26 Imba Sifa za Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

1

Wewe ndiye Mungu mmoja wa kweli ambaye ameonekana katika mwili,

Mwokozi ambaye amekuja kwa utukufu.

Wewe ndiye Mungu mmoja wa kweli ambaye amefanya kazi daima

kwa ajili ya wokovu wa binadamu.

Umekuwa ukiwaongoza binadamu hadi leo.

Ili kuwasafisha na kuwaokoa kabisa,

Umepata mwili mara mbili!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

2

Umepitia mateso na machungu mengi.

Umevumilia dhihaka kubwa na kukataliwa na enzi hii mbovu.

Gharama ambayo umelipa kwa damu, jasho na machozi Yako

imeonyesha kikamilifu upendo Wako kwa wanadamu kwa kila njia.

Mapenzi Yako na utakatifu Wako vinafichuliwa kwetu.

Tabia Yako iliyo ya haki,

yote imefichuliwa kwetu!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Daraja

Wewe unapendeza sana, Unastahili sifa ya milele.

Tunafurahia sana upendo Wako, tunataka tu kuulipa.

Mwenyezi Mungu, tunakupenda na kuimba sifa Zako daima!

Tabia Yako ya haki inapata nyimbo na dansi zetu za sifa!

Acha tuonyeshe upendo na shukrani zetu Kwako!

3

Unaonyesha ukweli, ukitunyunyizia kwa maneno Yako,

ili tuweze kuishi katika uwepo Wako.

Umemwaga ukweli wa uzima ulimwenguni,

ili Uweze, Uweze kutuokoa!

Baada ya kutenda maneno Yako,

tunakua katika maisha yetu, tunaelewa ukweli.

Maneno Yako huhukumu na kutakasa upotovu wetu,

na tunakuwa wanadamu wapya!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

4

Umerejesha maisha ya kawaida ya binadamu,

ukituleta katika hatima nzuri.

Umemshinda Shetani na

kutuokoa kikamilifu na kupata utukufu wote!

Tukiisifu hekima Yako, tutakukuza daima, tutakutukuza!

Tukisifu uweza Wako, tutakushuhudia!

Tutacheza na kuimba katika sifa Zako!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye kupendeka,

tunaimba sifa, tunaimba sifa Zako milele!

Iliyotangulia: 25 Tunamsifu na Kumwimbia Mungu

Inayofuata: 27 Ni Mwenyezi Mungu Anayetuokoa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp