, nataka kutubu Kwako na kukubali kazi Yako na wokovu Wako. Ninakuomba Unirudishe mbele Zako.” Baada ya kuomba, nilihisi furaha kwa kiasi fulani na hisia ya kufarijiwa ambayo singeweza kueleza. Kilikuwa kitu ambacho sikuwahi kuhisi kwa muda mrefu, na nilijua kuwa Bwana alikuwa amesikia maombi yangu, kwamba ni Bwana aliyekuwa akinifariji, na kwamba lilikuwa thibitisho niliyopewa na Mungu. Nilitaka kwenda mara moja katika Kanisa la Mwenyezi Mungu kuchunguza kuhusu jambo hilo, lakini niliwaza kuhusu jinsi ambavyo hakika nilikuwa nimewakosea ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kwa hivyo niliona haya sana kwenda katika kanisa lao.

Katikati ya mtanziko huu, Ndugu Yang alinipigia simu kuuliza ikiwa nilikuwa na wakati na alisema kwamba alitumai kuwa ningeweza kuendelea kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Nilimwambia kuhusu mashaka yangu. Ndugu Yang alisema, “Hamna shida, sisi waumini katika Mungu sote ni familia moja, na haiwasumbui akina ndugu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu hata kidogo.” Nilipomskia Ndugu Yang akisema haya, nilijua kwamba Mungu alikuwa akionyesha ufahamu juu ya kimo changu kichanga, na kwa hivyo siku iliyofuata nilienda katika Kanisa la Mwenyezi Mungu pamoja na Ndugu Yang.

Ndugu walifurahi kuona kwamba nilikuwa nimepata kujua jinsi ya kurudi kwenye njia. Walinishuhudia kirasmi kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi kuonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Pia walishiriki nami maana ya kazi ya Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho na pia umuhimu wa kupata mwili kwa wokovu wa mwanadamu. Baada ya hapo, nilisoma maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba ‘Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo’ watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).

Baada ya kusoma neno la Mungu, nilitafakari kwa uangalifu juu ya ukweli ambao ndugu zangu walikuwa wameshiriki nami na ambao walikuwa wameshuhudia. Nilifahamu kuwa kuna njia mbili ambazo Bwana atarudi katika siku za mwisho, moja ikiwa kuja kwa Kristo kulikofichwa na nyingine ikiwa kuja kwa Bwana waziwazi kwa wote. Sasa, kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu mwenye mwili ambayo inaanza ndani ya nyumba ya Mungu kweli ni kazi ya kuja kwa Bwana kulikofichwa. Kwa sababu Mungu mwenye mwili amerudi kati ya wanadamu, kuonekana Kwake ni kule kwa mtu wa kawaida na hakuna mtu anayeweza kujua kwa kumtazama tu kuwa Yeye ndiye Mungu. Hakuna anayejua utambulisho Wake kweli, na watu wamefichwa jambo hilo. Ni wale tu ambao wanaweza kutofautisha sauti ya Mungu ndio watakaomjua, watakaomkubali, na kumfuata. Ni kama tu Bwana Yesu alivyosema: “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Wale ambao hawatambui sauti ya Mungu hakika watamchukulia Mungu mwenye mwili kama mtu wa kawaida. Watamkana, watampinga, na kukataa kumfuata Mungu, kama tu Mafarisayo Wayahudi walivyofanya katika wakati wao. Walimwona Bwana Yesu lakini hawakujua sura Yake, na walimlaani Bwana pasipo kufikiria. Wakati wa sasa ni hatua ya kazi iliyofichwa ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Mwenyezi Mungu huonyesha neno kuwahukumu, kuwatakasa, na kuwakamilisha watu. Kabla ya maafa, Atafanyiza kikundi cha watu kuwa washindi, na mara kikundi hiki cha washindi kitakapokamilishwa, kazi ya kurudi kwa Mungu kulikofichwa itafikia kikomo. Maafa yatakapoanza, Mungu atatuza mema na kuadhibu mabaya, na ataonekana waziwazi kwa mataifa yote na watu wote. Wakati huo, unabii kwamba Bwana atakuja waziwazi utatimizwa, kama tu inavyosema katika Biblia: “Na kisha itatokea ishara yake Mwana wa Adamu huko mbinguni: na kisha makabila yote ya dunia yataomboleza, na wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa(Mathayo 24:30). “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7). Hii ndiyo sababu jamaa zote za dunia zitaomboleza Bwana atakaposhuka juu ya wingu. Wakati huu, moyo wangu ulijawa na nuru ghafla, na niliona kwamba kazi ya Bwana ya kuja kulikofichwa ni wokovu mkubwa kwetu. Tunaweza kutakaswa tu na kupata wokovu wa Mungu kwa kukubali hukumu ya neno la Mungu katika kipindi cha kuja kwa Bwana kulikofichwa. Ikiwa hatukubali kazi ya Mungu ya hukumu sasa, basi Mungu atakapokuja waziwazi na mawingu tutakuwa wale waliompinga Bwana, na hakika tutalia na kusaga meno yetu. Wakati huo, majuto yetu yatakuja yakiwa yamechelewa mno, kwa ajili Mwenyezi Mungu anasema: “Hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu.

Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu! Neno la Mungu hufunua siri zote na kufafanua ukweli waziwazi katika vipengele vyote—macho yangu yalifunuliwa na baadaye nilisadikishwa moyoni na kwa neno. Katika siku zilizofuata, nilienda kanisani mara kwa mara kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho pamoja na ndugu. Tulisikiliza nyimbo na kutazama video za muziki, video za masimulizi ya neno la Mungu, na sinema za injili, zote zilizotayarishwa na ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilihisi kuwa nilipata kitu kipya katika kila mkutano na nilihisi furaha isiyo na kifani. Hasa katika sinema za injili, ndugu walishiriki kila suala kwa undani na uwazi kiasi kwamba mashaka na mkanganyiko ambao nilikuwa nimekuwa nao katika imani yangu katika Bwana kwa muda wa miaka mingi ulitatuliwa hatua kwa hatua. Niliona kuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa kweli lina kazi ya Roho Mtakatifu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi! Kilichonifurahisha hata zaidi ni kwamba, siku ya tatu baada ya kujiunga na kanisa hilo, nilimwona yule dada aliyekuwa ameigiza wimbo wa sifa kwenye jukwaa wakati wa Krismasi mnamo mwaka wa 2016. Alikuwa pia amekubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Ninamshukuru Mungu kwa kweli, kwa kuwa ilikuwa mwongozo na nuru ya Mungu ambayo ilituongoza kuendelea kwa mwendo sawa na nyayo za Mwanakondoo, ambayo ilituongoza kufika nchi nzuri ya Kanaani kutoka nyikani na kurudi kwenye nyumba ya Mungu, na ambayo ilituongoza kufurahia neema na ruzuku ya maneno ya Mungu ya uzima pamoja na Yeye!

Nafikiri kwamba ilikuwa kwa sababu ya wema maalum kutoka kwa Mungu kwamba niliweza kurudi katika nyumba ya Mungu. Kwa kuzingatia asili yangu ya uasi, ningewezaje kukaribisha kurudi kwa Bwana bila uongozi na mwongozo wa Mungu au uvumilivu wa akina ndugu katika kufanya ushirika wa neno la Mungu kwangu? Upendo wa Mungu kwangu kwa kweli ni mkubwa sana kiasi kwamba ninauona kuwa mgumu kueleza! Nataka tu kuimba sifa yangu kwa Mungu kupitia nyimbo na kumfuata Mwenyezi Mungu kwa njia imara!

Inayofuata: Kukutana na Bwana Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nimeunganishwa Tena na Bwana

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo...

Sikiliza! Ni Nani Huyu Anenaye?

Na Zhou Li, ChinaKama mhubiri wa kanisa, hakuna jambo linaloumiza zaidi kama udhaifu wa kiroho na kutokuwa na lolote la kuhubiri. Nilihisi...

Kufichua Fumbo la Hukumu

Na Enhui, MalasiaJina langu ni Enhui; nina umri wa miaka 46. Ninaishi Malaysia, nami nimekuwa mwumini katika Bwana kwa miaka 27. Mnamo...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp