994 Mungu Anawaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi ya Maisha

1 Leo wote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia katika enzi nyingine, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuvuka mipaka ya enzi hii ya kale ya giza, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, ili kila mtu aweze kuishi katika ulimwengu wa uhuru. Kwa ajili ya kesho ya kupendeza, ili kwamba watu wawe wakakamavu katika hatua zao kesho, Roho wa Mungu anapanga kila kitu kwa ajili ya mwanadamu.

2 Na ili mwanadamu aweze kuwa na furaha kubwa zaidi, Mungu anajitolea jitihada Zake zote katika mwili Akiandaa njia mbele ya mwanadamu, ili siku ambayo mwanadamu anaitamani sana iweze kuja haraka. Nyote mngeweza kufurahia wakati huu mzuri; si tendo rahisi kufanya mkutano na Mungu. Ingawa hamjawahi kumjua, tayari mmekuwa pamoja naye tangu kitambo. Laiti kila mtu angeweza kukumbuka milele siku zote hizi nzuri lakini fupi, na kuzifanya kuwa mambo yao ya kuwafurahisha duniani.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (5)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 993 Unapaswa Kuthamini Siku ya Utukufu wa Mungu

Inayofuata: 995 Lazima Uthamini Baraka za Leo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp