918 Mamlaka na Utambulisho wa Muumba- Huishi Pamoja
1 Licha ya kama vilikuwa majini, au mbinguni, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hivi hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishwa na viumbe vyovyote. Havikuwahi kuthubutu kwenda nje ya mipaka viliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaana, na kutii kwa umakinifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa kufahamu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na amri na maagizo ya mbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo.
2 Upekee wa mamlaka ya Muumba ulionyeshwa si tu katika uwezo Wake wa kuumba viumbe vyote na kuamuru viumbe vyote kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na kupatia maisha na nguvu kwa viumbe vyote, na, vilevile, katika uwezo Wake kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu, viumbe vyote ambavyo Angeumba katika mpango Wake ili kuonekana na kuwepo katika ulimwengu ulioumbwa na Yeye kwa umbo timilifu, na kwa muundo wa maisha timilifu, na wajibu timilifu. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo fikira za Muumba hazikutegemea vizuizi vyovyote, hazikuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia vilevile milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili