915 Yote Chini ya Mamlaka ya Muumba ni Mazuri Kabisa

1 Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na uthibitishaji wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya uthibitishaji huu, viumbe vyote visingeweza kufanya chochote kingine ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba.

2 Huku vitendo hivi vya kimiujiza vya Mungu vikijionyesha, ulimwengu huu ulijaa, vipande kwa vipande, ukiwa na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ukabadilika kutoka kwa fujo na giza hadi kwa wazi na uangavu, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwa uchangamfu na nguvu zisizokuwa na mipaka. Miongoni mwa viumbe vyote vya uumbaji, kutoka kwa wale wakubwa hata wadogo, toka kwa wadogo hata kwa wale wadogo zaidi, hakuna hata kiumbe kimoja ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na kukawa na upekee na haja ya ndani kwa ndani na thamani ya uwepo wa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba.

3 Viumbe vyote vilivyo katika mamlaka ya Muumba vitaweza kuchezesha mdundo mpya wa ukuu wa Muumba, vitaanza utangulizi mwema kwa minajili ya kazi Yake kwenye siku mpya, na kwa muda huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria ya mimea ya machipuko, kukomaa kwa kiangazi, mavuno ya mapukutiko, na hifadhi ya kipupwe iliyochaguliwa na Muumba, viumbe hivi vyote vitaweza kutilia mkazo mpango wa usimamizi wa Muumba na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya, na mkondo mpya wa maisha, na hivi karibuni vitu vitaweza kuzaana katika mfululizo usioisha ili kuweza kukaribisha kila siku katika ukuu wa mamlaka ya Muumba …

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 914 Vitu Vyote ni Maonyesho ya Mamlaka ya Muumba

Inayofuata: 916 Mamlaka na Nguvu ya Muumba Havina Mipaka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp