529 Usijifurahishe kwa Sababu Mungu ni Mvumilivu

1 Hata kama kuna watu wachache sana wanaonijua, Sitatoa, kwa ajili ya hayo, hasira Yangu kwa binadamu, kwa sababu wanadamu wana dosari nyingi mpaka ni vigumu kwao kufikia kiwango ninachowauliza. Na hivyo Nimekuwa na huruma kwa binadamu kwa maelfu ya miaka, hadi wa leo. Lakini Natumai kwamba hamtakuwa tayari sana, kwa sababu ya huruma Yangu, kujishughulikia wenyewe; mnapaswa badala yake, kupitia Petro, kuja kunijua na kunitaka; kutokana na yale aliyofanya mnafaa kuangaziwa zaidi ya jinsi mlikuwa hapo awali na hivyo kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa na mwanadamu.

2 Kote ulimwenguni na maeneo yasiyo na kikomo ya anga, kati ya vyote vinavyopatikana mbinguni kama ilvyo duniani, vitu vyote lukuki duniani, na mambo lukuki mbinguni yote yanatoa juhudi zote kwa ajili ya ukamilisho wa kazi Yangu. Hakika hamtamani kubakia tu kama watazamaji walio kando, ambao huendeshwa hapa na pale na nguvu za Shetani? Shetani daima anagugumia maarifa ambayo wanadamu wameshikilia kunihusu mioyoni mwao, na daima, kwa meno na makucha wazi, akishiriki kwa maumivu ya mwisho ya mapambano yake ya kifo. Je, unataka kukamatwa na mipango yake danganyifu wakati huu? Unataka, wakati awamu ya mwisho ya kazi Yangu imekamilika, kukata maisha yako mwenyewe? Hakika bado hunisubiri Nisambaze huruma Yangu mara moja tena?

Kutaka kunijua ni jambo muhimu, lakini hupaswi pia kupuuza kuwa makini kwa mazoezi halisi. Nafichua ufahamu kwako moja kwa moja kwa maneno Yangu, kwa matumaini kwamba utaweza kuukubali mwongozo Wangu, na kukoma kuyafikiria matarajio ama miundo yako mwenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 6” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 528 Watu Hawatendi Kabisa Maneno ya Mungu

Inayofuata: 530 Anachochukia Mungu Zaidi ni Ukaidi na Uhalifu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp