35. Baada ya Kukubali Wokovu wa Mungu katika Siku za Mwisho, Tunapokea Uzima Mpya

Na Zhui Qiu, Malasia

Mimi ni mrembeshaji na mume wangu ni mkulima; tulikutana nchini Malaysia katika hafla ya kurusha machungwa, shughuli ya desturi kwa wanawake wanaojaribu kupata wapenzi. Harusi yetu, iliyoshuhudiwa na mchungaji, ilifanyika kanisani mwaka mmoja baadaye. Niliguswa sana na ombi la mchungaji kwa ndoa yetu na ingawa sikuwa wa dini, nilimsihi Mungu kimoyomoyo: “Mtu huyu na anitunze na kunishughulikia kwa upendo thabiti, na awe mwandani wangu katika maisha yangu yote.”

Baada ya kuanza maisha ya ndoa, ugomvi kati yangu na mume wangu uliibuka mmoja baada ya mwingine. Angeondoka nyumbani ifikapo saa 10 kila asubuhi kuuza mboga na hangerudi hadi baada ya saa 1 jioni, lakini sikuto kakazini hadi baada ya saa 4 jioni. Tulikuwa na wakati mdogo sana pamoja. Kila wakati nilipoukokota mwili wangu kurudi nyumbani, nilikuwa nikitumaini sana kupokea kiasi fulani cha usaidizi, utunzaji, naufahamu wa mume wangu; nilimtaka aniulize jinsi kazi ilivyokuwa imeendelea, ikiwa nilikuwa na furaha au la. Lakini kwa masikitiko yangu, kila nilipokuja kutoka kazini, kama hakuwa akitazama runinga alikuwa akichezacheza na simu yake, na wakati mwingine hata hangeshughulika kunisalimia. Ilikuwa tu kana kwamba hata sikuwepo. Jambo hili liliniacha nikiwa mwenye huzuni na nilianza kutoridhika na mume wangu polepole.

Wakati mmoja nilikuwa na ugomvi na mteja fulani na nilikuwa nikihisi kukasirishwa sana na kukosewa sana. Baada ya kufika nyumbani nilimweleza mume wangu kuhusu jambo hilo bila woga nikitumai kuwa angenifariji, lakini kwa mshangao wangu, huku akicheza kwenye simu yake alinitambua kwa shida, akisikiliza kwa makini kidogo tu. Kisha aliinamisha kichwa chake na kurudi moja kwa moja kwenye simu yake. Kutonijali kwake kabisa kulikuwa kwa kufadhaisha sana, kwa hivyo nilimfikia na kusema kwa sauti kubwa, “Umeumbwa kwa jiwe? Huwezi hata kuzungumza? Je, unamjali mtu yeyote?” Aliponiona nikiwa mwenye hamaki sana, alikataa kujibu. Kadiri nilivyozidi kunyamaziwa, ndivyo hasira yangu ilivyozidi kuongezeka. Nilimsumbua na kumsumbua, nikiazimia kabisa kumpa hoja ilikumshawishi. Bila kutarajia, alijibu kwa kunifokea kwa ghafla, “Je, si tayari umesema ya kutosha?” Jambo hili lilinifanya nihisi kughadhabika hata zaidi, na kukosewa hata zaidi, kwa hivyo niliendelea kujaribu kumpa hoja ili kumshawishi. Mwishowe, alikataa tu kusema chochote, kwa hivyo mabishano yetu yaliisha tu. Kuna wakati mwingine ambapo nilimlalamikia mume wangu kuhusu kitu ambacho kilinifadhaisha kazini nikidhani kwamba angejaribu kunifanya nihisi vizuri zaidi, lakini badala yake alijibu kwa ghaflana kwa dharau, “Ugomvi huhusisha watu wawili. Unachoona tu ni matatizo ya watu wengine—kwa nini hujiangalii?” Hasira yangu ililipuka mara moja na sikuweza kujizuia kumpa ukweli. Huku nikijawa na chuki, niliwaza, “Yeye ni mtu wa namna gani? Kwa nini niliolewa na mtu kama yeye? Hazingatii hisia zangu hata kidogo—hana hata neno moja la faraja kwangu!” Kuanzia wakati huo na kuendelea karibu niache kabisa kushiriki naye kilichojiri kazini. Wakati fulani baadaye alijaribu kuniuliza kuhusu kazi yangu, lakini sikuhisi kamwe kusikiliza alichokuwa akisema.Aliacha kuniuliza kuhusu chochote pole pole. Tulikuja kuwa na mada chache zaidi na zaidi ya mazungumzo ya pamoja na wakati wowote kitu cha kufadhaisha kilipojiri ningeenda tu kumtafuta rafiki wa kunisikiliza. Wakati mwingine ningekaa nje hadi baadaye na singefika nyumbani hadi baada ya saa sita usiku. Hata nilipofika nyumbani nikiwa nimechelewa sana, bado hakuonekana kujali lakini alisema tu kuwa nilikuwa nikichukulia nyumba yetu kama hoteli. Nilihisi kufadhaishwa sana, na kutoridhika kwangu na mume wangu kuliongezeka, ikitusababisha tubishanebishane na kugombana mara nyingi sana. Sote wawili tulikuwa tukiteseka. Sikutaka mambo yaendelee kwa njia hiyo, kwa hivyo niliamua kutafuta nafasi ya kuzungumza naye vizuri.

Siku moja baada dhifa, nilimuuliza, “Kwa kweli huwezi kunivumilia, siyo? Je, kwa nini kila wakati hunisikilizi? Ikiwa una tatizo nami, niambie tu moja kwa moja.” Alipokosa kusema chochote kwa kujibu, niliendelea tu kumsumbua kwa malalamiko. Jambo la kushangaza ni kwamba, alinifokea kwa hasira, “Acha kuniuliza maswali haya yote! Kila kitu ni tatizo kwa sababu yako—nimechoshwa na jambo hilo!” Kupata jibu la aina hiyo kutoka kwake kuliamsha hasira yangu mwenyewe, na tulianza kubishana tena, tukijibizana.Jambo hili liliendelea kwa muda hadi alipoinuka na kunipiga kikumbo; niliteleza na kuanguka na kujipata kwenye sofa. Kuona kwamba mume wangu angenipiga kulikuwa jambo la kuhuzunisha kabisa. Niliwaza, “Huyu ndiye mume niliyemchagua kwa makini sana? Hii ndiyo ndoa ambayo nilikuwa na matumaini sana nayo? Angewezaje kunitendea hivi?” Kuanzia wakati huo sikuwa na matumaini yeyote kwake tena.

Mnamo Aprili mwaka wa 2016, kwa bahati nasibu, dada mmoja alishiriki injili ya Bwana Yesu nami. Alisema kuwa Bwana anatupenda na alipigiliwa misumari msalabani ili atuokoe. Niliguswa sana na upendo Wake, na kwa hivyo nilikubali injili ya Bwana. Nilipozungumza na mchungaji wangu baadaye kuhusu matatizo yaliyokuwa katika ndoa yangu, aliniambia, “Hatuwezi kumbadilisha mtu mwingine yeyote isipokuwa tu tujibadilishe wenyewe kwanza. Tunapaswa kufuata mfano wa Bwana Yesu na kutekeleza stahamala na uvumilivu kwa wengine.” Kwa hivyo, nilianza kujaribu kujibadilisha. Ningeenda nyumbani mara tu nilipotoka kazini na kusafisha nyumba sana, na wakati mwingine mume wangu aliponipuuza na nilikaribia kukasirika, ningemwomba Bwana, nikimsihi Anipe stahamala na uvumilivu. Nyakati ambazo singeweza kujizuia na kuanza kugombana na mume wangu, baada ya ugomvi kutendeka ningejaribu kujitahidi kuwa wa kwanza kurahisisha mambo. Mume wangu alipoona mabadiliko ambayo yalikuwa yamefanyika kwangu, alianza pia kumwamini Bwana. Mara sote tulipokuwa waumini, tulibishana mara chache na kuwasiliana zaidi. Nilijawa na shukrani nyingi kwa Bwana baada ya kuona wokovu Wake binafsi kwetu.

Lakini muda ulizidi kupita, na bado tulibaki wasioweza kudhibiti hali zetu wenyewe za moyo. Ugomvi wa nyumbani bado ungezuka wakati mwingine, na hasa mtu mwingine alipokuwa na hali mbaya ya moyo hakuna mmoja wetu aliyeweza kutekeleza stahamala na uvumilivu, kwa hivyo matokea ni kwamba ugomvi wetu ulizidi kuwa mkali zaidi na zaidi. Moyo wangu ulisumbuliwa na uchungu baada ya kila ugomvi, na ningemwomba Bwana, “Bwana, Unatufundisha tuwe wavumilivu na wenye subira, lakini inaonekana tu kuwa siwezi kufanya hivyo. Ninapomwona mume wangu akifanya kitu ambacho sikipendi mimi huhisi kutoridhika naye sana. Bwana, ninapaswa kufanya nini?” Baadaye nilianza kwenda katika kila darasa lililoandaliwa na kanisa nikitumaini kupata njia ya utendaji, lakini sikupata kile nilichokuwa nikitarajia kutoka kwa jambo hilo. Niliomba usaidizi kutoka kwa kiongozi wa kikundi chetu, ambaye alisema tu, “Mimi na mke wangu hubishana mara nyingi pia. Hata Paulo alisema, ‘Kwani najua kwamba ndani yangu (yaani, ndani ya mwili wangu) hakuna jambo zuri: kwani kutaka kuko ndani yangu, lakini jinsi ya kutenda lile lililo zuri sipati’ (Warumi 7:18). Hakuna yeyote aliye na suluhisho la tatizo tunalokumbana nalo la mafuatano ya kutenda dhambi na kukiri kila mara. Tunachoweza tu kufanya ni kumwomba Bwana na kuomba rehema Yake.” Kusikia akisema haya kulinicha nikihisi kuchanganyikiwa: Je, inawezekana kwamba tuliandikiwa kutumia maisha yetu yote tukiwa tumekwama katika ugomvi?

Mnamo Machi mwaka wa 2017, mume wangu, ambaye alikuwa mnyamavu wakati wote, alibadilika ghafla kuwa mtu mchangamfu anayejua sana kuzungumza. Na mara nyingi angeshiriki ushirika nami kuhusuufahamu wake wa maandiko, na kilichonishangaza hata zaidi ni kwamba alichoshiriki katika ushirika kilikuwa kimejawa na nuru sana. Nilikanganywa; ilikuwa kana kwamba alikuwa ghafla amekuwa mtu tofauti, na mambo aliyokuwa akisema yalikuwa yenye utambuzi sana. Nilitaka sana kujua kilichokuwa kikiendelea. Siku moja niligundua kwa bahati kuwa alikuwa mshiriki wa kikundi katika programu ya mtandao wa kijamii, na bila kukawia nilimuuliza alichokuwa akizungumza nao kuhusu. Huku uso wake ukionyesha kutofanya mazaha, aliniambia kwamba alikuwa akifikiria kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwamba Bwana Yesu alikuwa tayari amerudi na jina Lake lilikuwa Mwenyezi Mungu. Alisema kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa tayari ametamka maneno mengi sana na alikuwa akifanya kazi ya hukumu na utakaso wa wanadamu katika siku za mwisho. Alisema pia kwamba jambo hilo lilitimiza unabii huu wa Biblia: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Mume wangu aliniambia kwamba tunapotafuta kuonekana kwa Mungu na kazi Yake, tunapaswa kulenga kusikia sauti ya Mungu badala ya kushikilia tu maoni na mawazo yetu pasipo kufikiria. Tusipotafuta ukweli ila tusubiri tu ufunuo wa Mungu kwa kukaa tu, hatutaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana. Kusikia jambo hili kulinitia bumbuazi na lilionekana kuwa jambo lisilofahamika. Baadaye wazo lilinijia kwamba wakati fulani nilikuwa nimemsikia mchungaji mmoja Mhindi akisema kwamba tukiwahi kusikia chochote kuhusu kurudi kwa Bwana, tunapaswa kutafuta kwa dhati na kuchunguza jambo hilo kwa bidii; hatungeweza kutegemea maoni na mawazo yetu na kutoa hukumu tu pasipo kufikiria. Kwa hivyo nilimwomba Bwana: “Bwana, ikiwa Mwenyezi Mungu kwa kweli ni kurudi Kwako, tafadhali niongoze na Unielekeze ili niweze kutafuta ukweli na kuchunguza jambo hili kwa dhati. Vinginevyo, tafadhali linda moyo wangu ili nisipotee kutoka Kwako. Amina!”

Nilifungua Biblia baada ya ombi hili na kuona haya katika Ufunuo 3:20: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi.” Nilikuwa na muda mfupi wa ghafla wa msukumo na nilihisi kuwa ni Bwana aliyekuwa akinizungumzia, Akiniambia kwamba atakaporudi, Atabisha mlango wangu; nilihisi huyu Alikuwa Yeye akiniamuru nisikilize sauti Yake na niufungue mlango. Ilikuwa tu kama wale mabikira wenye busara katika Biblia ambao waliharakisha kumkaribisha bwana harusi waliposikia sauti yake. Kisha niliwaza kuhusu Yohana 16:12-13: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo.” Nilipokuwa nikitafakari aya hizi za Maandiko, hisia za msisimko zilibubujika ndani yangu. Niligundua kuwa Bwana alikuwa ametuambia hapo zamani kwamba atakaporudi atanena maneno mengi zaidi na kutupa ukweli. Na kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ni kazi ya kuonyesha maneno ili kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu—je, inaweza kwamba Mwenyezi Mungu kwa kweli ndiye Bwana Yesu aliyerudi? Ikiwa kwa kweli Bwana amerudi na ameonyesha ukweli ili kusuluhisha matatizo yote ya wanadamu, basi kuna tumaini kwetu kutoroka minyororo ya dhambi. Basi je, matatizo kati yangu na mume wangu hayangeweza kutatuliwa? Sikupoteza muda kumuuliza mume wangu anisaidie kuwasiliana na ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu; nilitaka kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho pia.

Nilipokuwa katika mkutano mmoja, baadhi ya ndugu kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu walichagua aya kadhaa za Biblia ili kushiriki nami juu ya vipengele mbalimbali vya kweli kama vile namna ya kurudi kwa Bwana, jina jipya la Bwana, na ni kazi gani atakayofanya. Ushirika wao ulikuwa wa kusadikisha sana na mpya kabisa kwangu. Nilitaka sana kujua mengi zaidi kuhusu kazi ya Bwana ya siku za mwisho, kwa hivyo nilimwomba Mungu tena na tena, nikimsihi Anipe nuru ili kwamba niweze kuelewa maneno ya Mungu. Kwa kusoma maneno ya Mungu na kusikiliza ushirika wa ndugu hao, nilipataufahamu wa kusudi la Mungu katika usimamizi Wake wa wanadamu pole pole, hatua Zake tatu za kazi ya kuwaokoa wanadamu, na matokeo na hatima ya binadamu.Nilipokuwa nikichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, bado sikuweza kujizuia kubishanabishana na mume wangu juu ya vitu vidogo vidogo. Baada ya jambo hilo kutendeka, ningehisi mwenye hatia na kufadhaishwa sana, na ningejiuliza, “Kwa nini siwezi kamwe kutia maneno ya Mungu katika vitendo?” Jambo hili liliniacha nikiwa nimekanganyikiwa. Katika mkutano wakati mmoja, nilimuuliza dada fulani, “Je, kwa nini mimi na mume wangu hugombana kila wakati? Kwa nini hatuwezi kupatana kwa amani?” Alinitafutia vifungu kadhaa vya maneno ya Mungu. “Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Kisha alishiriki ushirika huu: “Hapo mwanzo, Adamu na Hawa waliishi kwa furaha mbele za Mungu katika bustani ya Edeni. Hakukuwa na mabishano; hakukuwa na mateso. Lakini baada ya kumsikiliza Ibilisi na kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, walianza kujitenga na Mungu na kumsaliti, wakipoteza utunzaji na ulinzi wa Mungu na kuishi chini ya nguvu za Shetani. Siku za huzuni na mateso kisha zikaanza. Imekuwa hivi hadi sasa, na tumepotoshwa na Shetani zaidi na zaidi. Tumejawa na tabia potovu, za shetani; sote ni wenye kiburi, wabinafsi, wadanganyifu, na wakaidi sana. Sisi ni wenye kujipenda katika mambo yote, kila wakati tuwakitaka wengine watusikilize. Hiyo ndiyo sababu watu hupigana na kuuana. Hata wazazi na watoto na waume na wake hawastahimiliani na kuvumiliana na hawawezi kuelewana kwa upatanifu—hatuna hata dhamiri na mantiki ya msingi zaidi. Ingawa tumekombolewa na Bwana Yesu, ingawa sisi humwomba Bwana, hukiri, na kutubu, na tunafanya bidii kufuata mafundisho ya Bwana, bado hatuwezi tu kujizuia kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Hiyo ni kwa sababu Bwana Yesu alitekeleza kazi ya kuwakomboa wanadamu tu; hakufanya kazi ya kuwaokoa na kuwatakasa wanadamu kikamilifu. Kukubali wokovu wa Bwana Yesu kunamaanisha tu kuwa sisi sio wa dhambi tena na tuna fursa ya kuja mbele za Bwana katika sala, kupokea rehema Yake, na kusamehewa dhambi zetu. Hata hivyo, hatujatakaswa kutokana na tabia zetu potovu. Asili zetu za dhambi bado zimekita mizizi ndani yetu; bado tunahitaji Mungu arudi katika siku za mwisho na kufanya hatua ya kazi ya kuwatakasa na kuwabadilisha wanadamu, hivyo kusuluhisha tatizo la asili zetu za dhambi. Na sasa Mungu amepata mwili kwa mara nyingine tena, Akionyesha maneno ya kufanya kazi ya hukumu na utakaso ili kutuokoa kikamilifu kutoka kwa tabia zetu potovu na kutuwezesha kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuokolewa kabisa. Mradi tuendelee sawa na kazi mpya ya Mungu, tukubali hukumu na kuadibu kwa maneno Yake, tutafute kweli, na kutia maneno ya Mungu kwa vitendo, tabia zetu potovu zitabadilishwa pole pole. Hivyo tu ndivyo tutakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu, na ndipo tu tutakapoweza kufanikisha upatanifu katika mwingiliano wetu na wengine.”

Mwishowe niligundua kutoka kwa maneno ya Mungu na ushirika wa dada huyu kwamba sababu kwambatulikuwa tukiishi siku zote katika hali hii ya kutenda dhambi na kisha kukiri ilikuwa ni kwa sababu ingawa Bwana Yesu alikuwa amefanya kazi ya kuwakomboa wanadamu, dhambi zetu kama waumini zilisamehewa tu; asili yetu ya ndani yenye dhambi, hata hivyo, ilikuwa bado madhubuti sana na tabia zetu za shetani bado hazikuwa zimetakaswa. Mfano mzuri kabisa ni jinsi nilivyokusudia kutekeleza stahamala na uvumilivu kulingana na mafundisho ya Bwana, lakini mara mume wangu aliposema au kufanya kitu ambacho sikukipenda, singeweza kujizuia kughadhabika. Sikuweza tu kujidhibiti tena bila kujali chochote. Bila kazi ya Mungu ya kutuokoa, haiwezekani kwetu kutupilia mbali tabia zetu za shetani, potovu tukitegemea juhudi zetu wenyewe. Na sasa, Mungu amepata mwili tena, akija kufanya kazi ya kuhuwahukumu na kuwatakasa wanadamu. Kwa kukubali kazi mpya ya Mungu na kuifuatilia sana ukweli, tuna nafasi ya kufanikisha mabadiliko ya tabia. Nilihisi kuguswa sana na mwenye shukrani sana kwa ajili ya rehema ya Bwana ambayo ilikuwa imeniwezesha kusikia sauti Yake. Lakini bado sikuwa bila shaka kabisa—nilijua kuwa Mungu alikuwa amekuja wakati huu kutamka maneno ya kututakasa na kutubadilisha, lakini je, maneno yanawezaje kuihukumu na kuitakasa tabia yetu potovu? Kwa hivyo, nilieleza mkanganyiko wangu.

Dada huyo alinisomea kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Aliendelea kushiriki ushirika zaidi nami. “Maneno ya Mungu yanatueleza waziwazi jinsi anavyofanya kazi ya hukumu. Yeye hutumia maneno kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu; kimsingi Yeye hutumia maneno kufichua na kuchangua moja kwa moja asili yetu na nafsi yetu potovu na tabia yetu ya shetani. Pia ametuambia waziwazi jinsi ambavyo tunapaswa kumtii na kumwabudu Mungu, jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu sahihi, jinsi ya kufuatilia ukweli ili kufanikisha mabadiliko ya tabia, jinsi ya kuwa mtu mwaminifu, na mapenzi ya Mungu na mahitaji yake kwa watu ni gani. Ametuambia ni watu wa aina gani anaowapenda na ni watu wa aina gani anaowaondoa, na zaidi. Pia huweka mahala watu, hafla, vitu, na mazingira ili kutupogoa na kutushughulikia, kutujaribu na kutusafisha. Hii huweka wazi tabia zetu potovu na kutulazimisha kuja mbele za Mungu na kutafuta ukweli, kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno Yake, na kutafakari na kujijua. Tunapokubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, tunahisi kana kwamba anazungumza nasi, uso kwa uso, waziwazi, Akifichua kabisa uasi na upinzani wetu Kwake, nia zetu zisizo sahihi, na fikra zetu na mawazo yetu. Ni wakati huo tu ndipo tunaweza kuona kwamba asili na nafsi zetu zimejawa na kiburi, majivuno, udanganyifu, upotovu, ubinafsi, na uovu. Tunaona kwamba tunakosa kabisa mioyo ya kumcha Mungu na kwamba tunaishi tu kulingana na asili zetu za shetani, potovu, na kwamba tunachofichua tu ni tabia yetu ya shetani, na kwamba tunakosa kabisa ufanani wa binadamu. Tunaanza kujichukia na kuchukizwa nasi wenyewe kutoka ndani ya mioyo yetu na kutotaka kuishi tena chini ya ushawishi wa Shetani, na kuchezewachezewa na kuumizwa na Shetani. Zaidi ya hayo, kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu tunaona nafsi takatifu ya Mungu na tabia Yake ya haki isiyovumilia dhambi. Moyo wa kumcha Mungu huzuka ndani yetu na tunakuwa tayari kutia ukweli katika vitendo ili kumridhisha Mungu. Mara tunapoanza kutenda ukweli, tabia ya Mungu ya kukirimu na yenye rehema huonekana kwetu. Kwa kusoma maneno ya Mungu kwa mfulizo na kupitia hukumu na kuadibu Kwake, tunapata ufahamu wa kina zaidi kuhusu asili zetu potovu, tunaelewa bora ukweli ulioonyeshwa na Mungu, na hata kuwa tayari zaidi kukubali na kujisalimisha kwa hukumu na kuadibu Kwake, na kuacha mwili, kutia ukweli katika vitendo, na kumridhisha Mungu. Tunafichua upotovu mchache na mchache, kutenda ukweli kunazidi kuwa rahisi na rahisi, na tunachukua njia ya kumcha Mungu na kuepukana na uovu pole pole. Kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, sote tunaweza kudhibitisha kutoka mioyoni mwetu kwamba hii ndiyo suluhisho ambayo inatuokoa na kutuondolea tabia zetu potovu. Huu ni upendo wa kweli kabisa wa Mungu kwetu wanadamu potovu, na bila kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, kamwe hatutaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu.”

Maneno ya Mungu na ushirika wa dada huyo yalikuwa na athari kubwa kwangu. Nilihisi kuwa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho ni ya vitendo sana, na kwamba ikiwa tunataka tabia zetu potovu zibadilishwe, lazima tupitie hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu. Vinginevyo, tutaishi milele katika mafuatano ya kutenda dhambi na kisha kukiri, na hatutaweza kamwe kutoroka minyororo ya dhambi. Kwa hivyo nilimwomba Mungu moyoni mwangu, nikimsihi Aninyunyizie na kunilisha kwa maneno Yake, na kuandaa mazingira ya kunihukumu na kuniadibu ili niweze kujijua, tabia yangu potovu ingeweza kubadilishwa siku moja, na ningeweza kuishi nikidhihirisha mfano wa kweli wa binadamu.

Baada ya kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho pia nilipataufahamu mpya kuhusu ndoa ambayo Mungu alikuwa amenipangia. Wakati mmoja dada fulani alinisomea vifungu vya maneno ya Mungu. “Watu huwa na picha nyingi kuhusu ndoa kabla ya kuipitia wao wenyewe, na picha hizi zote ni nzuri. Wanawake hufikiria kwamba waume wao watakuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, nao wanaume hufikiria kwamba wataweza kuoa Binti wa Kifalme Anayependeza. Kubuni huku kwa mawazo kunaonyesha kwamba kila mtu anayo mahitaji fulani ya ndoa, orodha fulani ya kile anachohitaji na viwango anavyopenda(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III). “Ndoa ni awamu muhimu katika maisha ya mtu. Ni zao la hatima ya mtu, kiungo muhimu katika hatima ya mtu; haiundwi kwa misingi ya uamuzi wa mtu yeyote binafsi au mapendeleo yake, na haiathiriwi na mambo yoyote ya nje, lakini inaamuliwa kabisa na hatima za wandani wawili, kupitia kwa maandalizi na kuamuliwa kabla kwa Muumba kuhusiana na hatima za wanandoa hao(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III). “Kwa hivyo mtu anapoingia kwenye ndoa, safari ya mtu katika maisha itaathiri na kumgusa yule mwenzake, na vilevile safari ya mwandani katika maisha itashawishi na kugusa hatima ya yule mwenzake katika maisha. Kwa maneno mengine, hatima za mwanadamu zimeingiliana na hakuna yule anayeweza kutimiza kazi yake maalum maishani au kutekeleza wajibu wake kabisa akiwa huru mbali na wengine. Kuzaliwa kwa mtu kunao mwelekeo kwa msururu mkubwa wa mahusiano; kukua pia kunahusisha msururu mkubwa wa mahusiano; na vilevile, ndoa inakuwepo bila shaka na kuendelezwa katika mtandao mpana na mgumu wa miunganisho ya binadamu, ikihusisha kila mwanachama na kuathiri hatima ya kila mmoja ambaye ni sehemu yake. Ndoa si mazao ya familia za wanachama wale wawili, hali ambazo wao walilelewa, maumbo yao, umri wao, ubora wao, vipaji vyao, au mambo mengine yoyote; badala yake, inatokana na kazi maalum ya pamoja na hatima inayohusiana. Hii ndiyo asili ya ndoa, zao la hatima ya binadamu lililopangwa na lililopangiliwa na Muumba(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III). Kisha alishiriki ushirika wake nami. “Kila moja ya ndoa zetu iliamuliwa kabla na Mungu, na Mungu hapo zamani aliamua ni nani tungeanzisha familia naye—haya yote yamepangwa kupitia hekima ya Mungu Mwenyewe. Ndoa anayotuchagulia haitegemei hadhi yetu ya kijamii katika jamii, sura zetu, au ubora wetu wa tabia, lakini inategemea wito wa watu wawili. Hata hivyo, tunadhibitiwa na tabia zetu potovu, kwa hivyo daima tuna mahitaji mengi kwa wachumba wetu, daima tukiwataka wafanye vitu kwa mbinu zetu. Wasipofanya hivyo, sisi hukataa kukubali jambo hili na kuhisi wasioridhika; tunabishana nao na kukasirika, au hata kulalamika, na tunamlaumu Mungu na kumwelewa visivyo. Hii inasababisha watu wote wawili waishi na uchungu. Aina hiyo ya uchungu haisababishwi na mtu mwingine yeyote, wala kusababishwa na utawala na utaratibu wa Mungu, lakini hutokea kwa sababu tunaishi kwa tabia zetu zenye kiburi, zenye majivuno na potovu. Aina hiyo ya tabia potovu hututenganisha na utawala wa Mungu; hatuwezi kujisalimisha kwa mipango na utaratibu Wake.”

Niliposikia ushirika wa dada huyu, nilikumbuka kuhusu wakati wa uhusiano wangu na mume wangu. nilikuwa nikionyesha kutoridhishwa naye siku zote na kudai kwamba afanye mambo kwa njia yangu kila wakati—ikiwa hangenikumbuka, kama hangeonyesha kunidhukuru na kunijali, kama hangeulizia afya yangu, ningelalamika juu yake na kufikiria kuwa hakuwa mzuri. Ningemdharau kwa kila njia na kupigana naye vita vya maneno, nikikataa kumkubali. Mwishowe niliona kwamba nilikuwa mtu mwenye kiburi sana, mwenye majivuno, mwenye ubinafsi, na mwenye kustahili dharau. Nilikuwa mtu ambaye alifikiria tu kuhusu masilahi yangu mwenyewe na sikujali hisia za watu wengine. Kwa kufikiria jambo hilo kwa makini, niliona kwamba haikuwa ukweli kabisa kuwa mume wangu hakunijali, ni kwamba tu alikuwa mndani zaidi na hakuwa mwenye kuonyesha hisia sana. Pia alikuwa na maoni na mapendeleo yake mwenyewe, lakini nilisisitiza kumlazimisha afanye vitu ambavyo hakupenda kuvifanya. Kila wakati nilitaka kila kitu alichofanya kinihusishe, na jambo hilo ndilo lilikuwa limesababisha ugomvi mwingi kuzuka kati yetu. Kisha sikuweza kujizuia kujuta kuhusu mwenendo wangu wa zamani. Nilifikiria pia kuhusu yale ambayo mume wangu aliyasema, kwamba hapo zamani, nilikuwa mwenye kushiriki naye injili ya Bwana, lakini sasa alikuwa ameshiriki nami injili ya Mungu ya siku za mwisho. Hii ilikuwa neema kubwa ya Mungu kwetu na utaratibu Wake wa kustaajabisha. Sisi sote ni watu waliobarikiwa sana, lakini sikujua shukrani ya aina yoyote. Badala yake, sikuwa tayari kujisalimisha kwa ndoa ambayo Mungu alikuwa amenipangia, nikimlaumu Mungu kila wakati. Niligundua kwamba nilikuwa mwenye kiburi sana, na bila mantiki kabisa! Namshukuru Mungu kwa kuniongoza kwa maneno Yake. Nilikuwa nimepata chanzo cha mateso yote katika ndoa yangu—nilipata hisia ya utulivu na ukombozi moyoni mwangu. Pia nilikuja kuwa tayari kumwegemea Mungu na kumtegemea Mungu maishani mwangu kuanzia wakati huo, kuacha tabia yangu yenye kiburi, yenye majivuno na upotovu, na kutendana na mume wangu kwa upatanifu.

Tangu wakati huo, mimi na mume wangu tumesoma maneno ya Mungu na kushiriki pamojakuhusu ukweli mara kwa mara, na tunatekeleza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa kwa uwezo wetu wote. Sisi pia tunalishwa na kunyunyiziwa na maneno ya Mungu kila siku; tunapokumbanana tatizosisi hutafuta mapenzi Yake kulingana na maneno Yake. Tukifichua upotovu au kuanza mabishano, sote wawili huja mbele za Mungu, na kutafakari juu ya jambo hilo na kujijua. Tunapotia hayakatika vitendo tunapataufahamu zaidi na kusameheana. Mabishano yetu yamezidi kupungua, maisha yetu ya nyumbani yamekuwa patanifu, na maisha yetu yamezidi kukamilika zaidi na zaidi. Kile ambacho kimekuwa cha kunigusa sana ni kwambaufahamu wa mume wangu kuhusu ukweli ni bora kuliko wangu. Mara nyingi yeyehushiriki ushirika nami juu yaufahamu wake kuhusu maneno ya Mungu, na anaponiona nikifichua tabia potovu, yeye hushiriki nami ushirika kuhusu ukweli na mapenzi ya Mungu. Kwa kweli nimehisi utunzaji na upendo wake kwangu—ninafurahi kutoka moyoni mwangu. Nikikumbuka njia yetu, mimi bado ni mimi, na bado yeye ni yeye; ni kwa sababu tu tumekubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kuelewa ukweli kiasi, kila kitu kimebadilika kabisa. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuokoa!

Iliyotangulia: 34. Uzinduzi wa Kiroho wa Mkristo

Inayofuata: 36. Kurejea kwa Mwana Mpotevu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

43. Kupotea na Kurejea Tena

Na Xieli, MarekaniNilikuja Marekani kufanya kazi kwa bidii kama vile ningeweza kutafuta maisha yenye furaha na hali ya juu ya maisha....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp