280 Mungu Ndiye Mkuu wa Pekee wa Majaliwa ya Mwanadamu
1 Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari inayosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na kuyamakinikia, ukubali hoja kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kutimiza ukweli, ndiyo maisha ya kila siku na mafunzo ya kimsingi ya kumjua Mungu ambayo kila mmoja anakabiliana nayo, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa.
2 Kama mmoja wenu angependa kuchukua njia za mkato ili kufikia shabaha hii, basi Ninakuambia, hilo haliwezekani! Kama mmoja wenu anataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuishinda. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi kipi, mtu hawezi kuathiri, sikwambii kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Yule Mungu Mwenyewe wa kipekee ndiye Anayeweza kuamuru tu mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili