945 Ishara ya Hasira ya Mungu

1 Tabia ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya asili. Haibadiliki kamwe na kupita kwa muda, wala haibadiliki kila wakati mahali panapobadilika. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Haijalishi ni nani anayetekelezea kazi Yake, hali Yake halisi haibadiliki, na wala tabia ya haki Yake pia. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika hali Yake halisi au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake.

2 Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anampima ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapojaribu kila mara ghadhabu ya Mungu—na ndio maana pia dhambi huongezeka—hasira ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 944 Mungu Aendeleza Kuwepo kwa Mwanadamu kwa Tabia Yake ya Haki

Inayofuata: 946 Hasira ya Mungu ni Onyesho la Tabia Yake ya Haki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp