953 Tukio la Ghadhabu ya Mungu
Mungu anapoachilia ghadhabu Yake kuu, ulimwengu mzima utapitia maafa ya kila aina kama matokeo, kama vile volkano kufoka. Ninaposimama juu kabisa ya angani, inaweza kuonekana kuwa duniani, maafa ya aina mbalimbali yanawakaribia wanadamu wote, yakikaribia kila siku. Nikiangalia chini kutoka juu, dunia inaonyesha mandhari mbalimbali kama yale yanayotangulia tetemeko la ardhi. Moto unaotiririka unasonga bila kupingwa, lava inatiririka kwa uhuru, milima inasonga, na mwanga wa baridi unametameta juu ya kila kitu. Dunia nzima imezama katika moto. Haya ndiyo mandhari ya Mungu akitoa ghadhabu Yake, na pia ndio wakati wa hukumu Yake. Wale wote ambao ni wa damu na nyama hawataweza kutoroka. Hivyo, vita kati ya nchi na migogoro kati ya watu havitahitajika kuharibu ulimwengu mzima; badala yake, dunia “itafurahia yenyewe kwa kufahamu” katika chanzo cha kuadibu kwa Mungu. Hakuna mtu atakayeweza kuiepuka; kila mtu atapitia katika mateso haya.
Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 18” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili