866 Maana ya Kuonekana kwa Mungu Baada ya Kufufuka Kwake
1 Hakutaka kuwaona watu wakimwepuka Yeye au wakijiondoa Kwake yeye; Aliwataka tu watu kumwelewa Yeye, kumkaribia na kuwa familia Yake. Hivyo basi, baada ya kufufuka Kwake, Bwana Yesu bado alijitokeza kwa watu katika umbo Lake la mwili na damu, na kula na kunywa pamoja nao. Mungu huwaona watu kama familia na pia anataka wanadamu kumwona Yeye kwa njia hiyo; ni kwa njia hii tu ndivyo Mungu anavyoweza kuwapata watu kwa kweli, na ndio watu wanavyoweza kumpenda na kumwabudu Mungu kwa kweli. Inaweza kusemekana kwamba misururu ya mambo ambayo Bwana Yesu alisema na kufanya baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ya fikira njema, na kufanywa kwa nia njema. Walijaa huruma na huba ambayo Mungu alishikilia kwa binadamu, na akiwa amejaa pia na mapenzi na utunzaji wa makini Aliokuwa nao kwa minajili ya uhusiano wa karibu aliokuwa Ameanzisha na wanadamu wakati Akiwa katika mwili. Hata zaidi walijaa kumbukumbu za kitambo na tamaa Alilokuwa nayo kutokana na maisha Yake ya kula na kuishi miongoni mwa wafuasi Wake wakati akiwa katika mwili.
2 Hivyo basi, Mungu hakuwataka watu kuhisi umbali kati ya Mungu na binadamu, wala Hakutaka wanadamu kuwa mbali na Mungu. Hata zaidi, Hakutaka wanadamu wahisi kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hakuwa tena Bwana ambaye alikuwa wa karibu na watu, kwamba Hakuwa pamoja tena na wanadamu kwa sababu Alirudi katika ulimwengu wa kiroho, alirudi kwa Baba ambaye watu wengi wasingeweza kumwona wala kumsikia. Hakutaka watu kuhisi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote katika cheo kati Yake na wanadamu. Mungu anapowaona watu wanaotaka kumfuata lakini wanamweka katika umbali fulani, moyo Wake unapata maumivu kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba mioyo yao iko mbali sana na Yeye, inamaanisha kwamba itakuwa vigumu sana Kwake yeye kuweza kuipata mioyo yao.
3 Yote haya ambayo Bwana Yesu alifanya yalimfanya kila mmoja aliyemwona Yeye kuhisi kwamba Bwana hakuwa amebadililika. Hata ingawa Alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia kifo, Alikuwa amefufuliwa, na hakuwa amemwacha binadamu. Alikuwa amerudi kuwa miongoni mwa wanadamu, na kila kitu Chake hakikuwa kimebadilika. Mwana wa Adamu katika njia hii aliwaruhusu watu kuhisi upendo huo, kuhisi kuwa watulivu, na kuhisi furaha ya kupata tena kitu ambacho kilikuwa kimepotea, na wao pia walihisi watulivu kwa njia tosha ya kuanza kumtegemea na kumtumainia Mwana huyu wa Adamu kwa ujasiri na kwa imani ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Walianza pia kuomba katika jina la Bwana Yesu bila ya kusita, kuomba ili kupokea neema Yake, baraka Zake, na kupokea amani na furaha kutoka Kwake, kupata utunzaji na ulinzi kutoka Kwake na kuanza kutenda uponyaji na kupunga mapepo kwa jina la Bwana Yesu.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili