236 Mwishowe Naishi Kwa Kudhihirisha Mfano wa Bibinadamu
1 Nikiwa nimeloweka katika ushawishi wa dunia, niliishi maisha ya uwongo na kujifanya. Nilikuwa mwangalifu sana na wengine, sikusema kamwe neno la kweli kwa urahisi. Nilitenda kwa falsafa za maisha, nikiwa mjanja nikijiamini kuwa mzuri. Niliridhisha kiburi changu lakini sikuweza kuficha uovu moyoni mwangu. Maneno ya Mungu yanahukumu na kufunua asili ya kishetani ya binadamu. Kama kuamka ndotoni, nilijua kuwa sikuwa naishi kama mwanadamu. Uongo, uovu na udanganyifu vikawa maisha yangu. Bila moyo mwaminifu, mzuri, kuna heshima au uadilifu gani? Watu wadanganyifu ni mashetani ambao lazima waondolewe na kutupwa na Mungu. Nachukia kwamba sina ubinadamu, naamua kujifanya upya.
2 Mungu ni mwaminifu na mwenye haki katika kiini na Yeye huchunguza vyote. Udanganyifu wa mwanadamu hauwezi kuepuka macho ya Mungu, hatimaye utafunuliwa. Watu waaminifu wanapenda ukweli na wana baraka na ulinzi wa Mungu. Ninapoelewa ukweli, naondoa barakoa yangu na kutafuta kuwa mtu mwaminifu. Kwa ufupi na wazi, najichangua na kujiweka wazi, na siogopi kuchekwa. Nina usawa katika usemi wangu, sitegemei mhemko na bila najisi ya nia. Sina udanganyifu mbele za Mungu na natoa moyo wangu Kwake. Natekeleza wajibu wangu kwa uaminifu, siulizi chochote kama malipo, ila kumridhisha Mungu. Moyo wangu uko huru na starehe ninapojiendesha kulingana na ukweli. Kuwa mtu mwaminifu na kuishi katika nuru ni maisha ya kweli ya binadamu. Kumtukuza Mungu na kuishi kulingana na maneno ya Mungu, sasa nina uadilifu na heshima. Maneno ya Mungu yamenitakasa, yakiniruhusu niishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.