Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

165 Ushuhuda wa Maisha

I

Siku moja huenda nikakamatwa kwa ajili ya kumshuhudia Mungu,

kuteseka huku ni kwa ajili ya haki,

ambayo najua moyoni mwangu.

Maisha yangu yakitoweka mara moja ghafla bin vu,

Bado nitakuwa na fahari kuwa naweza kumfuata Kristo

na kumshuhudia katika maisha haya.

Ikiwa siwezi kuona tukio kuu la ukuaji wa injili ya ufalme,

bado nitatoa matarajio mazuri zaidi.

Ikiwa siwezi kuiona siku ambayo ufalme unafanikishwa,

lakini naweza kumwaibisha Shetani leo,

basi moyo wangu utajawa na furaha na amani.

Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani,

mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu.

Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki.

Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia.

Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.

II

Siku moja nikiwa mfia dini, na nisiweze tena kumtolea Mungu ushuhuda,

injili ya ufalme bado itaenezwa kama moto

wa nyikani na watakatifu wasiohesabika.

Ingawa sijui naweza kuitembea njia hii yenye mabonde kwa umbali gani,

bado nitamshuhudia Mungu na nitautoa moyo wangu unaompenda Mungu.

Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani,

mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu.

Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki.

Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia.

Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.

III

Nina heshima kujitolea katika kumtangaza na kumshuhudia Kristo.

Kila ninachotaka kufanya ni kutekeleza mapenzi ya Mungu

na kushuhudia kuonekana na kazi ya Kristo.

Bila kutatizwa na dhiki,

kama dhahabu safi iliyotengeneza katika tanuu,

kutoka kwa ushawishi wa Shetani kunaibuka kikundi cha askari washindi.

Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani,

mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu.

Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki.

Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia.

Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.

Iliyotangulia:Sisi ni Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho

Inayofuata:Kutembea kwenye Njia ya Kumpenda Mungu

Maudhui Yanayohusiana